Namshukuru Mungu kwa kunipatia ajira Mwaka huu, kipato changu kwa mwezi ambacho nina uhakika nacho ni 2M,Je kwa kipato hiki naweza kweli kumiliki nyumba?
Siku zote huwa napenda kusema kwamba,kumiliki nyumba,wazo la mwanzo na mtaji wako ni Dhamira thabiti
Hivi jiulize,kwanini mamalishe anajenga nyumba na anapangisha au kukaa mwenyewe wakati wewe mkaba tai huna hata kiwanja.
Tena ni yule mamalishe ambae wewe kwa level yako huwezi kula sehem yenye ma inzi kama ile,ila yeye ametumia fursa ya wenye kipato kidogo kufanya biashara na kupata kipato kidogo sana kwa siku.
Unajua ni nini alichofanya?ni nidhamu ya pesa na Dhamira.
Mie nimejenga Chanika,ndio niliona jinsi mamalishe wamevyojipanga,na siku za Weekenda ndio utaona kila mmoja anaenda kuangalia sehem yake.ukiuliza utasikia mamalishe tena wale wa uswahili vichochoroni.Ukimuuliza anakuambia kiwanja nimenunua mwaka wa tatu sasa ndio nataka kujenga.
Ukiangali in 5 yrs anahamia kwake na nyumba anakuwa ameijanga.
Tatizo kwa sie vijana ni uvumilivu na dhamira ya kweli.Hivi nani umuambie kwamba nina mpango wa miaka 5- 6 naweka pesa ili nijenge atakuelewa?.Na usishangae hata kiwanja akakiuza,maana wengine tumewaona,walinunua viwanja mbio kuja kuona hali ya ujenzi wakakata tamaa kwamba hawawezi kujenga,na baada ya miaka sita wale wenzao wenye kipato cha chini ya wao wamejenga,mwisho wa siku unabakia kumuuliza hivi wewe umewezaje kujenga?
Napenda sana kutumia mfano wa mamalishe maana nina experience nao,yaani mama lishe bora afe lakini hadi akuuzie kiwanja alichonunua aisee ni issue.Mie huwa nikipita mitaani nikiwaona huwa nawaheshim saana wale madada,yaani kwa nidham ya pesa kwao ni kubwa kupita maelezo,kujituma ndio usiseme.
Kwa pesa ya 2m kama pato lako kwa mwezi,nakushauri cha kwanza,Mtafute mtu humu anaitwa Mc Anton(0713565999),anaviwanja Chanika ambapo ni mji unaokuwa kwa kasi ya ajabu sana.Mwambie akutafutie viwanja wivili,yaani kila kimoja 1.5m to make 3m(nimesema viwanja viwili ili uweze kujenga nyumba yenye nafasi kubwa na value ya viwanja itakuwa imeishakuwa kubwa which will reflect to the value of your house).Unalipa kwa awamu.Kwa makadirio ya kawaida na ukijibana kimatumizi si chini ya 1m unaweza kulipa kwa mwezi au laki nane.Sasa ndani ya miezi mitano huna deni.Then baada ya hapo unakitafutia hati Wizarani,which is simple tu.so,ndani ya miezi Saba unakuwa na kiwanja chenye hati.
Baada ya mwaka au wastan wa miezi minane baada ya kumaliza hayo yote,fungua fixed account ya muda wa miaka miwili.Then mwaka wa tatu Anza ujenzi.Ili ile pesa iwe supported na kiasi cha pato hilo.Huku ukiendelea ado ado.
Kwa mionekano wangu ni kwamba ndani ya 4-5 yrs una nyumba yako nzuri tu ya kuanzia maishaa.
Ila kama huna nidham ya pesa na uvumilivu,basi kwa pato hilo hujengi.