Kwa kilichotokea Zanzibar kuhusu kula hadharani Serikali ipige marufuku maafisa wa Serikali kukimbilia vyombo vya habari kutoa ufafanuzi, DPP ajiuzulu

Kwa kilichotokea Zanzibar kuhusu kula hadharani Serikali ipige marufuku maafisa wa Serikali kukimbilia vyombo vya habari kutoa ufafanuzi, DPP ajiuzulu

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Napongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar KULAANI waliojichukilia sheria mikononi wakidai kupiga marufuku kula adharani

Ningependa pia yule mtalii aliyetuzwa fedha arejeshewe fedha zake na wale waliokamatwa na polisi waachiwe huru.

Wakati huo huo jeshi la polisi lifute kauli yake na DPP Zanzibar ajiuzulu kwa kudanganya umma kwamba kuna sheria inayokataza kula mchana huku akijua anachofanya hakipo kisheria na kinachochea mpasuko.

Mwisho waliotetea jambo hili waone aibu kwa kutokuwa na fikra huru....funga yako isiwe kikwazo kwa wengine
 
Walishawahi kupiga mtalii mmarekani mweusi alikuwa akitembea usiku ati hilo ndio kosa!,walimcharaza mikwaju akijitetea wao wanasema unajifanya hujui Kiswahili leo utasema tu!.

Waliofanya vile walikiona maana mtalii alienda kushitaki ubalozini!.

Mji wakitalii lakini wenye mji wao hawajapambazuka kifikra!,mtu wa bara wanakuona kama umeenda kuharibu mji wao!, hizi dini zenyewe sio zakwetu na hata hao wenye dini zao hawatuheshimu waafrika,waarabu ni watu wabaguzi sana hata hao walioshikiria dini yao wanalijua hilo.

Mindset za ovyo kuna watu hawatufai karne hii ni fikra primitive sana kumzuia mtu kula kisa mfungo wako!.
 
Polisi wanahitaji kuzijua Sheria vizuri Si kupelekeshwa na vikundi vya kidini ndani ya Serikali.
 
Serikali ya Mapinduzi iachane na kuenforce sheria za Allah sheria za Allah aachiwe Allah mwenyewe kama atatuma Malaika wake nk.

Mbona huku Bara Waisilamu hawalazimishwi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwamba Wafunge au wasile chakula chao mpaka wajifungie uvunguni.?

Dini hailazimishwi.
 
slavery-french-magazine-illustration-of-arab-slave-traders-with-their-BDP7JC (1).jpg

Tumejikomboa kutoka kwenye hili👆

Bado kwenye hili👇
mental-slavery-illness-brain-that-260nw-2190979847.jpg
 
Jamii Check wametoa ushahidi kwamba ile video ni ya 2017, na hata hapa JF iliwahi kuwekwa hiyo 2017, na wametoa hadi link hii ya Youtube ikionesha ni ya 2017. Sasa ikiwa kila ikifika wakati kama huu hiyo video iwe inafufuliwa kuonesha kwamba ni tatizo la "leo", tutafika wapi kama taifa?
na polisi wanakamata wtu wanaokula hadharani mwaka gani?
 
Walishawahi kupiga mtalii mmarekani mweusi alikuwa akitembea usiku ati hilo ndio kosa!,walimcharaza mikwaju akijitetea wao wanasema unajifanya hujui Kiswahili leo utasema tu!.
Kwani watu huwa wanafunga usiku? hii chumvi nyingine imezidi tena.
 
Napongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar KULAANI waliojichukilia sheria mikononi wakidai kupiga marufuku kula adharani

Ningependa pia yule mtalii aliyetuzwa fedha arejeshewe fedha zake na wale waliokamatwa na polisi waachiwe huru.

Wakati huo huo jeshi la polisi lifute kauli yake na DPP Zanzibar ajiuzulu kwa kudanganya umma kwamba kuna sheria inayokataza kula mchana huku akijua anachofanya hakipo kisheria na kinachochea mpasuko.

Mwisho waliotetea jambo hili waone aibu kwa kutokuwa na fikra huru....funga yako isiwe kikwazo kwa wengine
Huko Zanzibar maafisa wengi ni waswahili waswahili tu, proffessionalism hakuna.
 
Back
Top Bottom