Wanabodi.
Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu Mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tu", na kama hiki tunachokiona sasa, sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja kweli ya kufanya tena uchaguzi wa rais? Si tumwache tu aendelee mpaka pale tutakaapoona tumetosheka?
1. Pamoja na ukanyagaji wake wa katiba ya nchi, lakini kwa kazi hii nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuinyoosha nchi hii iliyopinda kupindukia kwa rushwa, uzembe na ufisadi, hivi kweli Tanzania, tuna haja tena ya kufanya uchaguzi wa rais kwa mwaka 2020?, au tumwache tu aendelee mpaka 2025? na kama bado anatosha, aendelee tu?
2. Je, hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, na kumwacha Magufuli kupita bila kupingwa, ili kuokoa muda, pesa na mali?, hivyo Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025 and beyond?.
3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike kwa mujibu wa katiba, hata kama uchaguzi huo ni wastage of time, money and resources? Kwani katiba ndio nini hata iheshimiwe hivyo?
4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa; je kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?
5. Kwani katiba ni nini? Si ni kipande tuu cha karatasi? Ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, ingekanyagwa kirahisi rahisi na kupuuzwa, huku watu wakiangalia tu? Nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?
6. Na Katiba ni ya nani? Ni yetu? Na iko kwa manufaa ya nani? Si ipo kwa manufaa yetu? Hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?
7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?
8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Kama katiba inakanywa na hakuna kinachofanyika, Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?
9. Na baada ya katiba kukanyagwa, kwa mikutano ya siasa kuzuiwa, jee kuna ubaya wowote kama wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, haswa kwa kuzingatia the playing field is not level, na badala yake CCM tuu ndio iwe pekee inatoa mgombea urais siku zote kufuatia long eksipirience ya uzoefu wa muda mrefu wa CCM wa kumtoa rais ambaye siku zote huchaguliwa kwa ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huru na wa haki?
10. Na kufuatia somo la demokrasia ya Kiafrika, na mfano hai wa matokeo ya urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea urais wa kushindana na mgombea wa chama dola, CCM, kwa Tume hii hii, na mazingira haya haya ukategemea kuna ushindani?, yaani by now tumeishajua mgombea wa CCM kwa 2020 ni Magufuli, bado kuna chama kiko tayari kumteua mgombea wake kushindana na Magufuli ambaye ni a sitting president, huku kutakuwa ni kugombea urais au kugombea ili kujifurahisha tuu?, ni kama kugombea kisu cha makali kuwili huku mmoja ameshika mpini, wengine kwenye makali kuwili, unategemea nini?, au hata ikitokea Mungu akafanya muujiza, huyo mgombea wa upinzani akashinda kwa muujiza wa Mungu, jee atatangazwa?.
Kwa maoni hakutakuwa na uchaguzi wa rais 2020, kutakuwa tuu na igizo la uchaguzi, uchaguzi mwingine wa rais ni 2025, only if...
Hayo ni maswali tu nimeanza kujiuliza aloud.
Je, wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?
Paskali