Kwa Makala Hii ya Daraja la Kigamboni Mwanakijiji Kachemsha

Kwa Makala Hii ya Daraja la Kigamboni Mwanakijiji Kachemsha

Hivi leo likitokea gazeti jingine lina makala yenye kusifia serikali kuhusiana na mgomo wa madaktari na mwandishi ni "mwanakijiji" na watu wakashambulia imekuwaje nimeacha kusupport madaktari si ni haki kwangu kutoa maelezo? Nikipitia hiyo inayodaiwa kuwa ni makala na kugundua ni mkusanyiko wa maandishi yangu na nyongeza za mhariri bado nadaiwa kutoa maelezo? Nikiwaelekeza watu kwenye makala pekee niliyoandika juu ya somo na kwaambia hiyo makala iliyowekwa jina langu sikuandika wala kutuma bado notadaiwa kutoa maelezo? Wanaosema nioneshe without reasonable doubt kuwa sikutuma ndiio wataamini nawapa challenge: pendekezeni njia moja tu ya mimi kuweza kuonesha sikutuma makala hiyo zaidi ya kauli yangu kuwa sikutuma.

nimekuelewa!!

However, tell Kubenea that anafanya mambo ya zamani ya akina Kolimba not fair! anaandika yeye anajifanya kaandika mtu mwingine!!
 
Haijalishi kwani kama lengo lao ni kumchafua magufuli, hayo magazeti yao - ni asilimia 21% tu ya watanzania ambao source zao za news ni magazeti, tena on a weekly basis, not daily basis. Na hawa 21% ni pamoja na wale wanaoambiwa na ndugu, jamaa na marafiki zao kwamba gazeti fulani limeandika hiki na kile. Otherwise magazeti hayafikii zaidi ya 2% of the population on a daily basis. Habari hizo waziweke basi angalau front page, sio ndani kwani hata wewe umeikuta kwa bahati mbaya. Zikikaa mbele, basi katika pita pita ya vichwa vya habari kwenye radio zinazokamata nchi nzima majira ya asubuhi, angalau umma utasikia vijembe hivyo vinavyokusudiwa na wahusika, kwani zaidi ya 70% ya watanzania, source yao za habari ni radio (za simu na za kawaida combined, na mara nyingi huwa ni asubuhi.

Vinginevyo hata kama nani.... angekuwa ndiye Waziri wa ardhi, nyumba za serikali zingeuzwa tu. Inasemekana WorldBank ndio walioshinikiza hilo baada ya kuona serikali inapoteza fedha nyingi to maintain them, but only to build them again later baada ya malalamiko kuanza kuleta athari za kisiasa. But the bottom line is, serikali haistahili kumiliki utitiri wa nyumba namna ile, unless zingepelekwa kwa national housing ili zisaidie shirika lile kufanikisha malengo yake mbalimbali.

Magufuli na EPA, is a non - starter.

Magufuli na Kigamboni - pengine kinachowaumiza ni kwamba huo ni moja ya miradi michache inayoonekana kwamba itatekelezwa na serikali ya awamu ya nne, nje ya mradi wa richmond.

Lol! utafukuzwa chamani mkuu!

Kigamboni bridge is a bridge towards other scandals, daraja halina umuhimu sana, priorities zetu hazina priority. Reli ni muhimu zaidi
 
...
Vinginevyo hata kama nani.... angekuwa ndiye Waziri wa ardhi, nyumba za serikali zingeuzwa tu. Inasemekana WorldBank ndio walioshinikiza hilo baada ya kuona serikali inapoteza fedha nyingi to maintain them, but only to build them again later baada ya malalamiko kuanza kuleta athari za kisiasa. But the bottom line is, serikali haistahili kumiliki utitiri wa nyumba namna ile,....
Hapa nashindwa kukuelewa. WB wameshinikiza watawala kuuza nyumba......watawala kwa woga wao wakakubaliana na WB wakauza nyumba.....baadae huo woga umewaisha wameanza kujenga tena nyumba!

Mimi nadhani tuache visingizio....watu wabebe dhamana ya kile wanachofanya. Hatuishi kusingizia watu kutoka nje kama sababu za kushindwa au kuboronga kwetu. Kwenye suala la uuzaji wa nyumba Mh Magufuli anabeba the biggest chunk ya lawama kwa kushindwa kufanya maamuzi yenye maslahi mapana kwa Tz.
 
Inabidi wananchi waelewe madudu haya ya IMF, WorldBank, ushauri wao na madhara ya ushauri huo katika uchumi wetu. Ni muhimu sana-sana wananchi waelewe hili. Hata mradi wa umeme wa mchuchuma, ni hawa ndio wamekuwa wanauzuia kwa muda mrefu kwasababu IFC (biz wing ya worldbank), wana hisa katika mradi wa gesi ya songosongo, na umeme wa makaa ya mawe utaitoa biashara ya umeme wa gesi from the map in a minute. Worldbank wanataka kwanza angalau payback period ya investment yao isogee sogee, na tunakaribia huko.
 
Lets be realistic ndugu

Ulitaka Magufuli akatae order hiyo?

Order kutoka IMF na WB nchi hii zimeanza lini?, tangu enzi za nyerere... wanasema hiki na kile tunakipokea!! leo hii Magufuli akatae ataweza wapi? na inapitia kwa bosi wake, ikajadiliwa na baraza la mawaziri na ikawa hivyo!! hana ubavu huo!! Lawama m'bebeshe ila hakuna Tanzania hii ya leo mwenye ubavu wa aina ya akina Mugabe, hayupo!

