Machungu yapo mengi watu walikuwa kimya lakini sasa 2020 watu wana jambo lao kote Zanzibar na Tanganyika kutokana na ubabe wa CCM Mpya
ZANZIBAR HATARINI KUKOSA UMEME KUTOKANA NA DENI LA BILIONI 121
Posted by
Chumba-cha-Habari | Mar 6, 2017
Rais Dr. John Magufuli jana aliiagiza (Tanesco) kuwakatia umeme wateja wote wenye madeni makubwa ikiwemo serikali ya Zanzibar kutokana marimbikizo ya madeni yanayodaiwa.
Alisema kuwa Zanzibar kupitia shirika la umeme za Zanzibar (Zeco), imekua ikiongoza kwa deni la Tanesco kiasi cha shilingi bilioni 121 za Tanzania jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya TANESCO.
Akizungumzaalipokwenda kuweka jiwe la msingi kwenye kituo kipya cha Tanesco mkoani Mtwara, rais Magufuli alizitaka tasisi zote za umma kulipa madeni yao la sivyo zitakatiwa umeme haraka bila kuogopwa.
“Msiogope mnapaswa kukata huduma hii kwa taasisi yoyote ambayo hailipi bili zake.
Nataka kumwambia waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwamba umeme unapaswa kukatwa hata Ikulu.
Nikilala gizani, halafu maafisa wa Ikulu ambao hawajalipa watawajibika na sio wewe. Una hakikisho langu kwa hili.
Pesa za kulipa bili kawaida hutolewa kwa wizara zetu, lakini badala yake hupelkwa kwingine
.
”Ninaambiwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haijalipa Sh121 billion. Ninyi (Tanesco) si wanasiasa…mnapaswa kuzingatia majukumu yenu ya kitaaluma…kata huduma ya umeme.Nimesema hata kama ni Ikulu , polisi, jeshi ama shule , hakuna mwenye deni anaepaswa kuachwa .
Ni kwa njia hii tu tunaweza kuhakikisha kwamba pesa zilizotengewa wizara kwa ajili ya umeme zinatumiwa kama ilivyopangwa ili Tanesco iweze kuendesha kazi zake na kushughulikia matatizo ya uhaba wa umeme.
”Tanesco haiwezi kuboresha huduma kwa sababu ya madeni ya serikali yasiyolipwa”.
Nae Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa pili wa rais , Bwana Mohammed Aboud, alisema kuwa Maagizo ya rais Magufuli yako wazi, Madeni lazima yalipwe na yatalipwa na mipango inafanyika kwa ajili ya kuliwezesha shirika la Zeco kulipa madeni ya Tanesco.
” Tumeanza mchakato wa kuhakikishwa suala hili linatatuliwa.Pia tumeiagiza Zeco kuacha kulimbikiza madeni mapya”.
SHEIN - "Magufuli Hatimaye Kafanya Maamuzi, Amesamehe Deni"
Published on 21 Jan 2019
DKT SHEIN - "Magufuli Hatimaye Kafanya Maamuzi, Amesamehe Deni" BARAZA la mawaziri limeridhia utozwaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kiwango cha asilimia 0% , kwenye umeme unaouzwa na shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO) na kufuta malimbikizo ya deni la kodi ya VAT lililofikia Shilingi Bilioni 22.9 kwa TANESCO kwenye umeme wa ZECO. Kwa upande wake Rais wa Zanzibar, Dkt Shein, pamoja na kuridhia utozaji wa VAT kwa kiwango cha asilimia 0%, Baraza la mawaziri pia limekubaliana kuwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, ataitisha vikao vya kuzungumzia masuala ya Muungano kila mara kunapokuwa na hoja ya masuala ya Muungano ili kujadili na kutoa maamuzi.