Kwa kugawa wanyama wetu tumeuza upekee wetu. Tumebaki na nini?

Waachiwe kwenda jangwani?

Wataweza kumuona cheetah anawinda swala kama Serengeti?

Wataona Wilderbeast migration
Kinachoshindikana nini?.kama watu wa jangwan wanaweza kufanya mazingira wakalima mazao na wakatuletea kutuuzia unafikiri kinashindikana nini kutengeneza hifadhi.
 
Unafanya jambo la kizalendo sana. I hope tutaamka. Na wengine wanaweza kusema usilalamile tu toa ushauri nini kifanyike.

Ushauri wangu ni huu, hili jambo lingefanywa kwa uwazi kabisa. Moja ya faida za kufanya hivyo ni pride. Watanzania wakijua wanasaidia kujenga mataifa mengine kwa fadhila kama hizi, watatembea vifua mbele kwa pride badala ya kuishi kinyonge kama sasa.

Pili tungeingia ubia na hizo kampuni zinazoendesha hizo zoo na parks. Hii itatuhakikishia mapato ya vizazi vijavyo. Hizi pesa za kulipana chini kwa chini kwanza zina harufu ya ufisadi na zinaweza kuishia kufanyia matumizi yasiyo na tija. Pia tukiwa kwenye management za uendeshaji, tutajifunza mengi ambayo tunaweza kuja kuyatumia hata huku kwetu.

Yote haya yanahitaji viongozi na watendaji waadilifu sana.
 
Huwa nashangaa sana ninapoona viongozi wanaenda huko nje na kuomba wafundishwe mbinu mbalimbali, najiulizaga hivi dunia hii tunaijua kweli?

Kama tunataka tujifunze vitu, peleka vijana wakasomee hayo mambo, wakimaliza wape mitaji warudi wafanye hizo biashara. Hivyo ndiyo Wachina, Wajapan na Wakorea wamefanya. Sisi tunapeleka uswahili wa kumuomba jirani chumvi nyanja za kimataifa.
 
Sijasema hivyo. Kwa hiyo unabisha kuwa ukiacha wale tausi tuliompa Kenyatta hatujawahi kugawa wanyama wetu kwa mataifa mengine?
Mkuu kwamba Tanzania ndiyo asili ya wanyama waliojaa dunia nzima?
 
Mambo mengine yanaudhi mpaka mtu unatamani kulia. Mwalimu alikuwa ameacha madini ili baadae yaje kuchimbwa wakati tunaweza kupata faida iliyo stahiki.

Matokeo yake sasa, madini yamechimbwa na tumeachiwa mashimo na hakuna cha kujivunia

Sent from my SM-J810F using JamiiForums mobile app
 
Mambo mengine yanaudhi mpaka mtu unatamani kulia. Mwalimu alikuwa ameacha madini ili baadae yaje kuchimbwa wakati tunaweza kupata faida iliyo stahiki.

Matokeo yake sasa, madini yamechimbwa na tumeachiwa mashimo na hakuna cha kujivunia

Sent from my SM-J810F using JamiiForums mobile app
 
Labda angeyaruhusu yachimbwe wakati huo ilikuwa rahisi kudhibiti, la kwanza tulikuwa wachache na pili Uadilifu na uaminifu ilikuwa kawaida sana

Hakujua tu kuwa mambo yatabadikika na watakuja majambazi wasiokuwa na uchungu wa nchi ambapo wanaweza hata kuuza hewa tunayovuta ya bure ili tufe wote

Wakati mwingine naona wakuja ni wazalendo kuliko hao wanaojiita wazawa na kutambia makabila bali majizi yasiokuwa na Soni wala aibu
 
Mkuu kwamba Tanzania ndiyo asili ya wanyama waliojaa dunia nzima?
Mbona umekazia sana hilo swali? Na mimi nitakuuliza tena Tanzania hatujawahi kugawa wanyama?
 
Kwa mtazamo wangu, dunia inahitaji mashirikiano kati ya nchi na nchi ila ni muhimu sana kumaintain competitive advantage uliyo nayo katika uchumi na biashara. Uzalendo unaanzia hapo.[emoji1545][emoji817]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…