Mtu mjinga tu ndio anaweza kufananisha kesi ya Mbowe na Sabaya. Sabaya hata asingepelekwa mahakamani na kushitakiwa kama ilivyo Makonda, bado ukatili wa Sabaya chini ya Magufuli ulikuwa bayana sana. Hakuna mtu yoyote mwenye akili timamu anaweza kusema mahakama iko huru, eti kisa wamemfunga Sabaya, bali tunashangaa imepata wapo uthubutu wa kumfunga kiongozi wa ccm aliyefanya unyama na kupata sifa ya kukifanya ccm kishinde kwenye eneo lake la utawala.
Kesi ya Mbowe hata mtoto mdogo anajua ni ya kubumba, na hiki kinachoendelea sasa mahakamani kutoka mashahidi wa upande wa jamuhuri, kinathibitisha hadi mahakama kwa sasa inatumikia siasa chafu za ccm. Hii kesi iendelee hivi hivi ili wananchi wengi zaidi ya hawa wa sasa, wajue ni jinsi gani mahakama imekubali kutumikia siasa chafu za ccm.