Kwa kweli Kiswahili ni kigumu

sensor sio kisimbuzi ni king'amuzi

mouse (in computer set) sio kipanya, lipo jina la kiswahili, nimelisahau.

Force sio kani, ni nguvu.

Kani ni neno la kiswahili ambalo lina maana ya neno Torque katika engineering.
 
Mwaka 2007 Niliwahi kufika Kyela kwenye kijiji kimoja kinaitwa IKOLO wakati najaribu kuweka vocha nikapewa ujumbe huu Hakuna Mtandao wa Tandabui kumbe ndio No Network Coverage Kiswahili balaa
 
sensor sio kisimbuzi ni king'amuzi

mouse (in computer set) sio kipanya, lipo jina la kiswahili, nimelisahau.

Force sio kani, ni nguvu.

Kani ni neno la kiswahili ambalo lina maana ya neno Torque katika engineering.

Hayo ya sensor kama ni kisimbuzi ama ni king'amuzi nawaachia wajuvi.

Nitachangia kwenye Force, kani, torque, nguvu na yanayohusiana na hayo.

Force ni kani. Nguvu ni power. Torque sifahamu neno sahihi kwa Kiswahili. Maelezo yanafuata.

Kazi= kani X umbali ambao kile kinachosukumwa na hiyo kani kimesogea kuelekea upande uleule wa msukumo wa kani. (Work=force X distance moved in the direction of the force ). Alama hii 'X'ni alama ya kuzidisha.

Nguvu = kasi ya kufanya kazi(Nguvu =kazi/muda wa kufanya hiyo kazi). (Power is the rate at which work is done. Power=Work/Time). Alama '/'ni alama ya kugawanya.

Sasa Torque. Torque ni matokeo ya kuzidisha kani na umbali. Uelekeo wa kani na uelekeo wa huu umbali vipo perpendicular ...hahaha(hivi perpendicular kwa Kiswahili tunasemaje?). Torque is the product of force and the perpendicular distance from a fixed point to the point where the force is being applied.

Nimejaribu kueleza kadiri ya sayansi na Fizikia niliyojifunza
shule ya msingi na sekondari kwa mfuatano huohuo (yaani respectively🙂
 
Mtoa mada sijui kigumu nini hapo, mbona maneno ya kawaida sana hayo? Isipokuwa machache ambayo uwa hayatumuki sana. Hata hicho Kiingereza mnachodai ni kirahisi si hivyo, ndio maana MAhakama Kuu wasomi wenye Ph.D huwa kinawatoa jasho.
 
vibanzi vikavu na pepsi.
Aisee!
 
Maneno mengi unayoyasema ni ya kitaalamu, na huwa hayatumiki sana kwa hiyo si ajabu kuona watumiaji hawayatumii na hawayafahamu kabisa.
Lugha haipimwi kwa idadi ya msamiati wa kitaalamu anaofahamu/asiofahamu mtu bali uwezo wake wa kutumia lugha hiyo katika mawasiliano ya kila siku na ya msingi.
Kuna kundi la msamiati huitwa msamiati msingi, hakuna neno hata moja kati ya uliyoorodhesha ambalo linaingia katika kundi hili. Uwezo wa kusema lugha/umilisi huamuliwa kwa kiwango cha matumizi ya kundi hili la maneno.
 
Aksante umeniongezea maarifa,ila kwa baadhi ya maneno nikiyaongea nadhani hakuna mtu atanielewa kama KADIWIA kwa SIM CARD.
 
Mmenye...Una kadi ya kiotomela ya benki gani...?

Nilihitaji kununua mweko mbili, mdaki mmoja na vinukuzi viwili..nikaenda mpaka kwenye kiotomotela ya Benki ya Ushirika na Maendeleo vijini; ile nataka kufanya muamala si nikastuka nywila yangu nimeisahau!!!!
 



Umetisha sana mkuu, tujivunie nakujielimisha zaidi tu ndiyo lugha yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…