Heaven Seeker
JF-Expert Member
- May 12, 2017
- 479
- 1,071
Heshima kwenu Wakuu.
Mtoto wa binamu yangu hakufanikiwa kupata ufaulu mzuri wa kuendelea na masomo ya kidato cha tano mwaka huu.
Lakini kutokana na kipaji cha uchoraji alichonacho tukaona ni vema ajiendeleze kwa kuongezea taaluma juu ya kipaji chake.
Kulitolewa wazo la kumpeleja VETA na mipango yote ikafanyika. Ikashauriwa asome course inaitwa " Paintig and Sign Writing". Ila baada ya majibu kutoka akawa amechaguliwa hapo VETA Chang'ombe course inaitwa "Pre Press and Digital Printing". Sikujua kama unaweza kwenda VETA kuomba kusoma kitu flani na usipewe ila ukachaguliwa kitu tofauti na ulichoomba. Any way hiki ni kibwagizo tu..
Naomba niwe muwazi kuwa sina ufahamu wa kutosha wa hizo courses zote mbili. Vilevile sina ufahamu wa kutosha wa aina na kiwango cha Elimu ya VETA inavyotolewa. Muda wa mafunzo VETA inaonesha ni miaka miwili na ada ni kama 300K hivi na senti kidogo.
Concern yangu kubwa imekuwa ni thamani ya muda huo atakaokuwa hapo VETA na aina ya ujuzi ama Taaluma atakayoipata. Maana ningefurahi kama angejifunza kitu kitakachomuwezesha kujiajiri na kuendeleza kipaji chake.
Baada ya Tafakari ya muda, nimefikiri labda tumpeleke Training center ambayo ni private hapo Posta akajifunze Graphics designing kwa miezi miwili badala ya kutumia muda wa miaka 2 kujifunza vitu ambavyo hatuvielewi kwa undani. Akijifunza Graphics anaweza kujiajiri huku akiangalia namna ya kuendeleza kipaji chake cha uchoraji.
Naombeni ushauri wenu katika hili. Je, kwa kipaji cha uchoraji alichonacho mtu anaweza kujiendeleza kwa njia gani?
Naambatanisha na picha zake ambazo huwa anachora. Samahani kwakuwa hazionekani vizuri sana.
Natanguliza shukrani zangu kwa dhati Wakuu. Mawazo yenu huwa nayaheshimu sana. JF imekuwa dira katika mambo yangu mengi sana..