Kwa kinachoendelea ni dhahiri kulikuwa na mipango ya kumuondoa Mbowe CHADEMA sema Mwamba alistuka mapema

Kwa kinachoendelea ni dhahiri kulikuwa na mipango ya kumuondoa Mbowe CHADEMA sema Mwamba alistuka mapema

Mkuu ni lazima ukubali kuangalia upinzani beyond kiongozi. Staying for too long is not healthy. 'Umuseveni' kwenye upinzani hauna maana.

Miaka 30 ni umri wa mtu mzima, zaidi ya hapo ni lazima kiongozi aharibu hata yale mazuri alyoyafanya hapo awali.

Mrema aling'ang,ania uongozi weee mpaka akafa na chama cha TLP. Mbatia naye yasingekuwa mapinduzi, naye alikuwa anafuata mkondo wa Mrema.

Lipumba naye sarakasi ni hizo hizo za kuzikwa na chama na bila shaka naye kajifunza kwa Museveni. Njoo kwa mzee Cheyo it is even worse than the rest!!

Mkuu haiwezekani watu wote wawe ni wasaliti linapokuja suala la kubadili uongozi uliokaa muda mrefu. Change is like rest!! Kila jambo huenda na wakati.

Usisahau kauli yenu huko nyuma kwa chama tawala almaarufu kwamba; nanukuu, "Huwezi kutegemea mfumo ulioleta matatizo kuleta majawabu sahihi" mwisho wa kunukuu.

Kauli ile, huu ndio muda muafaka wa kuitumia.

Wanaotaka mabadiliko sasa wako sahihi kwa muda sahihi. Ni tatizo na upunguani wa akili kuamini kuwa hakuna mtu mwingine anaweza kuongoza chama vizuri isipokuwa kiongozi aliyepo madarakani.

Haiwezekani Chacha Wangwe, ZItto Kabwe, Sumaye na sasa Tundu Lissu. Wote wawe wrong when it comes to leadership change!! Hawa wote kwa nyakati tofauti wawe ni wasaliti, sio kweli!!!

Bila kumung'unya maneno shida ni uongozi, shida ipo kwenye uongozi na ni kubwa kuliko inavyoonekana!!

Kimsingi anayenufaika zaidi na utaratibu huu wa viongozi kung'ang'ania uongozi ndani ya upinzani ni chama tawala.

Mkuu uongozi wa Chadema kwa sasa hauna mbinu mpya wala mtazamo mpya, wamefika kwenye ukuta. Mabadiliko ya uongozi hayaepukiki.

Kwa sasa huo ni mvinyo ule ule ndani ya bilauri ile ya zamani!!!
Comment hii ingelisomwa na walamba viatu pamoja na machawa wote wa Ccm, hakika ujinga, utetezi na ubishi wa kipumbaf kutetea 'chama zee' kungelipungua sana na watu wangelibadishana mawazo kistaarabu.
 
Just Imagine Msigwa,Heche,Lema na wenzao wangeshinda kwenye Kanda wakamuweka Mbowe mtu kati halafu Lissu akachukua Fomu nini kingetokea?

Lialia ya Msigwa,Lema na Heche na yanayoendelea kwa Lissu sasa hivi yanatafakarisha na kuleta majibu mengi sana ya kwanini Agenda ya kulamba asali ilianzishwa hapo nyuma na imeendelea kupiganiwa kwa sura ya Rushwa kwenye Chama, inaonyesha huu ulikuwa Mkakati.

Binafsi nakubali kazi na Ujasiri wa Lema,Lissu na Heche na kazi waliyoifanya katika Mageuzi na kujenga Demokrasia hapa nchini ila katika hili la kusambaratisha CHADEMA wapigania mabadiliko hawatawasamehe,nina uhakika watapotea wao na CHADEMA itaendelea kuwepo.

Binafsi nilitamani wote wabaki na vyeo vyao kama vilivyo na zaidi Heche akabidhiwe Kanda ya Serengeti waendeleze Libeneke, na Mbowe nae aambiwe abadili Siasa zake aingie kwenye Hard Politics ili kuipa pressure system ilete Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi ya ukweli, ila sikubaliani na kuchafuana na kushughulikiana.

Namuona Lissu akishindwa kumuondoa Jabali Mbowe,na Lissu nje ya CHADEMA namuona akipoteza Credibility yote aliyoijenga kwa Gharama kubwa na akienda ACT ataisha kisiasa kabisa bora akafanye mambo yake mengine.

