Pre GE2025 Kwa kauli ya DC Mbeya, maandamano ya CHADEMA yanafanyika sababu Rais Samia ameruhusu na sio kwa sababu ya Katiba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tymejaliwa viongozi wapumbavu wengi.

Ukiwa na akili zako unapoteza sifa za kuwa kiongozi
 
Tymejaliwa viongozi wapumbavu wengi.

Ukiwa na akili zako unapoteza sifa za kuwa kiongozi
Hawana ubavu wa kuamua jambo wenyewe. Chadema wataandika barua ya kuomba kuandamana, RPC atamuuliza IGP ikiwa wawaruhusu, na IGP atamuuliza waziri mambo ya ndani ikiwa wawaruhusu. Waziri mambo ya ndani atamuuliza waziri mkuu ikiwa wawaruhusu, waziri mkuu atamuuliza raisi ikiwa wawaruhusu. Na labda raisi atamuuliza katibu mwenezi wa CCM, huwezi kujua!
 
Tanzania tunapaswa kufanya mambo yetu kwa taratibu za kikatiba, sio utashi wa mtu mmoja mmoja hata kama mtu huyo ndio Raisi wa nchi, au waziri,au IGP au Katibu mwenyezi wa CCM nk. Namna hiyo ya uongozi haitatufikisha popote.
Naunga mkono hoja. Siku mikutano ya siasa na maadamano yaliporuhusiwa nilisema mikutano ya vyama na maandamano ni haki na sio hisani!, haki ni kitu stahiki na sio hisani!, nikauliza Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
P
 
Ccm imejimilikisha Tanzania hivyo wanafanya watakavyo, hiyo katiba haiwazuii kutofuata.
 

Kutokana na ubovu wa katiba yenyewe ni kweli haya maandamano ni ruhusa ya rais, na anaweza kuyazuia na yasiwepo bila kujali katiba inasema Nini. Kwa Sasa amri kutoka juu ina nguvu kuliko katiba na Sheria. Na kama katiba itaendelea kuwa hii hii, akija mwanaccm mwingine kuwa rais, atasitisha maandamano na atasema Kila zama na kitabu chake.
 
Hao ndio aina ya watawala tulio nao na ndio maana Taifa tunakosa kutoka hapa tulipo!
 
Umesema kweli kabisa mwamba! Tuna viongozi wapumbavu sana!
 
 

Attachments

  • VID-20240430-WA0014.mp4
    2.4 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…