LGE2024 Kwa kauli hii ya Amos Makalla ya "Mwana CCM ukishapiga kura, rudi nyumbani", Upinzani jiandaeni kwa virungu vya polisi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Huu ni mtego kwa Wapinzani kupigwa virungu na Polisi, wakati vyama vya CHADEMA na ACT Wazalendo wakisema baada ya kupiga Kura wafuasi wao wakale kisha warudi vituoni kulinda kura upande wa CCM kupitia Amos Makalla, amesema Mwana CCM akishapiga Kura arudi zake Nyumbani.

Soma, Pia:
Mwenyekiti wa CHADEMA Katavi: Ninawaomba muwe na hasira mlinde kura zenu na polisi wakija msitishike na mabomu!
Ezekiah Wenje: Siasa sio ya Kubembeleza, CCM tutaenda nao Mperampera. Ukishapiga kura linda kura

==

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Amos Makalla, amewataka wanachama wote wa CCM kutolinda kura pindi watakapomaliza kupiga kura, bali warudi nyumbani kupumzika.

Akiwa Kata ya Mwananyamala jimbo la Kinondoni, Makalla amesema wanawaamini mawakala wao na ndio maana hawatalinda kura.
 
Huo ndiyo ustaarabu katika demokrasia, piga kura, rudi nyumbani kuskilizia matokeo.

Kuganda kituo cha kupigia kura hali ya kua hauhusiki tena, ni kiashiria cha fujo na vurugu.

Na kwahivyo utachukuliwa hatua muhimu za kukudhibiti ikiwa ni pamoja na kuchezea virungu vya maana vya polisi, ili iwe fundisho kwako na kwa wanaopanga kufanya vitendo viovu kama hivyo.

Aidha, nawatakia nyot uchaguzi mtulivu na wa Amani kwenye maeneo yenu kesho 🐒
 
Chadema kwa kulalamika 🙌
Kwan sheria c ndo inataka hvy ukishapiga kura uondoke eneo la tukio au?
 
Tunatest mitambo ya 2025

Maana 2025 tutagawana mbao

Since 2019 CCM wanachezea sharubu za amani
 
Asante mama kwa kuwapa polisi virungu vipya
 
Maandalizi ya wizi wa kura, polisi waache kuingilia Siasa wawaachie wana Siasa kazi zao.
 
Huu ni mtego kwa Wapinzani kupigwa virungu na Polisi, wakati vyama vya CHADEMA na ACT Wazalendo wakisema baada ya kupiga Kura wafuasi wao wakale kisha warudi vituoni kulinda kura upande wa CCM kupitia Amos Makalla, amesema Mwana CCM akishapiga Kura arudi zake Nyumbani.

Soma, Pia:
Mwenyekiti wa CHADEMA Katavi: Ninawaomba muwe na hasira mlinde kura zenu na polisi wakija msitishike na mabomu!
Ezekiah Wenje: Siasa sio ya Kubembeleza, CCM tutaenda nao Mperampera. Ukishapiga kura linda kura

==

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Amos Makalla, amewataka wanachama wote wa CCM kutolinda kura pindi watakapomaliza kupiga kura, bali warudi nyumbani kupumzika.

Akiwa Kata ya Mwananyamala jimbo la Kinondoni, Makalla amesema wanawaamini mawakala wao na ndio maana hawatalinda kura.
Ni lini wapinzani hawakupigwa virungu?
 
Back
Top Bottom