Ili uondokane na umasikini wa kipato ni sharti na ni lazima ufanye kazi kwa bidii,juhudi na maarifa.Ni lazima ujitume kwelikweli,ni lazima ujitoe na kuwa na malengo mazuri,ni lazima uzitumie vyema fursa za kiuchumi zinazopatikana katika eneo lako au nje ya eneo lako,ni lazima uwekeze katika miradi mbalimbali na uweke akiba na hiyo akiba izalishe na kuleta faida na hiyo faida ilete na kuongeza mtaji wako.
Usipofanya kazi kwa bidii ,ukabweteka tu.Nakuambia utailaumu serikali mpaka siku zako za maisha ya hapa Duniani zitakapo koma.kazi ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa wewe na mimi mwananchi kufanya kazi kama ifanyavyo serikali ya Rais samia.mfano kwa sisi wakulima serikali imeweka mazingira wezeshi na rafiki kwa mkulima kuinuka kiuchumi kwa kutoa mbolea za Ruzuku,kuweka soko la uhakika,kuweka sera rafiki kwa kilimo na mkulima,kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa pembejeo na kwa bei nzuri, kujenga miundombinu ya barabara inayosaidia katika kusafirisha mazao yetu kulifikia soko kwa urahisi.
Kwa hiyo kwa sisi wakulima hiyo ni fursa kwetu ambayo tukitumia vizuri hakuna atakaye bakia katika umaskini .lakini kama ukikaa utajikuta wewe unabaki maskini na wenzio wanapiga hatua mbele za maendeleo halafu wewe unabakia unalalamika kila siku,kana kwamba unataka serikali ije ikulimie shamba huku wewe umejiegesha nyumbani kwako