Kwa Korea Kusini hakuna muigizaji Bora wa kiume kama Lee Byung-hun Jamaa anajua Sana. Squad Game ni muendelezo wa uwezo wake

Kwa Korea Kusini hakuna muigizaji Bora wa kiume kama Lee Byung-hun Jamaa anajua Sana. Squad Game ni muendelezo wa uwezo wake

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Mpo salama!

Huyu jamaa kwa mara ya Kwanza niliangalia picha yake ya Kwanza Miaka ya 2009/2010 huko katika Series Moja iitwayi IRIS. Hapo ndio mwanzo wa kuzipenda na kuanza kufuatilia baadhi ya Filamu za Kikorea. Nikiri wazi kuwa kabla ya kuangalia Filamu ya IRIS sikuwa mpenzi wa Filamu za Kikorea.

Huyu jamaa kwa ambao wameona Filamu alizocheza wataungana na Mimi kukubali kuwa jamaa ni bingwa na mahiri katika tasnia ya uigizaji na Mimi nampa namba moja katika taifa la Korea ya Kusini.

Baadhi ya picha maarufu alizocheza ni pamoja na;
1. IRIS. (Kijasusi)
2. TERMINATOR (action movie)
3. Mr. Sunshine (Kijasusi)
4. Squad Game (Kijasusi)
5 concrete Utopia (Kijasusi)
6. Reds. (Action movie)
7. Terminator 2. (action movie)
Na miongoni mwa nyingi.

Kama wewe sio mpenzi wa Filamu lakini unatamani kuzipenda Basi Anza na hizo hapo. Kama utaweza Anza na Mr. Sunshine.

Kwa mwenye picha yake anaweza kuiweka.

Mungu awabariki
 
Umehitimisha vema sana "Mungu awabariki"bila shaka utakuwa muungwana anyway wakorea Kila nikijaribu kuwafatilia nashindwa
 
Hajamfikia jung Lee mpwa wake na Bruce Lee alizaliwa korea ana urefu wa fut 5.5 ana mke na watoto wawili, wakwanza anaitwa Chun Lee wapili ni Yuong Lee

Enzi za mabanda ya video
 
Mara ya kwanza namwangalia kwenye "A bittersweet life" anajua sana.
 
Sio Squid Game? Squid game huwa ina pop up kwenye Netflix yangu wala sijawahi kufikiria hata kuisoma inahusu nini.

Hutojutia kuangalia.
Anza season one kisha malizia na Mbili.

Wakati naianza kuangalia season one niliidharau lakini wale jamaa walinibadilikia. Wamecheza vizuri Sana.

Nisikumalizie uhondo
 
Bahati mbaya una hulka kama za mbowe na uchairman wake wa milele kuwa usemacho na wengine waamini watake wasitake.

Au ndo ile kipofu kaona ghafla voom punda yule mbele yake kisha akarudi kwenye hali yake kila akiambiwa kuhusu wanyama iwe ng'ombe,twiga etc yeye atasema punda ndo kibako yao
 
Watu wanambwembwe ila Korea wake mbali sana kwenye movie
Mbwembwe gani tena? Nilijua series za kikorea ndio zile zile za kike so wala sikuwa na time nayo. Itabidi niiangalie watu wanaisifia sana humu JF.
 
Back
Top Bottom