Kwa kauli za Masauni, Tanganyika tumekuwa koloni la Zanzibar

Kwa kauli za Masauni, Tanganyika tumekuwa koloni la Zanzibar

Bavicha hamtaachwa salama mkiendelea na chokochoko,tena Kauli kama hizi ndio tunazipenda
IBARA 4 (2) ya mkataba huu wa Kimangungo inasema endapo Tanzania inapotaka kuweka mwekezaji mwingine maeneo mengine ya bandari inatakiwa iende Dubai kuomba ridhaa, Dubai wakikataa kutoa idhini, ndio basi. Yaani nchi huru ikaombe ridhaa Dubai? Tena kwa mali zake? Ni kichaa peke yake ndio anaweza kuushabikia mkataba wa aina hii.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Anawaagiza polisi watushughulikie tunahaoji mkataba wa kuiuza tanganyika. Ni rasmi tanganyika tumekuwa koloni la Zanzbar.
Polisi msikubali Tanganyika iuzwe na wazanzibari. Tumieni akili zenu vizuri.
Sisimizi kamkaba tembo
 
Anawaagiza polisi watushughulikie tunahaoji mkataba wa kuiuza tanganyika. Ni rasmi tanganyika tumekuwa koloni la Zanzbar.
Polisi msikubali Tanganyika iuzwe na wazanzibari. Tumieni akili zenu vizuri.
Mbona na wewe una mumunya sasa!


Ungesema Tanzania/Tanganyika tumekuwa koloni la Waarabu. Jeshi liwe makini na mipaka yetu known and imagined!
 
Naona watu wanahusisha issue ya bandari na UCCM na uCHADEMA.Hii issue inahusu Tanganyika kuuzwa rasilimali zake.Bila kujali tofauti ya vyama ,Watanganyika inabidi tuungane kwenye hili!
Wao wanasema CC na NEC ya CCM imekwishabariki mali za Tanganyika kuuzwa, wanasahau kwamba huko huko CC na NEC ndiko walikojaa waZanzibari wakiamua mambo ambayo hayawahusu kabisa.

Kwa hiyo sasa wanaviamuru vyombo vya waTanganyika viwashughulikie waTanganyika wenzao. Akili mbovu ya aina hii utaiona Tanzania pekee.
 
Kama bado Mwalimu nyerere angekuwa bado hai angejishangaa maamuzi yake yakulazimisha muungano
Hapana.
Hakuwa na lengo la Muungano kama huuu tulionao sasa hivi.

Kwa hili ninakubaliana nawe kabisa kwamba angerudi leo, angeshangaa sana kilichotokea wakati akiwa hayupo.

Naamini kwa jambo kama hili lililopo sasa hivi angetamani kuwacharaza viboko hawa waliotupeleka huko.
 
Bavicha hamtaachwa salama mkiendelea na chokochoko,tena Kauli kama hizi ndio tunazipenda
Hamad Masauni alifukuzwa UVCCM kwa kashfa ya kufoji umri ili aendelee kukalia kiti , Alipunguza umri wake kwa miaka 6 zaidi .

Huyu ndio ataisumbua Bavicha ? na ukileta ujinga nitamuanika Zaidi .
 
Back
Top Bottom