Kwa kianzio cha bajeti ya 25M, naweza kufikia hatua gani ujenzi wa nyumba ya vyumba 4.

Sawa mkuu.
Hiyo hatua tunapambana nayo mbele kwa mbele mtu ukiwa ushahamia kabisa
 
mkuu room 4 ujengee tofar 3500? sirias
utumie cement 100 sirias, unajenga ama unapaka paka cement.

kwa maelezo ya mtoa mada nyumba yake inataka SPACE yaan room kubwaa, siting ilioshiba
Kwani mtu akisema kubwa, we unachukuliaje? Ametaja vipimo mpaka uogope? Vyumba vitakuwa na ngapi, 3.6x3.9? 4×4? Sebule itakuwa ngapi, 7×7?

Tofali 3,500 ni chache? Inategemea, labda kama unafanya castle!

Cement mifuko 100 ni michache? Kwani unafyatulia tofali?

Chukulia nyumba ina 14 × 16
  • Tofali nyingi sana zitakuwa 4,000, kozi 15 kuanzia msingi, na hapa ni hujakata matundu ya milango na madirisha.
  • Cement mifuko 80 max, boma linasimama.

Sasa, nyumba ya vipimo vya 14×16 ni kuuubwa tu.

Nimeone nyumba yenye ukubwa wa 18m × 19m, kwenye mteremko kidogo, imeingia tofali 6,500; upande mmoja wa msingi ziliingia kozi 12.
  • Zingatie hiyo 18×19 kuwa sio kiwanja, ni nyumba!
  • Kiwanja cha 18×19 unatoa nyumba ya room 3 na parking space unapata!

So, bado naamini mambo sio magumu hivyo unavyoona!
 
Unahamia na kubakiza finishing ndogo ndogo
 
Kwa hili hitaji la moyo wako liko sahihi kabisa.
Kuna ngeni kuja unawaza.
Nimekupata basi komaa nakuomba ndoto yako ufanikishe maana Maisha yetu ni kula kulala na kuzaliana so ukiyapatia hayo matatu utastawi siku zote za maisha yako
 
CC: Alvin
CC: Alvajumaa
 
Vifaa vya ujenz vmepanda bei si utani, unahitaji kufanya tathimini kabla ya kuanza ujenzi usije ukaishia njiani. Kila la heri......pili mimi si muumini wa nyumba kubwa saana, watoto wakienda mnabaki ww na mkeo nyumba inawelemea. Jenga nyumba ya "saizi" hata kwa baadae ukiamua kuipangisha iskuletee changamoto ya kuja kuikata kati wakati hyo pesa ya kuikata kata huenda ungesimamisha chumba kingine cha uani kwaajili ya mabachela.
 
Nakubaliana na wazo lako la kutoa kuwa muumini wa nyumba kubwa, ila hili wazo lako naona linawafaa zaidi watu ambao tayari wana familia zilizosimama na wala si yule anayeanza au yuko mwanzo wa kujenga Familia.

Kuanzia sasa hadi mtoto wa kwanza aje aanze kujitegemea itapita miaka 25, sasa wakati akiwa nyumbani unataka tubanane kwenye nyumba ndogo maana atakuwa na wenzio pia(watoto wenzake), hili suala la kubaba ndio silitaki.

Nimeplan kujenga nyumba ya kueleweka then ishu ya kujenga iishe na zifuate issue zingine za maendeleo.
Kila mtu ana plan zake, hivyo hizi ndio plan zangu
 
Wee jenga nyumba kubwa watoto wenyewe siku hizi mpaka waje kutoka nyumbani wana miaka 30. So utamuwa nao home tuu hapo wana waya waya wakati wanatembeza bahasha.

Alafi sikukuu kama hivi wakija wanajiachia ndani ya mjengo wa dingi bwana. Nyumba vyumba vinne ni standard kabisaaa
 
Asante mkuu kwa kuunga mkono mawazo yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…