Kwa kipato hiki nianzie wapi ili kumiliki nyumba

Kwa kipato hiki nianzie wapi ili kumiliki nyumba

gambagumu

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
2,091
Reaction score
2,816
Namshukuru Mungu kwa kunipatia ajira Mwaka huu, kipato changu kwa mwezi ambacho nina uhakika nacho ni 2M,Je kwa kipato hiki naweza kweli kumiliki nyumba?
 
umenikumbusha,mke wangu wa zamani aliwahi kuniambia na lini kwa walionakazi kama yako watajenga,nikamweleza lazima nitajenga,tulitengana mwaka jana mwezi wa tatu,na mwezi wa sita nikanunua kiwanja na nikajenga.karibu madale kwa daimond platnumz
 
Unataka kuanza kujenga lini mkuu?
Tulia kwanza jipange coz huwezi kuanza kazi leo na kujenga papo hapo.

Mara nyingi huwezi kutegemea mshahara katika ujenzi hivyo ni vema kufikiria kuwa na pato la ziada

Mshahara utakwezesha kukopesheka ktk saccos au taasisi za fedha kwa maendeleo binafsi ikiwemo kujenga.
Bajeti vyema matumizi yako na angalia namna utakaoyweza kuwa na kipato cha ziada pia kitakochokuwezesha kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka zaidi.

Kila la kheri, kama nakuona vile ulivyo na ma-plan ya kufa mtu!!
 
Nyumba ndo.maisha mkuu, asamte kwa ushauri.
 
2 mi inaweza kuwa kubwa au ndogo kulingana na nyumba unayoitaka... Kama unategemea hapo kwa kila kitu.... Weka serving ya 1.5 kila mwez..... Baada ya 6 months.... Utakuwa pazur na kama unataka haraka.... Nenda bank kopa
 
kuna baadhi ya watu watakuja kukunanga huo mshahara ni mkubwa sana unajenga ghorofa kabisa..

hawa watu sijui hawanaga majukumu au hawajawahi kuishi miji mikubwa na expensive as Dar na kufanya kazi kwenye corporates.. a lot of bills zinaitaka hiyo 2m yako.. bado wategemezi, extended etc etc..

kujenga utajenga kaka lakini cha moto lazima ukione kama utategemea kipato hicho hicho
 
namshukuru mungu kwa kunipatia ajira mwaka huu, kipato changu kwa mwezi ambacho nina uhakika nacho ni 2m,je kwa kipato hiki naweza kweli kumiliki nyumba?
si lazima kila mtu ajenge..
Fanya mambo mengine ya maana kwanza.
Halafu ujenge baadae kama ikibidi
from here humu ndani hakuna atakaye kuwepo miaka 30 ijayo
so kipaumbele sio nyumba.
Kula bia.
 
si lazima kila mtu ajenge..
Fanya mambo mengine ya maana kwanza.
Halafu ujenge baadae kama ikibidi
from here humu ndani hakuna atakaye kuwepo miaka 30 ijayo
so kipaumbele sio nyumba.
Kula bia.
[/QUOTE
Mh..we jamaa wewe.
 
Kaka kwa hicho kipato ningekuwa nshamaliza kajumba kangu pale Bunju.
Unless kama una michepuko mingi
 
Namshukuru Mungu kwa kunipatia ajira Mwaka huu, kipato changu kwa mwezi ambacho nina uhakika nacho ni 2M,Je kwa kipato hiki naweza kweli kumiliki nyumba?

Siku zote huwa napenda kusema kwamba,kumiliki nyumba,wazo la mwanzo na mtaji wako ni Dhamira thabiti

Hivi jiulize,kwanini mamalishe anajenga nyumba na anapangisha au kukaa mwenyewe wakati wewe mkaba tai huna hata kiwanja.
Tena ni yule mamalishe ambae wewe kwa level yako huwezi kula sehem yenye ma inzi kama ile,ila yeye ametumia fursa ya wenye kipato kidogo kufanya biashara na kupata kipato kidogo sana kwa siku.
Unajua ni nini alichofanya?ni nidhamu ya pesa na Dhamira.
Mie nimejenga Chanika,ndio niliona jinsi mamalishe wamevyojipanga,na siku za Weekenda ndio utaona kila mmoja anaenda kuangalia sehem yake.ukiuliza utasikia mamalishe tena wale wa uswahili vichochoroni.Ukimuuliza anakuambia kiwanja nimenunua mwaka wa tatu sasa ndio nataka kujenga.
Ukiangali in 5 yrs anahamia kwake na nyumba anakuwa ameijanga.

Tatizo kwa sie vijana ni uvumilivu na dhamira ya kweli.Hivi nani umuambie kwamba nina mpango wa miaka 5- 6 naweka pesa ili nijenge atakuelewa?.Na usishangae hata kiwanja akakiuza,maana wengine tumewaona,walinunua viwanja mbio kuja kuona hali ya ujenzi wakakata tamaa kwamba hawawezi kujenga,na baada ya miaka sita wale wenzao wenye kipato cha chini ya wao wamejenga,mwisho wa siku unabakia kumuuliza hivi wewe umewezaje kujenga?

Napenda sana kutumia mfano wa mamalishe maana nina experience nao,yaani mama lishe bora afe lakini hadi akuuzie kiwanja alichonunua aisee ni issue.Mie huwa nikipita mitaani nikiwaona huwa nawaheshim saana wale madada,yaani kwa nidham ya pesa kwao ni kubwa kupita maelezo,kujituma ndio usiseme.

