Kwa kilichotokea leo kwenye kesi ya Mbowe na wenzake watatu ni vyema IGP Sirro akajiuzulu mapema sana

nyboma

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2021
Posts
2,308
Reaction score
7,366
Kwa ufupi tu ni kwamba Kesi ya Mh. Mbowe tangu ianze kuunguruma hadi leo hii kitu nilichojifunza kwa Jeshi letu la polisi linaongozwa kihuni,kikatili na ubabe usio na ulazima kwa maagizo ya IGP NYAKORO SIRRO.

Pia jeshi la polisi limejaa askari wajinga, bumbumbu wa sheria na hata ufahamu wa maisha ya kawaida kwa ujumla.

Ni muda sasa wa Mh. Raisi kumteua IGP mpya atakayesimamia vyema sheria ya jeshi la polisi na kuwaongoza vyema askari wake wasiendelee kutumia ubabe kuonea watu hovyo na kuwabambikia watu hivyo kesi pasipo kuwa na ushahidi wa kutosha.

Kwa ile press aliyoitisha SIRRO kumnanga Mh. Freeman Mbowe hadi muda huu nitapoandika hapa hakutakiwa kuwa ofisini.
 
Wa kumwajibisha IGP naye anatakiwa kuwajibika sababu alishatoa hukumu kwenye vyombo vya habari kabla ya mahakama. Wanachezea kodi za watanzania bila woga kabisa.
Kwenye food web SIRRO ni secondary consumer Mama Samiah Ni tertiary consumer kwa namna yoyote ile lazma aondoke kumlinda Boss wake..
 
Ilikuwa ni kipindi cha uchaguzi mkuu
Alifanya vile kwa maagizo ya SIRRO pamoja na DIWANI ATHUMANI hawa watu inabidi wawajabike katika nafasi walizopo kwa sasa.

Wanatumika kumhujumu Mh. Rais waziwazi kabisa
 
Kwa ufupi tu ni kwamba Kesi ya Mh. Mbowe tangu ianze kuunguruma hadi leo hii kitu nilichojifunza kwa Jeshi letu la polisi linaongozwa kihuni,kikatili na ubabe usio na ulazima kwa maagizo ya IGP NYAKORO SIRRO.

Pia jeshi la polisi limejaa askari wajinga, bumbumbu wa sheria na hata ufahamu wa maisha ya kawaida kwa ujumla.

Ni muda sasa wa Mh. Raisi kumteua IGP mpya atakayesimamia vyema sheria ya jeshi la polisi na kuwaongoza vyema askari wake wasiendelee kutumia ubabe kuonea watu hovyo na kuwabambikia watu hivyo kesi pasipo kuwa na ushahidi wa kutosha.

Kwa ile press aliyoitisha SIRRO kumnanga Mh. Freeman Mbowe hadi muda huu nitapoandika hapa hakutakiwa kuwa ofisini.
Huenda IGP akakata rufaa kesi ya Mboye iendelee
 
atakuja IGP mpemba hapa...yakheee hana kosa huyoo....."tutajua hatujui"
 
Kikubwa mbowe ametoka bei za bidha na chakula zitapungua bei jamni Mana wakutusemea alikua hayupo
 
Back
Top Bottom