Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Wanabodi,

Leo siku ya Machi 17 ndio siku Taifa tulipotangaziwa kifo cha Shujaa wetu JPM, hivyo katika kumkumbuka, na kumuenzi, mnaonaje tukijikumbusha baadhi ya mabandiko ambayo tulimshauri JPM na ushauri huo ukafanyiwa kazi, kwa kutaja Bandiko, ulishauri nini, na nini kilikuja kufanyika kwa ushauri huo, na jee kulisaidia JPM? Kulisaidia nini?

Kwa vile JPM alikuwa ni mbabe kwa kufanya baadhi ya mambo kibabe, hadi kutafsiriwa ni dikiteta, hivyo baadhi ya ushauri kwa JPM pia ulitolewa kibabe kwa kumpiga Spana za kutosha, ila tukubali tukatae, Spana za JF zilimsaidia sana JPM na kulisaidia taifa.

Kumuenzi JPM, naomba tujikumbushe baadhi ya mabandiko, tuliwahi kushauri nini kwa kuandika nini na kutoa ushauri wa nini kifanyike, na kufuatia ushauri huo, nini kilifanyika na jee kilimsaidia JPM?kilimsaidia kivipi?. Jee kililisaidia taifa?, kililisaidia kivipi?

Hili ni moja ya mabadiliko hayo ambalo limemsaidia sana na kulisaidia taifa.

Na mwisho kwa vile sasa Samia ndie Rais wetu, JF tunapaswa kuendelea kutimiza wajibu wetu kwa kumsaidia Samia, kwa vile JPM alikuwa ni rais mbabe vivyo hivyo ushauri ulitolewa kibabe, lakini Samia no Mtaratibu, mstaarabu, jee licha ya utaribu na ustaarabu, Mama Nate tumpige Spana kama za JPM? au twende naye taratibu kama alivyo, kwa Mama iwe ni kumkuna tuu, na tusimpare kama alivyo shauri mwenyewe, kuwa ukinikuna vizuri nitakukuna ila ukinipara, nitakuparua?

Mabandiko mengi ya kuwakumbuka marehemu huishia kwa RIP kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi kwavile wanakuwa hawajui marehemu yuko wapi,, lakini mimi kwa vile tayari nimeisha kulishwa JPM yuko wapi Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani bado kuna haja ya kuendelea kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi huku tayari najua yuko peponi?.

Pumzika Magufuli Pumzika! Tutakukumbuka Daima!

Paskali!
 
Maisha ni kama hadithi tu, basi ewe ndugu yangu kuwa hadithi nzuri kwa hao watakaosimuliwa, niliwahi kumsikia Alhaj Ali Hassan Mwinyi (Raisi wa awamu ya pili) akisema.
 
Nilichojifunza kwenye maisha, ukitaka kuishi vizuri na watu hata viongozi wako, always have less expectations. Expect less From them.

Samia ameweza kuachieve vitu ambavyo ngosha mwenzangu alitumia nguvu kubwa sana Na hakufanikiwa. Mfano upinzani ni ideas. You can’t simply wish them away hata ungewapiga risasi wote. Ni nuisance ambayo huna budi kuishi nayo kwa akili. Kikubwa jifunze kuimanage vizuri. Samia has done exactly that. She is happy. Wapinzani are happy…na maybe mabeberu wako happy. Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana. 2025 akiwapa hata 20% ya viti vya ubunge….she will be regarded as an icon of democracy in Africa. Siasa ni sayansi. Lakini sayansi siyo siasa.

Ngoja mama yetu wa Kizimkazi atufunze siasa! tulichelewa sana!
 
Mwendakuzimu mlimuabudu Sana Yule Ibilisi
Mungu aendelee kumuweka Motonia
 
Mzee mwenzangu, Mimi JPM ndo alinifunza niwe na less expectations na viongozi /binadamu wenzangu. Huyu bwana just alivokuwa, he would have achieved a lot kwa hili taifa letu. He had everything he needed BUT hakuwa na karama ya kuongoza wengine. Hakuwa mvumilivu. Hata pale pasipohitaji nguvu, alitumia nguvu kubwa Sana. hata Nyumbani baba anayefokafoka, na kutosikiliza ushauri wa watoto na mwenzi wake, ni ngumu kulea familia kwa mafanikio.

Mama Samia hajafanya lolote extraordinary. Lakini, amejifunza art ya kuongoza wenzake. Huyu mama bado atawashangaza watu. Wait and see.

Ogopa sana mtu asiyependa kukosolewa. Muogope mnoo. Kwangu Mimi JPM is the President we all dreamed of, but we never had.

JPM ni Kiongozi wengi tulitamani kumpata, bahati mbaya hatukubahatika.
 
Mkuu Masanja nakuunga mkono 100% chini ya 100% na ndio maana lile tukio kikatokea!.
P
 
Mkuu Masanja nakuunga mkono 100% chini ya 100% na ndio maana lile tukio kikatokea!.
P
You don’t win by suppressing your opponests. You win by artfully empowering them. hili ni somo kubwa sana kwenye maisha.

Paskali hawa wazee unakunywa nao beer, uwe unawapa darasa Mara moja moja. Vingine ni inadequacy ya exposure.
 
You don’t win by suppressing your opponests. You win by artfully empowering them. hili ni somo kubwa sana kwenye maisha.

Paskali hawa wazee unakunywa nao beer, uwe unawapa darasa Mara moja moja. Vingine ni inadequacy ya exposure.
Kiukweli tumewasaidia sana haswa yule Blaza wangu!, wengine hata uwasaidie vipi, hawasaidiki, mtu mkimwambia pita njia hii ndio salama huku kunashimo utatumbukia, halafu ukisikia alipita njia ile ile na ametumbukia!, unaumia sana maana you tried to help!.

Ndipo nikagundua kuna watu usiishie tuu kuwaambia, tuu kwa sauti, hawasikii!, wabananishe, washike mkono waelekeze, pa kupita, wakiisha pita salama ndipo wachache huko mbele waendelee wenyewe, hivyo sasa huyu Mama hatumwachii, tunambananisha !.
P
 
Sometimes you have to be cruel to be kind.
 
Sometimes you have to be cruel to be kind.
It's very true baadhi ya mabandiko yangu ni very cruel!. Mfano bandiko hili Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini... mtu ni Spika, ili kumuepushia aibu unamshauri yeye asigombee na badala yake ampishe bidada, jamaa akagoma mwisho wa siku kang'olewa kwa aibu!.

Hata ile 2015 kule Zanzibar, nilishauri Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shein na matokeo ni kweli ila ZEC wakapindua meza!.

Hata huku bara 2025 nimeshauri Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
P
 
Magufuli aliletwa na Tume mbovu ya Uchaguzi kupitia Katiba ya hovyo na kutwaliwa na Kirusi cha Corona.

Acheni kumsingizia Mungu.
Mungu ndiye huweka serikali za mataifa, hata serikali za kidikiteta ni Mungu huruhusu ziwepo!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…