The Shah of Tanganyika
JF-Expert Member
- Jul 2, 2023
- 602
- 1,572
Mwenyezi Mungu alitupa nchi takatifu. Akatupatia waasisi. Akawapa elimu na utambuzi na akaamuru tuwe taifa huru. Watu mtakaoishi humo mpate hifadhi ya makazi na ardhi nzuri ya kuzalisha kila aina ya bidhaa.
Ardhini akawawekea wanyama ili mkiwatumia na kuwahifadhi mpate fedha za kuishi. Hamkuwatengeneza ninyi.
Chini ya ardhi akawawekea kila aina ya madini, ili mtakapokuwa na elimu muyatumie kuzalisha bidhaa na kuziuza duniani huko.
Katika anga akaiamuru mvua isipungue juu yenu. Akaizingira nchi na bahari, maziwa makubwa na mito ya kutosha.
Akawapa na amani, musije mkamlaumu kuwa kawawekea ncha ya silaha ili msifike mbali.
PAMOJA NA FADHILA HIZI ZOTE
Sisi tukiongozwa na viongozi wetu tumemkebehi Mungu na kumdhihaki kuwa yote aliyowatendea alikosea. Tumempa jibu moja kuwa hakupaswa kutuandalia sisi wana wa nchi hii vyote hivyo bali alipaswa kuviumbia watu wengine huko.
Tumemtukana, na kumdhihaki kuwa sisi hatuhitaji vyote hivyo bali tutaenda kwa mwarabu atupe pesa ya bure. Kwanini atupe mateso ya kuanza eti kusoma na kubuni teknolojia wakati mwarabu anaweza kutumwagia pesa ya bure?
Jibu letu kwa Mungu ni kuwa atuache tugawe tupate hiyo pesa. Asitulazimishe eti tuendeleze ardhi hii itufae. HATUTAKI.
Hata kama tutatawaliwa na tutawaliwe tu. Tumempasha kuwa yeye ni nani mpaka atulqzimishe sisi kufanya kazi? Kwani tukimpa mwarabu si atafanya kazi yote ya kuendeleza na sisi tutachota pesa za bure?
Jibu letu kwa Mungu ni moja tu. Sisi tumekuzidi akili. Utuache tufanye tujuavyo. Usituingilie wala kutupangia. Tumechoka kuyasimamia haya mambo ya ardhi, madini, gesi, mito, wanyamapori, bahari, maziwa, nk. Tumempata shoga wa kutusimamia. Sisi tunaenda kulala tusubirie makapu ya pesa.
HUKUMU YA MUNGU JUU YA TANGANYIKA
Hukumu na ghadhabu ya Mungu ipo juu yetu.
Ole wetu kwa yatakayotupata.
Awezaye kuomba na aombe sasa. Awezaye kukesha na akeshe sasa.