Kwa kauli hii, Rais Magufuli anakiri kuna mabaya yanafanyika chini ya utawala wake?

Sina mashaka kabisa na juhudi za Rais Magufuli katika utendaji kazi. Sina mashaka na dhamira yake ya kutaka nchi ipate maendeleo.

Pekee kubwa lililowaumiza watu wengi kwenye utawala wake ni hili kundi la wasiojulikana. Watu wanaoteka, wanaoua na kupoteza watu. Kundi la pili ni Polisi wanaowatengenezea watu makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.

Rais Magufuli ana nafasi nzuri zaidi ya kuheshimika na kupendwa kwa kutokujishughulisha na ulipizaji visasi au kuwakomoa watu wanaotofautiana naye. Wanaojifanya wanampenda, na hivyo kuwatesa na kuwapoteza wote wanaomkosoa, ndio wanaomtengenezea chuki kutoka kwa wananchi. Maana kwa mwanadamu, hata ufanye mazuri gani, hakuna linalozidi thamani ya uhuru na haki ya mwanadamu kuishi.

Anayeteka, anayetesa, anayepoteza au anayeua watu kwa sababu tu watu hao wamemkosoa au kumsema Rais, huyo ndiye adui mkuu wa Rais.
 
Huwezi kufanya mema wakati wote, kuna kuteleza kama binadamu na yeye anatumbua hilo, bila shaka.
Sent using Jamii Forums mobile app by My phone
 
Wachache sana tumekuelewa wengi hawawezi kukuelewa
Njaa ndio imezalisha wapiga vuvuzela wengi. Wengi wangekuwa wanajisomea historia kuna mapambio yangejifia kwa ni majukumu ya kawaida kabisa ya serikali.
 
Lakini pia JPM atashinda na kutangazwa baada ya kupata aslimia 20 ya kura zilizopigwa
 
Ivi mkuu unataka kusema wewe haupo huru? Tuachane na mambo ya chadema na mbowe!!! apo kinachoongelewa ni utendaji kazi wake na namna gani atakumbukwa meko siku akiwa hayupo madarakani

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunamkumbuka Baba wa Taifa kwa kutuletea uhuru. Majukumu ya kujenga barabara kila Rais amefanya kwa nafasi yake. Na wenzie wamejenga bila kuua watu wala kuwabambikia makesi na kuwanyang'anya hela kama yeye anavyofanya.
 
Wengine tunatumia akili kabla ya kuandika wakati wengine akili mmeacha maliwato. Kwa mfano kada ya madaktari, Mpaka 2015 madaktari wote walikuwa wanaajiriwa na Serikali halafu unataka kudanganya watu hapa kuwa eti huyu anatengeneza mazingira ya kuajiriwa miaka 4 baadaye. This is STUPID thinking. Mtu aliye graduate 2016 hajaajiriwa mpaka leo eti anasubiri SGR ikamilike mwaka 2026 ndiyo apate kazi. Watu wengine shule hazijawasaidia kabisa
 

Pascal,
Karma; kama ilivyo imani zingine katika nguvu za giza - psychic powers - mfano, madai ya uwezo wa kusoma akili za watu (telepathy), madai ya kujua mambo yajayo (clairvoyance) na ramli (occult); ni imani ya ushirikina.

Karma is a superstition. It is an irrational/unscientific phenomenon.It is not a result of reason or causality (as you claim).

ili hili jukwaa lisiwe mahali pa kufagilia imani za kishirikina, tukubaliane katika hii kanuni: tujiepushe na kutetea vitu ambavyo haviwezi kielezewa kwa kutumia kanuni za asili (ie., phenomena that are inexplicable by laws of nature).
 
Hakuna anyemuangusha.
 
Mshi
jamaa anapiga kazi na ana ndoto nzuri tu! Tatizo liko kwenye kikosi! Muda mwingine nawaza! Hivi kulitumikia taifa ndani ya serikali ni mpaka uwe mwanasiasa!!? Kuna wazee navijana wamejazana nadhani mshua angewatumia tu kwa manufaa ya taifa!
 
Nakubaliana na wewe....nimeangalia clip ya kukagua daraja pale kilosa leo....wale viongozi wa tan roads yaani wote vitambi tupu..watafanye kazi katika Hali ile??!! Shame on them..
 
Uzi tayari ,pathetic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…