Pre GE2025 Kwa kauli ya Nape kuhusu chaguzi zetu, anastahili kulaumiwa au kupongezwa kwa kuusema ukweli?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
KKube
Kumbe ccm ni majizi ndio najua leo
Uwe na heshima na adabu, majizi ni yale yanayoiba vitu vya watu wengine, vitu vikiwa ni vya kwako mwenyewe, Huwezi jujiibia, ni unajichukulia tuu, unaweka, waa!.
Hii nchi ni yake, watu ni wake, serikali ni yake, Tume ni yake, na kura ni zake!, hivyo sio kuiba bali kujitwalia tuu kitu chako mwenyewe, unakifanya unavyopenda.
P
 
Hata Mimi nimeshangaa CHADEMa kumshambulia Nape wakati kasema ukweli mbele ya wananchi wa Bukoba
Hawa jamaa hawajitambui kabisa, wanataka nini, wanahitaji kusaidiwa sana ili kujitambua, akina sisi tunawasaidia sana tuu.
P
 
Pasco the ndumilakuwili.
Shilingi ina pande mbili, sio lazima uchague upande, sisi wengine fani zetu zinatutaka tuwe, truthful, neutral, na impartial, ukiwa mkweli, kwenye mazuri utapongeza ,mabaya utakosoa, wema na wabaya ni wale wale, sasa ukipongeza mazuri, ukaja kukosoa utaonekana ndumila!, mimi nimezoe, naendelea kutimiza wajibu wangu.
P
 
Hata Mimi nimeshangaa CHADEMa kumshambulia Nape wakati kasema ukweli mbele ya wananchi wa Bukoba
CHADEMA kazi yao ni kupinga kila kitu. Hata siku wakishinda uchaguzi watakataa
 
Tunahitaji umoja wa kitaifa, usawa wa binadamu na kuheshimiana.
Kauli ya Nape ni mbaya sana kwa binadamu wanaojielewa. Ni kama mwizi aibe mali yako, atambe kwamba nimekuibia, utanifanya nini.
Watu wenye akili wanajua kwamba ukila na kipofu usimshike mkono, sasa yeye kaona kwamba hata kumshika mkono ni sawa tu. Hii siyo habari ya ushabiki wa kijuha wa vyama bali ni kwa mustakabali mwema wa jamii na taifa kwa ujumla.
Lazima tuwe wastaarabu, hata dhambi tutende kwa ustaarabu ili Mungu atusamehe kwa sababu yeye ndiye asili ya ustaarabu wote (napunguza makali alivyomtaja Mungu kama siyo mungu).
 
Kweli Paschal akili Huna, kwa hiyo Mwizi akisema ukweli wake kuhusiana na ushiriki wake wa Wazi anapongezwa!
 
Nape ataendelea kushutumiwa, kulaumiwa, na kulaaniwa. Swali, ni kina nani watalaumu, shutumu, na kulaani?
information is power, Nape ni insider, hiyo info ni from deep inside, wanaomshutumu ni wasiojua the value of vital information. Sisi tunaojua, tunampongeza! Hata mwanga, ukimstukia na kumwambia wewe ni mwanga, hakuwangii tena!. Hivyo uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2025 unakuwa huru na wa haki. Hakuna tena bao la mkono!.
P
 
Kuilingana na kauli yake ni kwamba "CCM haijawahi kushinda tangu upinzani uanze" angalia wakati wa Mrema. Aliyeshinda ni upinzani ila mtangazaji akageuza. Awe macho sasa vijana wa Kenya wanatufundisha cha kufanya.
 
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na kwa maslahi ya taifa.

Nimenote Mhe. Nape, akilaumiwa, kushutumiwa na kulaaniwa kwa kauli yake kuhusu chaguzi zetu.

Huu ni uzi wa pongezi kumtia moyo, asilaumiwe, kushutumiwa na kulaaniwa kwa kauli yake hiyo kwasababu huo ndio ukweli wenyewe, wa chaguzi zetu!.

Ushahidi ni huu, Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Baada ya uchaguzi wa 2015, nilisema Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!

Hivyo hicho alichokisema Nape ni kitu cha kweli, badala ya kulaumiwa, Nape anapaswa kupongezwa na jina lake kuingizwa kwenye list ya mashujaa wa taifa hili kwa kuuweka wazi ukweli huu, hivyo itasaidia sana kutufanya tubadilike!. Big Up Mhe. Nape!.

