Mkataba kuhusu wanadiplomasia ni
Vienna Convention on Diplomatic Relations of 1961. Hakuna kuvunja mkataba huo kwa kuongea na watu wowote.
Tanzania imejaribu mwaka 2016 kuunda mashariti
https://www.nation.co.ke/news/africa/Tanzania-issues-tough-rules-for-diplomats-local-movement/1066-3061614-f37ej3/index.html ("The circular further directed all members of the diplomatic corps to seek permission from the Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Co-operation, before traveling upcountry and meeting any local government authorities or grassroots organisations. ").
Ila jaribio hili ni kinyume cha mkataba wa Vienna nisipokosei. Kifungu 26 kinasema:
"Article 26 Subject to its laws and regulations concerning zones entry into which is prohibited or regulated for reasons of national security, the receiving State shall ensure to all members of the mission freedom of movement and travel in its territory. "
Nchi inaweza kufunga maeneo maalumu shauri ya usalama. Inaweza kukataza maafisa wa nchi kuongea na balozi bila kibali cha awali.
Laini haiwezi kumkataza balozi kuongea na hao ambao anataka. Ni kweli nchi kadhaa wanajaribu kubana mabalozi. Hapa wanajibana wenyewe maana kwa kawaida nchi nyingine inajibu kwa mashariti yaleyale.
Kuna nchi zinazotaka kupata taarifa ya awali kutoka mabalozi shauri ya usalama kuhusu safari nje ya mji mkuu. Hii inakubaliwa mara nyini lakini hata kama balozi anasema anakwenda huko au pale kwa kusudi fulani hakuna sheria ya kimataifa inayomzuia kufanya pia mambo mengine.
Na hawezi kushtakiwa au kukamatwa maana mapatano ya Vienna inampa balozi "immunity" (
Article 29 The person of a diplomatic agent shall be inviolable. He shall not be liable to any form of arrest or detention. The receiving State shall treat him with due respect and shall take all appropriate steps to prevent any attack on his person, freedom or dignity )
Kila nchi ni huru kumtangaza balozi kuwa "persona non grata" (mtu asiyetakiwa), lakini hapa imeshafukuza balozi wake pia kutoka nchi nyingine, maana kwa kawaida kama nchi A inamfukuza balozi wa B, basi B humfukuza pia balozi wa A.
Chanzo:
legal.un.org/ilc/texts/instruments/english/conventions/9_1_1961.pdf