Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
MAFAO YA KIINUA MGONGO; WABUNGE WANAOGELEA.
Kiinua mgongo kwa mbunge mmoja wa Bunge la Tanzania ni Sh272 milioni baada ya kipindi cha miaka 5 akihudumu kama mbunge wa Bunge la Tanzania.
Jumla ya idadi yote ya wabunge ni 393. Wabunge wa majimbo ni 264. Wabunge wa viti maalum ni 113. Wabunge kutoka katika baraza la wawakilishi ni 5.
Wabunge wa kuteuliwa na Rais ni 10. Mwanasheria Mkuu wa Serikali 1. Jumla ya wabunge wote katika Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania ni 393.
Ukichukua kiinua mgongo Sh272 milioni ukazidisha kwa jumla ya idadi ya wabunge wote katika Bunge la Tanzania 393 unapata Sh106,896,000,000.
Malipo ya kiasi cha shilingi 272 milioni kwa kila mbunge kama mafao ya kustaafu, ni sawa na madawati 1,916 kwa bei ya shilingi 120,000 kwa dawati moja.
Kiasi hicho cha fedha za umma kinaweza kujenga nyumba tano za walimu. Kiinua mgongo cha wabunge 393 kinaweza kujenga nyumba 1,965 za walimu
.Lakini mbunge mmoja katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapata kwa kufanya kazi miaka 5 akiwa bungeni akigonga meza kutetea Serikali.Wakati waliostaafu
Bunge la 8 lililoongozwa na Spika Pius Msekwa, wabunge waliokuwepo bungeni walilipwa mafao ya kustaafu shilingi 20 milioni kila mmoja.
Bunge la 9 lililokuwa likiongozwa na Spika Samuel Sitta, wabunge waliokuwepo katika bunge hilo walilipwa mafao ya kustaafu shilingi milioni 72 kila mmoja
.Bunge la 10 lililoongozwa na Spika Anna Makinda, wabunge waliokuwepo bungeni walilipwa mafao ya kustaafu, shilingi 230 milioni kwa kila mbunge.
Bunge la 11 lililoongozwa na Job Ndugai, wabunge waliokuwepo katika bunge hilo walilipwa mafao ya kustaafu, shilingi 272 milioni kwa kila mbunge.
Malipo ya kustaafu yanajumuisha kiinua mgongo (gratuity) hii ni 40% ya malipo ya mshahara ya mbunge katika jumla ya kipindi alichotumikia bungeni.
Posho ya hitimisho la kazi (winding up allowance) ambayo ni 40% ya kiinua mgongo), posho ya usumbufu (relocation allowance) 40% ya kiinua mgongo.
Pia, inajumuisha posho ya mpito (transitional allowance). Mishahara ya mbunge ya miezi 3 na mafao ya utumishi wa mbunge. Wanaogelea mapesa.
Mafao ya Uzeeni hulipwa kwa Mwanachama aliyetimiza umri wa kustaafu kwa mujibu wa Sheria ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ya 2018.
Awe Mwanachama wa PSSSF. Awe amechangia kwenye Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi 180 au miaka 15. Awe ametimiza umri wa kustaafu kisheria,
Mwanachama mstaafu aweze kupata Pensheni ya Uzeeni, inabidi kuwasilisha fomu PS-BEN.1 ambayo imejazwa vyema pamoja na viambatanisho.
Umri wa kustaafu kwa hiari wa miaka 55 na kwa lazima ni miaka 60. Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anahitaji miaka 5 tu kulipwa mafao.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Kiutoka mtandao wa X