Kiukweli kabisa wengi wa wanasiasa wetu ni watu malaghai!, wanaweza kusema uongo, mchana kweupe huku macho makavu kabisa bila hata Lepe!.

Ila kuna wanasiasa wachache ni mijitu very bold type ya Mhe. Luhaga Mpina, hawa watausema ukweli, no matter what, hata kama baadae wataomba msamaha by just paying lip service ,lakini ukweli unakuwa umejulikana.

Mhe. Nape Nnauye ni mmoja mmoja wa hao wanasiasa bold, truthful, bonafide and very genuine, alichokisema ndio ukweli wa kinachotokea kwenye baadhi ya chaguzi zetu!.

Badala ya kumlaumu na kumshutumu Mhe. Nape Nnauye, tunapaswa kumpongeza kwa kuisema hadharani siri hii, hivyo sasa ni fursa ya kubadilika, tufanye chaguzi huru na za haki.

Kwa vile haya mambo ni mambo ya kweli na yanafanywa sirini, kitendo cha Nape kuyatamka hata kwa jokes tuu, ni jambo jema na jambo la kheri la kutusaidia kubadilika na kuachana na hizi mambo.

Kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2020, nilitoa ombi hili mahsusi Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!

Kwa vile sasa the cat is out of the basket, haya mambo, tuyajadili kwa uwazi kwa lengo la kuyaepuka.

Pia tumpongeze Nape kwa kutoa jokes za ukweli, na zinapo backfire anakuwa ni mwepesi kuomba msamaha!.

Nape ndie muasisi wa maneno
"Kinyago ukichonge mwenyewe halafu kinakutisha".
"Bao la Mkono" na sasa hii
Kauli ya kuhusu uchaguzi.

Kichama kosa lake ni kuropoka ukweli wa kinachofanyikaga. Kitendo cha kutoa siri za chama za mbinu za ushindi wa uchaguzi, kichama ni kosa kubwa, ila ki haki, kibaraka, alichokisema Nape ni roho wa Mungu amezungumza kupitia Nape. Kauli hii inaweza kumponza Nape kwa kum cost his political carrier, lakini kwa kupigwa kwake, sisi tunaponywa na taifa linaponywa, tunabarikiwa.

Keep it up Mhe. Nape, sisi wakweli wote, tuko na wewe, tuko nyuma yako na tutasimama na wewe. Ukipaswa kuwajibika kwa kauli yako, wajibika tuu, na Mungu atakunyanyua na kukuweka juu palipo inuka!.

Naamini Mama ameisikia kauli hii, hivyo sasa hili ombi linakwenda kwa Mama, Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!
Tuziache hizi mambo, tubarikiwe, tuziendeleze na tuendelee ku ...

Mungu Akubariki sana.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
Hata wayahudi enzi za Yesu waliuchikia ukweli!Hasa mafarisayo wakidai Kwa Nini anaponya watu siku ya Sabato,lakini wao wakata wapate njia ya kumuua siku hiyohiyo ya Sabato!mmh,Mungu mwema tutafika tuu.
 
Nape anastahili pongezi kubwa, na mara zote kama hamjamsoma nape huwa analenga kuichafua serkali hasa Mama Abdul, nadhan hiyo nafasi anaitaka sana.

Kuna siku alisema ukipiga hata picha yako nzuri tu ukijipost usiache kutag "Nasimama na Mama", huu si uchawa ni Kejeri kubwa kumaanisha Upambe wa Mama Abdul umefikia hatua ya kuforce/aibu.
 
Nape asipigwe mayai viza anatufumbua macho!
Ndiyo maana serikali na CCM ukiwaambia suala la kuandika katiba mpya na tume huru ya uchaguzi wanafura balaa!!
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na kwa maslahi ya taifa.

Nimenote Mhe. Nape, akilaumiwa, kushutumiwa na kulaaniwa kwa kauli yake kuhusu chaguzi zetu.

Huu ni uzi wa pongezi kumtia moyo, asilaumiwe, kushutumiwa na kulaaniwa kwa kauli yake hiyo kwasababu huo ndio ukweli wenyewe, wa chaguzi zetu!.

Ushahidi ni huu, Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Baada ya uchaguzi wa 2015, nilisema Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!

Hivyo hicho alichokisema Nape ni kitu cha kweli, badala ya kulaumiwa, Nape anapaswa kupongezwa na jina lake kuingizwa kwenye list ya mashujaa wa taifa hili kwa kuuweka wazi ukweli huu, hivyo itasaidia sana kutufanya tubadilike!. Big Up Mhe. Nape!.

