Kwa madudu anayoanika CAG, kumbe Magufuli uongozi wake ulikuwa sifuri tu

Chadema wanaingiaje hapa?
 
Kwa mifumo iliyopo Tanzania hata rais awe Tundu Lissu, Makamu Lema, Waziri Mkuu Mbowe, Waziri wa mambo ya ndani Sugu, IGP Mnyika, CDF Yeriko Nyerere, Waziri wa Katiba Msigwa, Mkuu wa TAKURURU Heche, CAG Zitto, Uchumi Lipumba, Madini Mbatia.... madudu yataendelea tu. Ni falsafa ya Mtanzania kuwa akipata madaraka ni lazima aibe; na asipoiba akaja kuondoka madarakani hana kitu jamii hiyo hiyo inamgeuka na kuanza kumcheka na kumuita mshamba huku mafisadi yakitukuzwa kwa kuitwa matoto ya mjini, majoka makengeza....

Na kubadili falsafa ya jamii, kujenga mifumo imara na kuleta mwelekeo mpya wa jamii ni suala la muda mrefu na lenye kuhitaji vizazi kadhaa. Nyerere alijaribu sana katika hili lakini tatizo ni kwamba kumbe hata yeye alikuwa peke yake. Alipoondoka akaondoka na falsafa zake japo yeye mwenyewe alikuwa mwadilifu kabisa kabisa. Hata watu aliowaamini sana kama mwanafunzi wake Ben na komredi Kingunge nao wakaja kumgeuka na kuwa wapigaji tu. Kwa hivyo haitoshi tu kiongozi kuwa mchapakazi na mwadilifu, bila kubadili mifumo na fikra za jamii ni kazi bure.

Kwa hali ya sasa, Tanzania hii hata atawale nani (ukiwemo wewe mwenyewe), madudu na upigaji vitaendelea tu. Na ukijifanya wewe ni mkali, utakuwa na maadui wengi wa ndani na nje; na ukizubaa unaweza hata kuuliwa.

Mwendazake alijaribu sana. Tena kwa ukali mno lakini wapi. Upigaji uliendelea tu japo pengine ulipungua kidogo na ulikuwa unafanyika kwa kujificha ficha kidogo na siyo waziwazi kama kwa watangulizi wake.

Ni rahisi kuongea kishabiki kuhusu haya mambo lakini ukiyaangalia kwa undani wake ni mazito na yenye kusikitisha sana!
 
Media zilibanwa wala usizilaumu, Yani baada ya kifo chake tu ,ndio niliona kama kuna relief flan , hata huyo Cag amekuwa huru kuongelea ufisadi .
 
Nasikia KAGAME amekomesha kabisa wizi cjw alifanyaje.

Nimeanza kuamini kumbe JIWE kuondoka inawezekana ni mpango wa SIR GOD mtenda haki.

Sifurahi kifo chake lakini tulifichwa mengi.

MUNGU IBARIKI TZ, MUNGU MBARIKI SSH RAIS WETU MPYA.
 
ungehoji vipi hlf upitiwe na watu wasiojulikana??
 
Magu alikuwa corrupt kuliko rais yeyote alie wahi kuongoza hili Taifa.
Inawezekana yeye alikuwa haibi ila suala la kutokushaurika na kuruhusu watu waongee likawa ndiyo limetufikisha hapa.
 
Kwa kifupi sisi ni wanafiki na vigeugeu!
 
Pesa zimeibiwa mno sana sana
 
Yeye mwenyewe alikuwa mwizi Kwa nini akatae ripoti za wazi , CAG aliyepita walitofautiana Kwa sababu ya ukweli na uwazi , kuzima saut za Wapinzani wa ndani na nje ya chama kulitoa mwanya Kwa yeye kuiba na kuibiwa pia ....
 
Mhh,,,,,,,
 
Ndiyo maana vyombo huru vya habari vilipigwa pini, watu wamehomola kupita maelezo,haya nyie mavuvuzela ya mwendazake njooni mumtetee hapa
 
Kuungana na Pyongyang kweli? bado una hamu tena na hayo mambo πŸ˜… πŸ˜… πŸ˜…
 
Jiwe lisingeweza kuzuia ufisadi, mana alijaza genge lake ambalo lilineemaka na utawala wake.
 
Wasukuma buana,kwa hiyo huwataja hao wapinzani ndiyo utetezi kuwa meko na genge lake hawakutupiga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…