Kwa pesa ya 2m kama pato lako kwa mwezi,nakushauri cha kwanza,Mtafute mtu humu anaitwa Mc Anton(0713565999),anaviwanja Chanika ambapo ni mji unaokuwa kwa kasi ya ajabu sana.Mwambie akutafutie viwanja wivili,yaani kila kimoja 1.5m to make 3m(nimesema viwanja viwili ili uweze kujenga nyumba yenye nafasi kubwa na value ya viwanja itakuwa imeishakuwa kubwa which will reflect to the value of your house).Unalipa kwa awamu.Kwa makadirio ya kawaida na ukijibana kimatumizi si chini ya 1m unaweza kulipa kwa mwezi au laki nane.Sasa ndani ya miezi mitano huna deni.Then baada ya hapo unakitafutia hati Wizarani,which is simple tu.so,ndani ya miezi Saba unakuwa na kiwanja chenye hati.

Baada ya mwaka au wastan wa miezi minane baada ya kumaliza hayo yote,fungua fixed account ya muda wa miaka miwili.Then mwaka wa tatu Anza ujenzi.Ili ile pesa iwe supported na kiasi cha pato hilo.Huku ukiendelea ado ado.

Kwa mionekano wangu ni kwamba ndani ya 4-5 yrs una nyumba yako nzuri tu ya kuanzia maishaa.

Ila kama huna nidham ya pesa na uvumilivu,basi kwa pato hilo hujengi.
 
Kwa mshahara huo unaweza ukajenga na ukahamia ndani ya miaka 3-4 bila pressure yeyote.Mwaka wa kwanza unanunua kiwanja,mwaka wa pili unajenga msingi na kupandisha hadi levo fulani,mwaka wa tatu unamaliza hadi lenta na kuezeka mwaka wa 4 unahamia kabisa huku ukifanya finishing ukiwa ushahamia
 
Duh mkuu hicho kipato mbona kikubwa sana asee kama tu ukiwa unadhamira ya kujenga,maana kuna watu kipato chao ni laki 4 tu lakini wanawaza hichohicho unachokiwaza ww,
kwa hicho kipato kinatosha sana kujenga la! ukiona huwezi kuvumilia ingia benki chukua mkopo hata wa milioni 30 hv afu teremsha kitu fasta ili hata kwa mwezi ukiwa unakutana na salio la laki 5 kama salary inakuwa sio mbaya.
 
Mh...Hallo kipato chako ni cha kawaida sana. Sio kikubwa wala kidogo. Mpangilio wa kutimiza ndoto zako upo na utaendelea kuwepo.. Kwa 2m unaweza kujenga au usiweze kutegemea unataka nyumba ya aina gani. Chumba na sebule ni miezi kadhaa tu unajenga.

Lkn kwa nyumba std ya vyumba vitatu sebule dining jiko na toilets ita hitaji kuanzia 50 m na kuendelea.

USHAURI: USIKOPE kabisa.

Tafuta biashara ambayo unaweza unaweza kuifanya huku unaendelea na kazi. Na biashara hiyo iwe ya Network Marketing.

Google materials za network marketing utaona how it works.

Cha muhimu uchague kampuni nzuri yenye network iliyosimama. Hapo ndo unaweza kufanikisha ndoto zako kiulaini.

Ni PM no zako kwa maelekezo zaidi.
 
Mkuu si vyema kumuingiza huyu muungwana anaye anza maisha kwenye upatu design ya DECI.
Hizi ni pyramid biz
wachache ndio hufaidi na wengi huwa watumwa wa kuishi ki ndotondoto kwamba mtatoka.
 
Mkuu inategemea matumizi yako yakoje,unaishi wapi na unataka kujenga nyumba ya namna gani na pia unataka kuwapa contract wachina wakujengee au akina mbonde.
Kila la kheri mkuu.
 
Namshukuru Mungu kwa kunipatia ajira Mwaka huu, kipato changu kwa mwezi ambacho nina uhakika nacho ni 2M,Je kwa kipato hiki naweza kweli kumiliki nyumba?
Kumiliki mali iwe nyumba, gari etc hakutegemei nini utapata, bali nini unatunza na kuwekeza.

Kuna watu wanapata mara tatu ya kipato chako, na hawana wategemezi bado wanaishi ktk nyumba za kupanga. Na wapo wanaopata nusu ya kipato chako na wana wategemezi kibao lakini wanamiliki nyumba nzuri za kisasa.

So, ni akili yako tu
 
Namshukuru Mungu kwa kunipatia ajira Mwaka huu, kipato changu kwa mwezi ambacho nina uhakika nacho ni 2M,Je kwa kipato hiki naweza kweli kumiliki nyumba?

kuna watu wanastaafu kazi serikalini hata mshahara huo nusu yake hawana tgs E tgts E wamejenga na wanasomesha

graduate tu analipwa 625000-630000 na wanamambo makubwa.
point ya msingi kuwa na kiwanja ujenzi ni kidogokidogo.
kingine anza na unachokiweza mfano kama umepanga vyumba viwili why not build your own two rooms?
tatu kuwa na mipango ya kipato cha ziada kwa maendeleo zaidi.
 
Back
Top Bottom