Kiukweli kabisa wengi wa wanasiasa wetu ni watu malaghai!, wanaweza kusema uongo, mchana kweupe huku macho makavu kabisa bila hata Lepe!.

Ila kuna wanasiasa wachache ni mijitu very bold type ya Mhe. Luhaga Mpina, hawa watausema ukweli, no matter what, hata kama baadae wataomba msamaha by just paying lip service ,lakini ukweli unakuwa umejulikana.

Mhe. Nape Nnauye ni mmoja mmoja wa hao wanasiasa bold, truthful, bonafide and very genuine, alichokisema ndio ukweli wa kinachotokea kwenye baadhi ya chaguzi zetu!.

Badala ya kumlaumu na kumshutumu Mhe. Nape Nnauye, tunapaswa kumpongeza kwa kuisema hadharani siri hii, hivyo sasa ni fursa ya kubadilika, tufanye chaguzi huru na za haki.

Kwa vile haya mambo ni mambo ya kweli na yanafanywa sirini, kitendo cha Nape kuyatamka hata kwa jokes tuu, ni jambo jema na jambo la kheri la kutusaidia kubadilika na kuachana na hizi mambo.

Kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2020, nilitoa ombi hili mahsusi Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!

Kwa vile sasa the cat is out of the basket, haya mambo, tuyajadili kwa uwazi kwa lengo la kuyaepuka.

Pia tumpongeze Nape kwa kutoa jokes za ukweli, na zinapo backfire anakuwa ni mwepesi kuomba msamaha!.

Nape ndie muasisi wa maneno
"Kinyago ukichonge mwenyewe halafu kinakutisha".
"Bao la Mkono" na sasa hii
Kauli ya kuhusu uchaguzi.

Kichama kosa lake ni kuropoka ukweli wa kinachofanyikaga. Kitendo cha kutoa siri za chama za mbinu za ushindi wa uchaguzi, kichama ni kosa kubwa, ila ki haki, kibaraka, alichokisema Nape ni roho wa Mungu amezungumza kupitia Nape. Kauli hii inaweza kumponza Nape kwa kum cost his political carrier, lakini kwa kupigwa kwake, sisi tunaponywa na taifa linaponywa, tunabarikiwa.

Keep it up Mhe. Nape, sisi wakweli wote, tuko na wewe, tuko nyuma yako na tutasimama na wewe. Ukipaswa kuwajibika kwa kauli yako, wajibika tuu, na Mungu atakunyanyua na kukuweka juu palipo inuka!.

Naamini Mama ameisikia kauli hii, hivyo sasa hili ombi linakwenda kwa Mama, Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!
Tuziache hizi mambo, tubarikiwe, tuziendeleze na tuendelee ku ...

Mungu Akubariki sana.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
 
Uwe na heshima na adabu, majizi ni yale yanayoiba vitu vya watu wengine, vitu vikiwa ni vya kwako mwenyewe, Huwezi jujiibia, ni unajichukulia tuu, unaweka, waa!.
Hii nchi ni yake, watu ni wake, serikali ni yake, Tume ni yake, na kura ni zake!, hivyo sio kuiba bali kujitwalia tuu kitu chako mwenyewe, unakifanya unavyopenda.
P
paskali leo umetafuna kavu kabisa. sijui kama ndiwe umejitoa kwenye koti lako tulilokuzoea nalo mtaani. bilashaka roho wa bwana yu aendelea kuyanyoosha mapito kuelekea nchi ya ahadi.

nabarikiwa sana na machapisho yako japo mengi ni magumu lakini yananijenga.

je vous felisté cher monsiur, ajoûte.
 
Watu weusi ndo,viumbe wenye upeo mdogo wa kufanya tafakari na kutenda.Maana namna jinsi walivyo ni "ishara ya upeo mdogo wa kufikili"Botha.

Mwafrika ameshindwa hata kusimamia jambo dogo kama la uchaguzi,alafu anawaza mageuzi ya kimfumo na kujikomboa toka kwenye utumwa wa fikra za kikoloni na wakati huo matendo yake ni Sawa na mtu asiye na ustaarabu.

"Hata umtwange mpumbavu na mchi kwenye kinu pamoja na ngano, upumbavu wake hauwezi kumtoka"Mfalme Selemani

"Mwafrika hawezi kujitawala" Botha

"Baadhi ya nchi kadhaa za Asia na Afrika ni Sawa na sehemu za kutolea haja kubwa"Trump
 
Back
Top Bottom