Kwa kina dada tu; ingekuwa wewe ungefanyaje?

Maneno utageuziwa ukikurupuka... wanaume wangapi walitoka nje ya nyumba zao na mke akatulia (it is not right but ndio reality kua wanaume mara nyingi hawajatulia)... Kama najua kabisa it is a good marriage, kweli rafiki yangu SITAMHUSISHA katika hili for najua maumivu yake ni intensive... naamini kua ukingoea nae (huyo shemeji) ni rahisi kukuelewa kulika hata ukitaka uingilie kati....

Katika hili lolote la weza happen... kama ni mwanaume jeuri najua anaweza geuza kibao na akasema hayo in blue... But bora hilo kuliko kuivunja hio ndoa.. for believe me you kama akanisingizia (huyo mwanaume) na ndoa yao ikawa bado intact; then at the end of the day it was worth it....

Usimkatishe uhondo, mwache akamalizane na chombo kipya, kisha baada ya siku mbili utamtafuta na kumuonyesha picha ulizompiga. Hakika atajirekebisha

Ni bora mwanamke ajue uozo wa mumewe ili achukue hatua. Kwani usilolijua ni kama uck wa giza nene. Kama anabusara atalifuatilia na kujua ukweli ambao atautumia kufanya maamuzi ya busara!

Hata kama walimuoana hatakuwa na jeuri ya kumkoromea. Pili hataweza bado kufikiri kuwa ni yeye amepiga hizo picha kwani wadaku wako kazini kila mahali.

una uhakika gani hawakumuona?
labda na wao walijikausha tu but walimuona na wakahisi yeye hajawaona????

Kumsemelea live hatari bebii. Hapo atumie tu njia ya barua. Ili watakapo kuwa kwenye kasheshe yeye awe kama mshauri tu. Lakini the wife deserves to know! Na urafiki wao utaendelea. Kumwambia live si vyema sisi wanawake hukawii kugeuziwa wewe kibao kuwa unawachonganisha kumbe tatizo ni umalaya wa mumewe.

mi namsemelea live khaa

mi naona bora kupiga kimya....ili kunusuru ndoa ya watu....na kuepusha uadui....
makubwa huo sio urafiki bali ni unafiki kama kweli manheshimiana ni afadhali hata mme wake jifanye kama unajoke kumbe unafikisha ujumbe

Najua tuko tofauti. Mimi napenda kupata news kama hizo kuliko ku relax kumbe mtaani watu wananing'ong'a. Na siyo siri huwa natafuta hizo taharifa now and then usiniulize how.
Assumptions nyingine bana! Jiulize - ingekuwa wewe ungependa kupewa taarifa kama hizo?

Hivi AD una amini kuwa uki mconfront shemejiyo na kumkanya aache tabia ya uzinzi atakusikia kuliko angekuwa confronted na wife wake??? Na wanaume navyowajua eti umfate umwambie aache kutembea nje ya ndoa nakwambia atakwambia na wewe unamtaka.

Afu ukikaa kimya no matter how happily married they are ikapita miaka miwili wakaanza kuhara kwa ngoma wont you feel guilty????

Mimi kwa kweli LAZIMA ningepeleka taharifa ila BILA KUJULIKANA kama ni rafiki yangu kweli na namtakia mema.

Kuna wanaume wengi tu wanahacha uzinzi baada ya kugunduliwa na wake zao. Kwa kukaa kimya huyo jamaa ataweka makazi kabisa kwa huyo small.

Kuna wazinzi wengi tu tunawajua ila tunafunga midomo kwa kuwa hawatuhusu; lakini best friend wangu au ndugu yangu hakika siwezi kukaka kimya ntasema tu though not directly.

NK bado naendelea kutafakari..... Dah! Ila nimependa saaana hapo in Red....

kwanza jiulize huyo rafiki yako anakifua? anawezakuhandle hizo news?? kama rafiki yako is strong enough mwambie but isimpe picha mwache yeye mwenyewe afanye utafiti wake akishagundua kama uliyosema ni kweli ndio amconfront mumewe...lakini kama huyo rafiki yako hana kifua usimwambie maana kwa mtazamo wangu ujue urafiki wenu ndio utaishia hapo, na wewe utaonekana mbbaya, na mumewe atamkataza kuonana na wewe coz anajua utampa umbea.tatizo watu wakipewa info kama hizo wanakurupuka wakati kinachotakiwa afta that, ni muhusika kuanza kumfuatilia mumewe ili ajue kama hayo mahusiano bado yanaendelea...binafsi nilikutana na mkasa kama wako, best yangu alikuwa nje ya nchi kimasomo,mimi na patna wangu tukaenda hotel tukakutana na mume wa best yangu akiwa na mwanamke mwingine n she looked pregnant!tulinywea,lakini sikumwambia shost wangu coz namjua hata amfumanie mumewe live hawezi kumuacha, sasa ya nini nimpe maumivu ya moyo wakati majibu ninayo?? kuna watu wanajua udhaifu wa wanaume zao na wameyakubali bora liende, ninachokushauri pima upepo kwanza wa rafiki yako vingenevyo potezea, ila najua as a true friend kinakuuma bt thats life.

Aisee mjadala umenoga na nimepata views tofauti kama nilivyotegemea! Ilinitokea recently, husband wa shoste wangu ambaye he is also my best friend had a girlfriend; how did l came to know, one weekend we went for nyanachoma, n then he received a call, toka kwa msichana ambaye baadaye niligundua ni mpenziwe! Yule dada alitujoin, tukala na kunywa, mashauzi yaliyoendelea yalinistua kidogo!

Jioni yake, tulikuwa twende kwenye party ya harusi pamoja na mkewe! So jamaa akanitafuta before, na kunieleza live kuwa huyo ni demu wake so l should be careful nisiropoke about the afternoon kwa mkewe (shoste) wangu! Kwakweli nilichanganyikiwa kiasi kwamba sikutaka kwenda kwenye party! It took a month mimi kuongea na yule kaka (mkewe anafanya kazi nje ya mji). Nikaamua kumcofront mwanaume na kumpa live na pia kumwambia l won't be joining him popote nitakapomkuta; before sijamwambia chochote, yeye akaniambia kuwa amemuacha yule msichana na bla bla bla nyingi!

Kwa kweli nilikuwa relieved sana, ingawa uwezekano mkubwa ananidanganya. Kitendo cha kumtunzia siri (ingawa nisingemwambia rafiki yangu) lakini nilikuwa nafeel guilty sana, as if nashirikiana na mumewe kumsaidia kucheat!

Usimkatishe uhondo, mwache akamalizane na chombo kipya, kisha baada ya siku mbili utamtafuta na kumuonyesha picha ulizompiga. Hakika atajirekebisha

Ngoja nikimuona mkeo anacheat, nitamwacha kwanza akapate new experience ndio ninconfront! Ha ha hah!

I always admire your contributions!!!!!!! Hakika yake wote tungekuwa kama wewe tungefika mbali sana. Keep it up Madam Nsiande

Usimkatishe uhondo, mwache akamalizane na chombo kipya, kisha baada ya siku mbili utamtafuta na kumuonyesha picha ulizompiga. Hakika atajirekebisha
mkuu kumbe na ww ni mdada hongera zako

Nimeipenda hiyo; eeh mkionana unampa issue yote au ilikuwa show tu kwa wale cheaters?

<br / KTKN NA PRESHA ATAKAYOKUA NAYO ATAJIELEZA MWNYW KWA WIFE JAPO HATASEMA KW NI KIMADA WK.

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…