Swali la kujiuliza ni kuna haja gani ya kuwa hata na chaguzi ilhali tunajua kabisa mwisho wa siku CCM ndo atatangazwa mshindi?
Pasco ni mapema mno kuwaza haya.
Tumpongeze kwa kiasi fulani lakini pia tusisahau kuweka akiba ya maneno.
Safi sana naona umejisalimisha CCM nilidhani bado unazungusha mikono ukisubiri mabadiliko ya Lowassa.
...hili swali la msingi sana, hata wakimuondoa Magufuli kwa mizengwe kwenye chama chao, wakasimamisha kibuyu bado kitashinda tu, kwanza huyo Magufuli alishinda, au alishindishwa?!
Uzi wa kipuuzi.
uchaguzi mwingine wa rais tufanye 2035 aongoze kwa miaka 20 mfululizo.
Huwa nikiona comment za kuibiwa kura huwa nacheka sana...maana nakumbuka Lowasa aliwambia wapige kura kazi ya kulinda amwachie...!
Haikutosha makamanda walimsajili mtu aliye wadanganya kuwa yeye ni mtaalam wa kuiba kura lakini wapi...!
Pasco,
Kwanza nikiri wazi kwamba huwa naheshimu sana maoni ya watu. Pili huwa nafuatilia na kuvutiwa na hoja zako nyingi hapa jukwaani! Ila niseme ukweli leo umeongea kijinga sana kwenye hii hoja! Nasema kijinga kwa sababu bado unaweza kujielimisha,kuelimishwa na ujinga wako ukaondoka!
Tanzania hatufanyi uchaguzi eti kwa sababu Nchi haina uongozi mzuri ama kwa sababu hakuna kiongozi shupavu. Mpaka sasa anachokifanya magufuli sio kitu kigeni,kiliwahi kufanywa huko nyuma na waliomtangulia lkn bado tulilazimika kuingia ktk uchaguzi! Tulikuwa tunafanya uchaguzi tukiwa na mfumo wa chama kimoja, leo tunao mfumo wa vyama vingi unakuja na mawazo ya kijinga namna hii?
Ushamtema mamvi?
Sikushangai, nnaona umesalim amri kama wapumbavu na malofa wenzako wengi tu.
KAMA atafanya vizuri mimi sina shida kuiunga mkono CCM! Mimi sina chama ila ninataka uongozi mzuri! Naona mnatumia nguvu nyingi sana kumsifu Magufuli japo bado hajafanya chochote kipya. Mtaweza kucheza na bongo za wabongolala ambao hawana kumbukumbu. Alikuwepo Mrema na alitingisha kuliko Magufuli mara kumi... lakini uongozi wa kutegemea mtu badala ya mfumo haudumu na haubadilishi chochote!
Swali la kujiuliza ni kuna haja gani ya kuwa hata na chaguzi ilhali tunajua kabisa mwisho wa siku CCM ndo atatangazwa mshindi?