Bishanga Abishaija. . .
Tajiri la Kihaya. . .
Mkali kama fire. . .
Yani nimeona unatafuta namba yangu mpya nikajisikia vibaya kweli. Yani ukorofi nilete mimi wa kunitafuta uwe wewe kwakua mi kiburi kimenijaa mpaka mashavuni. Naomba unisamehe mpenzi, nisamehe. . nisamehe. Nilikua nimekasirika wakati nafanya vile hata sikuwa nafikiria, ila sasa najua kile kitendo hakikua sahihi kabisa. Sasa hivi najua thamani yangu kwako na yako kwangu. . . sitaki tupotezane hivyo naomba unipokee nyumbani. Sasa hivi niko hapa nje kwente taxi nasubiria uniruhusu kurudi tuanze upya mapenzi na maisha yetu.
Nakupenda sana Bishanga. . .
Japo hujanifurahisha kuleta mambo yetu huku nasahau hilo ili tuanze upya. Naomba unipokee tafadhali.