Nehemia Kilave
JF-Expert Member
- Jan 9, 2022
- 1,530
- 3,422
Habari JF, kwa sasa mivutano na teuzi za wawania Urais ,ubunge na udiwani ndani ya CCM ndio habari kuu mitaani kwa wote wana CCM na wana CHADEMA, maandalizi ya uchaguzi yanaendelea na tuna miezi miwili .
Tundu lissu na CHADEMA wana kesi ambazo hazijulikani mwisho wake lini na ni nini hatma yake ,CCM na vyama vingine 18 hili hawajali wanaendelea na maandalizi ya uchaguzi October 2025 .
Ni ajabu wana CHADEMA sasa hivi na wao wana mtu wao katika wawania ubunge wa CCM wanataka apite awe mbunge au akatwe .
Binafsi naona hoja ya No reforms No election imechelewa sana tungeanza nayo miaka miwili Nyuma kipindi cha Mheshimiwa Mbowe kwa kuwekewa mkazo mkubwa ikiwemo nguvu ya umma.
Kwa sasa nini kifanyike ili kwa huu muda mchache REFORMS zifanyike na CHADEMA tushiriki uchaguzi October 2025 ?
Najibu kichwa cha mada tu; hayo mengine sina muda nayo.Habari JF, kwa sasa mivutano na teuzi za wawania Urais ,ubunge na udiwani ndani ya CCM ndio habari kuu mitaani kwa wote wana CCM na wana CHADEMA, maandalizi ya uchaguzi yanaendelea na tuna miezi miwili .
Tundu lissu na CHADEMA wana kesi ambazo hazijulikani mwisho wake lini na ni nini hatma yake ,CCM na vyama vingine 18 hili hawajali wanaendelea na maandalizi ya uchaguzi October 2025 .
Ni ajabu wana CHADEMA sasa hivi na wao wana mtu wao katika wawania ubunge wa CCM wanataka apite awe mbunge au akatwe .
Binafsi naona hoja ya No reforms No election imechelewa sana tungeanza nayo miaka miwili Nyuma kipindi cha Mheshimiwa Mbowe kwa kuwekewa mkazo mkubwa ikiwemo nguvu ya umma.
Kwa sasa nini kifanyike ili kwa huu muda mchache REFORMS zifanyike na CHADEMA tushiriki uchaguzi October 2025 ?
nani kasema uchaguzi lazima uwe na ushindani kati ya chadema na CCM?..uchaguzi bila chadema utakosa ushindani na utakuwa mufilis.
Too late, walivyoanzisha NRNE walifikiri na vyama vingine vitadandia lift kumbe siyo, hiyo agenda ili kufanikiwa ingebebwa na vyama vyote vya upinzani na ingekuwa ni UNYAMA mwingi, arrogance ya TAL ilikuwa ni myopic, kwa sababu chama kimoja hakiwezi fanikisha hilo jambo.Waangalie jinsi ya kurudi kwenye uchaguzi huo ndiyo ukweli
Ccm hilo haliwahusu..uchaguzi bila chadema utakosa ushindani na utakuwa mufilis.
Warudi halafu wakafanyiwe uhuni kama ule uchaguzi serikali za mitaa mwaka jana??Waangalie jinsi ya kurudi kwenye uchaguzi huo ndiyo ukweli
Uchaguzi utafanyika na maisha yataendelea...uchaguzi bila chadema utakosa ushindani na utakuwa mufilis.
Uchaguzi utafanyika na maisha yataendelea.
Wahenga walimsema "Heri Tisa kamata kuliko kumi nenda rudi"
Hekima kuu ingewatuma kugombea hata akipatikana Mbunge 1 huyo atatumika kuisemea CHADEMA katika jukwaa rasmi.
Miaka 5 nje ya uwanja watashangaa wenyewe.
Reforms kufanyika nje ya ushiriki wa siasa ni ndoto za mtoto mchangaWarudi halafu wakafanyiwe uhuni kama ule uchaguzi serikali za mitaa mwaka jana??
Ili iweje.
Wakirudi kuhalalisha uhuni watakuwa wamebugi sana, kumbuka vyama vingine vyooote ni takataka havina nguvu yoyote kuitisha ccm...anayeangaliwa kitaifa & kimataifa dhidi yao ni CHADEMA tuu!
Ukitaka kujua nguvu ya CHADEMA mfano mdogo tu ni hapo Arusha Mjn mtu kama Makonda asingeshinda uchaguzi wa ubunge dhidi ya CHADEMA endapo reforms zingefanyika uwanja wa ushindani ukiwa sawa!!.
Mnajidanganya nyie...uchaguzi bila chadema utakosa ushindani na utakuwa mufilis.