Kwa kianzio cha bajeti ya 25M, naweza kufikia hatua gani ujenzi wa nyumba ya vyumba 4.

Acha uoga kopa japo kidogo angalau 20m, kwa sababu inaonekana kipato chako ni kikubwa
Bado sijaona ulazima wa kukopa kwa sasa, labda siku za usoni na siombei hilo litokee sababu mikopo inaumiza kwa muda mwingine kwa mtu ambaye hajainuka kiuchumi.
 
Mkuu...kweli Duniani wawili wawili...

Nilitaka kuanzisha uzi wa namna hii tofauti ni eneo tu....mimi eneo ni Dar huku...kiwanja ni Flat labda wataalam waje watoe makadirio kuna mmoja kasema hapo naishia kwenye msingi ramani hii hapa.
 

Attachments

  • LASTANZA (7).jpg
    2.5 MB · Views: 10
  • LASTANZA (8).jpg
    2.4 MB · Views: 8
Karibuni Nile house 🏠 🏠 designs!!

kwa sasa tumeboresha huduma zetu Ili kukufikia mteja zaidi, tunatengeneza michoro na muonekano (3d) wa nyumba, majiko, sebule, bars, mandhari( landscape ) na huduma yoyote unayotaka kuanzisha,
Wasiliana nasi Leo tukupe huduma unayohitaji,

Call/Whatsapp 0715477041
 
Bro usiogope mim nimejenga vyumba 3 ila nyumba kubwa san, saiv najipana na usaf
 
Vyumba vinne hapo boma tu litakula;
20M (For best quality housing)
15M (for standard quality)
10M (for poor quality)

Ila kwa maelezo yako nazan unataka kitu quality so ni wewe uamue unajenga vipi

I'm talking from experience
Mkuu, boma bila hata kupaua ndio likale milioni 25 😳😳
 
Inategemea na ukubwa wa nyumba na ujenzi huo unafanyika mkoa gani
 
mkuu room 4 ujengee tofar 3500? sirias
utumie cement 100 sirias, unajenga ama unapaka paka cement.

kwa maelezo ya mtoa mada nyumba yake inataka SPACE yaan room kubwaa, siting ilioshiba
Hata mm nimepata shock humu kama hujui nyamazq ujifunze hyo ni tofali 5500 mpk 6000 kwengine sitaki kuingia
 
jamani eeeh chumba cha 4 x 3.5 m knakula tofali ngapi?
 
JF tunazidiana uwezo. Kuna mtu million 25M ni hela ya msingi mpaka finishing. Mwingine in pesa ya boma na kupaua. Mwingine ni pesa ya boma. Mwingine 25m, hata msingi haitoshi. Ndo maana kila mtu ana Ushauri wake.

Ukichangia nyuzi za ujenzi na magari humu JF, siku zote weka angalizo kwamba unachangia kulingana na kipato chako. Kuna watu mpaka adundulize aipate hiyo 25m ni shughuli pevu sana. Unadunduliza kununua gari ya 25m, wakati kwa wengine hiyo hata ushuru haitoshi. Ndo uhalisia wa maisha.

Ukichangia nyuzi za ujenzi na magari humu JF epuka hizi kauli, “mtanzania wa kawaida”, “mtanzania halisi”, vipato vya walio wengi” nk. Wewe pambana na Hali yako. Mtanzania wa kawaida hajulikani.

Siku zote; maisha yako ni ndoto ya wengi.
 
Kwenye mazingira kama ya Chanika,Mlandizi au Bagamoyo kwenye aridhi ya kichanga isiyozalisha nyufa Mil 25 Iinatosha kujenga na kupaua.. maana hauhitaji nondo nyingi km unajenga kwenye maeneo yenye udongo wa kinongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…