Take it from me Watanzania wengi wanailinda CHADEMA isife ndiyo maana kuondoka kwa Magiant wengi kama Zitto,Slaa,Kaburu,Msigwa,Covid 19,Mamia ya waunga juhudi nk bado kumeiacha CHADEMA.Je Lissu atapita njia hiyohiyo?

Tutarudi hapa baadae kuonyeshana haya matokeo kama Magiant yatafanikiwa kuondoana CHADEMA
Aliyekutuma hajakuandikia vizuri au ulisimuliwa ukasahau ulivyosimuliwa
 
Sijasema hivyo, don't put words in my mouth. Ninachosema ni NOBODY KNOWS, ni gamble which can go either way. Lissu ana charisma ya aina yake ambayo akikaa kwenye uongozi italeta upya amsha amsha lakini bado kwenye upande wa strategies na kukabiliana fitna za ki-Mafia za chinichini za chama tawala kuzikabili watu aina ya Mbowe lazima wawepo.
Sawa, kwani mbowe asipokuwa mwenyekiti anatoka chadema? Kukipambania chama sio lazima awe mwenyekiti tu, anaweza pewa kazi mahususi ndani ya chama na mambo yakaenda
 
Sawa, kwani mbowe asipokuwa mwenyekiti anatoka chadema? Kukipambania chama sio lazima awe mwenyekiti tu, anaweza pewa kazi mahususi ndani ya chama na mambo yakaenda
Si lazima awe mwenyekiti la hasha, kama wenyewe wamekubaliana aachie bodi it's well and good ila wamuweke karibu kwenye upande wa mikakati, kuongoza chama si siasa za majukwaani tu bali mikakati na fitna za chinichini huwa ndiyo nyingi zaidi ambazo watu tulio nje ya mifumo ya kisiasa huwa hatuzioni. Umeona mbinu iliyoiua CUF? Lipumba alikubali kununulika akakiua chama kilaini kabisa and that's how CCM operates.
 
Wanaotetea Mbowe abaki kama mwenyekiti mnakidogosha CHADEMA kuwa hakifai kuchukua dola kwa vile hakina watu makini isipokuwa Mbowe tu.

Kwa hili wachaga mnaonyesha ujinga wa kiwango cha lami.

Ukabila na uzezeta.
 
Natamani kuona Lissu, Heche na Lemma wakijiunga na CCM ili Mbowe tuone kama atalamba tena asali kwa chama Cha level ya CUF au TLP
Hivi unamuona Lissu ni mpumbavu wa kuweza kuunga juhudi za genge ambalo lilitaka kumtoa uhai? Kwa Lemma siwezi kumsemea lakini Lissu na Heche kwenda CCM ni ngumu sana, na kwa taarifa yako Lissu ndiye mwenyekiti ajaye na Heche ni Katibu Mkuu ajaye, na Mbowe ataendelea kuwaepo Chadema.
 
Mbowe akiendelea kubaki chadema kama mwenyekiti, utakuwa mwanzo wa chadema kuporomoka kwa Kasi, mbowe amefika mwisho, vinginevyo atafutiwe kitengo ndani ya chama kama Baraza la wadhamini nk.Kugombea uongozi ndani ya chama inakuwaje kusambaratisha chama?

Wapumbavu hawatakuelewa kamwe.
Binadamu wana tabia ya kukinahi jambo au kitu au mtu.

Hata mapenzi yana muda yakifikia yanafubaa. Watu wanabaki wakivumiliana tu.

Trump ni mfano alipokua madarakani wamimchoka akapumzika wakamchoka Biden wakamkumbula Trump.

Watu wana mpenda Mbowe ila wanataka mabadiliko waone kasi mpya .

Mbowe akipuuza ataua Chama.

Hivi watu hawajiulizi kuwa kwa sasa Lisu ni tishio kubwa sana kwa CCM na hawatamani agombee hata Urais c
achilia mbali uenyekiti wa chama .

Lisu ana nguvu kubwa Kiroho na kiutawala kuliko Mbowe.
Mbowe ana nguvu ya pesa sio nguvu ya kisiasa ndio maana anapigwa màkofi mpaka nyumbani kwake na UVCCM na hakuna mtu anaguswa hata kumpambania kwa kurusha hata jiwe
Tofauti na Lisu akiwa jimboni kwake ni kama mfalme japo hana pesa . Huu ni ushahidi wa kuwa na nguvu za kiroho na kiutawala na uongozi.
 
Back
Top Bottom