Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
BRADLEY Lowery ni jina ambalo limemea kwenye fikra za wapenda soka kote duniani. Kijana huyu mdogo, umri wa miaka SITA (6) alifariki dunia juma lililopita tarehe 07/07/2017 kwa maradhi ya Saratani akiwa mikononi mwa Baba na Mama yake. Huzuni iliyoje!
Hii leo ilikuwa siku ya kumuaga, na kumpumzisha katika makazi yake ya milele. Mashabiki wa soka nchini Uingereza, kwa wingi wao wameusindikiza mwili wa Malaika huyu mpendwa, "Shujaa Wetu Angani" ni kichwa cha utenzi kilichoimbwa kwa hisia na Mama Yake Mzazi, Gemma wakati wa kumuaga kanisani.
Gari lililobeba mwili wa Bradley, Shabiki Shujaa lilipungiwa mkono na mamia ya watu waliosimama pembeni mwa barabara kuelekea katika Kanisa la Blackhall Colliery, huko Country Durham.
Rafiki yake mpendwa, Nyota wa Sunderland Jermain Defoe amekatisha kambi ya mazoezi kujiandaa ya msimu mpya ili kuhudhuria mazishi ya Rafikiye Kipenzi. Watu waliombwa kuvalia mavazi ya rangi nyeupe na nyekundu, rangi zitumikazo na klabu ya Sunderland, ambayo Bradley alikuwa mnazi mkubwa kama heshima yake ya mwisho.
PUMZIKA KWA AMANI, BRADLEY.
YHWH IS GOOD