Pre GE2025 Kwa kauli ya Nape kuhusu chaguzi zetu, anastahili kulaumiwa au kupongezwa kwa kuusema ukweli?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sidhani kama anahitaji pongezi, yeye ni wa upande huohuo. Aliongea kama dhihaka, kebehi na majivuno. Sema ni Tanzania, ingekuwa nchi inayojielewa kuanzia Mwenyekiti mpaka nafasi ya mwisho walitakiwa waachie hizo nafasi.

Kila mara vyama vya siasa, wananchi na Asasi mbalimbali wanalalamikia hilo, leo mtu anakiri hadharani na hakuna kinachofanyika mnataka apongezwe si sawa. Tz ni wanyonge ila hili mtazidi kunyongwa sana.
 
Unajua faida ya Demokrasia - Hata kama ni uongo inaleta ile illusion kwamba hizi pumba tulizichagua wenyewe kwahio ngoja miaka mitano ipite tuchague tena hence inafanya watu wasifanye vurugu wakiamini kuna kesho

Sasa mtu mwenye dhamana ya kuendeleza haya maigizo akisema vinginevyo inaonekana kwamba tunatuma gharama kubwa kwenye haya maigizo na hio sio tu upuuzi bali ni lack of foresight....

Anyway nilishasema hapo awali...
 
Dharau tunazofanyiwa na viongozi wa CCM hazina mfano na bahati mbaya wananchi tunachekelea kama mazuzu! Nadhani kuna hitilafu kubwa sana katika mfumo wa elimu tunayoipata mashuleni.

Tunafundishwa unyenyekevu, nidhamu uoga na kusujudia viongozi badala ya kufundishwa maarifa na kujitambua utu wetu na kulinda Utaifa na haki!
 
Pascal Mayalla a.k.a NYANI MZEE
 
Mbona hujasema 2015 huku bara!!?lowasa alivyoshinda!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…