Kwa mafundi fridge, naombeni msaada wenu

Kwa mafundi fridge, naombeni msaada wenu

Godee jr

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2012
Posts
1,836
Reaction score
2,536
Fridge langu mlango wake haubani vizuri. Yaani ukifunga kunabaki upenyo unaosababisha baridi kutoka nje. Najua Kuna zile lock Kama za milango ya nyumba lakini kwangu naona kama ni za kizamani Sana na zinaaribu muonekano wake.

Naomba kujua kama kuna lock za kisasa au ambazo zinatumika sumaku au hata kama zile zinazofunga makabati ya kioo ambazo naweza kuzitumia

JPEG_20210528_110632_1580157084447401886.jpg

Hiyo seal/gasket (iyo nyeupe kuzunguka mlango wa friji) aidha imetoka kwenye njia yake (groove) so inaitaji kubanwa vyema au

Lining ya sumaku ndani ya iyo seal haina nguvu tena, hapa utahijati kununua seal mpya kwenye maduka ya spare za friji (KKoo kule kuna maduka mitaa ya Kisingani na Nyamwezi)
 
Nahisi ni sumaku ndio imeisha nguvu mkuu. Asante kwa ushauri wako
 
yangu ilifanya hivyo nikaona isiwe tabu nikagongelea kile kidude kama cha kuwekea kufuli hivi ikabana sasa hivi hata nisipobana inabana yenyewe
 
yangu ilifanya hivyo nikaona isiwe tabu nikagongelea kile kidude kama cha kuwekea kufuli hivi ikabana sasa hivi hata nisipobana inabana yenyewe
Mi sitaki kugongea hicho kidude aisee. Bado nataka ibaki na muonekano wa upya wake ingawa Ina miaka 3
 
Mi sitaki kugongea hicho kidude aisee. Bado nataka ibaki na muonekano wa upya wake ingawa Ina miaka 3
Miaka 3 tu kweli mchina sio poa. Unaona zile used,zina miaka zaidi ya 10 na milango inabana mpaka linakufa.
 
Ni rahisi kuna raba imezunguka mlan
Mi sitaki kugongea hicho kidude aisee. Bado nataka ibaki na muonekano wa upya wake ingawa Ina miaka 3
Kuna raba nyeupe imezunguka mlango kwa ndani sasa uwenda ni chafu au imejikunja au imeisha ubora wake uangalie hiyo na inapatikana kariakoo nunua nyingine weka
 
Miaka 3 tu kweli mchina sio poa. Unaona zile used,zina miaka zaidi ya 10 na milango inabana mpaka linakufa.
We acha tu mkuu. Ila wameandika Warrant ya 5 years. Sijui hiyo warrant inacover nini na nini
 
Ni rahisi kuna raba imezunguka mlan

Kuna raba nyeupe imezunguka mlango kwa ndani sasa uwenda ni chafu au imejikunja au imeisha ubora wake uangalie hiyo na inapatikana kariakoo nunua nyingine weka
Yaah. Nimeangalia leo naona sumaku yake imeisha nguvu. Nimejaribu kupitisha kisu naona hakuna sumaku kabisa
 
Toka nimtafute fundi fridge akaja kuongeza gas kwa kutumia mwanga wa mshumaa sina imani nao tena hawa mafundi, kilichomtokea nadhani ataweza sahau maishani kwake sijua ata kama anaendelea na iyo fani.
 
Yangu leo naona taa ya mlango wa chini haiwaki na ubaridi haupo.

Sijui tatizo nini na ina miaka miwili mitatu tu!
 
Hivi ikiwa taa inawaka ila halipoozi ndio gesi inakuwa imeisha?
 
Back
Top Bottom