Kwa Makala Hii ya Daraja la Kigamboni Mwanakijiji Kachemsha

Mchambuzi, Waberoya,

..sidhani kama WB waliishauri serikali iuze nyumba za serikali plus plots kwa bei ya hasara kiasi kile.

..zaidi sidhani kama WB tena waliishauri serikali ijenge nyumba nyingine kwa bei ya kuruka.

..mara nyingi Watanzania tunaboronga wenyewe halafu tunawasingizia WB na IMF.
 
Nina hakika hilihalikufanyika bila utaalam na wataalam. Kilichotokea ni kuwa wanasiasa walijua kuwa wao ndio watakaofaidika na mpango huo. Hakuna aliye raise concern au kusimamia concern kama ilitolewa na wataalam.

Ilikuwa rahisi kujiuliza , 'sisi mawaziri tutaishi wapi na usalama wetu utakuwaje'. Kuanzia hapo jibu lingekuwa wazi.
Uwezekano wa kurudisha NHC haukuwepo kwasababu ungeingilia mpango mzima wa jinsi walivyojipanga kugawana nyumba.

WB wanachukizwa ziadi na kujenga nyumba ghali kwa mantiki yako kuwa wanataka kile kidogo wakichukue.
Hata hivyo tukubali kuwa WB hawatuzuii kufikiri, na tumekuwa wepesi sana wa kuwalaumu hata kwa mambo yaliyo katika uwezo wetu

WB wametumika kuhallaisha uuzaji wa nyumba kwa njia ya sadaka na kukwepa njia muafaka.

Mimi sikubaliani na neno 'back fire' kwasababu hii haikuwa coincidence, ilikuwa ni well calculated, designed and executed move under the usual banner of moral decay.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…