Mtu ambaye ana siasa za kiburi na kuweza kuwagomea watu wa nje ni caliber ya Lissu,
 
This is the effect of neo-colonialism.

Tangu tulipokubali kuingia kwenye globalization/free market na kuwa tied na hawa jamaa basi nchi inaongozwa na WB/IMF kwa ukaribu zaidi. Ngau enzi za Nyerere alikuwa na ubavu wa kusema no!

Mkuu kipi kifanyike??, maana yake bado lawama zitawaangukia viongozi, why are they silent in these matters? maana miradi mingi ni WB/IMF this and that!

Is it possible in anyway tukajiondoa kwenye free market na kujivua urafiki na hizi organisation? even if we are going to die?
 
Lets be realistic ndugu

Mtu ambaye ana siasa za kiburi na kuweza kuwagomea watu wa nje ni caliber ya Lissu,

Umenifurahisha sana kuhusu Lissu. Mtu huyu anaogopwa sana na uongozi wa CCM kuliko watu wanavyodhania. Wengi walitoa maoni kwamba mara kumi Slaa aingie ikulu lakini sio Lissu Bungeni. Ingawa inawezekana hawakuwa serious lakini ni ujumbe mzito.
 
Mkuu kipi kifanyike??

Is it possible in anyway tukajiondoa kwenye free market na kujivua urafiki na hizi organisation? even if we are going to die?
It's not a top-down kinda solution.
Hii inabidi itoke kwa watu/watanzania.
Angalau wachina wanaingia ubia na sisi kwenye baadhi ya miradi.
 
Lets be realistic ndugu

Ulitaka Magufuli akatae order hiyo?

Order kutoka IMF na WB nchi hii zimeanza lini?, tangu enzi za nyerere... wanasema hiki na kile tunakipokea!! leo hii Magufuli akatae ataweza wapi? na inapitia kwa bosi wake, ikajadiliwa na baraza la mawaziri na ikawa hivyo!! hana ubavu huo!! Lawama m'bebeshe ila hakuna Tanzania hii ya leo mwenye ubavu wa aina ya akina Mugabe, hayupo!

Mtu ambaye ana siasa za kiburi na kuweza kuwagomea watu wa nje ni caliber ya Lissu,
Nisome tena hapo juu! Kama WB hawataki serkali iwe na nyunba imekuwaje tunajenga tena? Woga uneisha au shinikizo limeondolewa? Kama tuna ubavu wa kujenga tena ilikuwaje vigumu kukataa kuuza?
 
This is the effect of neo-colonialism.

Tangu tulipokubali kuingia kwenye globalization/free market na kuwa tied na hawa jamaa basi nchi inaongozwa na WB/IMF kwa ukaribu zaidi. Ngau enzi za Nyerere alikuwa na ubavu wa kusema no!

Mkuu kipi kifanyike??, maana yake bado lawama zitawaangukia viongozi, why are they silent in these matters? maana miradi mingi ni WB/IMF this and that!

Is it possible in anyway tukajiondoa kwenye free market na kujivua urafiki na hizi organisation? even if we are going to die?

You are right. Ila swali gumu sana Mkuu. Kwa mtazamo wangu, tuna options mbili. Ya kwanz ni kuweka jitiada za dhati tuondokane na utegemezi wa wahisani kuchanguia bajeti zetu za kila mwaka tangia uhuru. Na given rasilimali tulizonazo, nadhani tukiwa na malengo, tutaweza fanikisha hili ndani ya miaka hata saba. Kenya waliweza na hawana rasilimali za ajabu, kwanini sisi tushindwe? Tukimaliza hilo la kuondokana na bajeti tegemezi, tunaweka bidii kulipa madeni yao yote sustainably, hata kama itachukua miaka 30, lakini tuweke msingi mzuri wa kuzalisha, kuendesha na kulisha taifa vizuri including huduma za kijamii, lakini pia kutotibua debt repayment...;

Option ya pili mbali ya hii ni kujibwaga kwa wachina na kushirikiana nao katika miradi yote ya maana, kuanzia migodi mipya ya madini, mafuta, gesi etc, huku serikali ikikamata hisa angalau 25% kwenye kila mradi. Pia serikali kulazimisha kupewa free shares na migodi yote iliyopo operational hivi sasa. Lakini kuhusu China, wakubwa wanapishana sana katika hili, kuna wanaotaka tutegemee west, na kuna wengine wanaotaka tutegemee east. Mama clinton alipokuja juzi, moja ya agenda yake na wakuu ni kuhusu wachina kushika utamu wa rasilimali za afrika.

All in all, tatizo letu ni population growth, ni kubwa sana kwani inakaribia 3% annually na imekuwa hivyo for almost 20 yrs now. Feeding this population, bila kuvuna from it in terms of tax etc, ni mzigo mkubwa sana. Uchumi unatakiwa kukuwa atleast twice ya popn growth, lakini ukuaji wenye benefits kwenye communities, sio ukuaji wa sasa wa kuchota chota gold isiyo na manufaa zaidi ya kupaisha GDP growth kuwa on average at 7% since 2000, growth that doesn't trickle down to the needy. Ukitoa suala la Gold exports from the equation ya GDP yetu, na uchanganye na capital flight, mgao wa umeme, etc, economic growth yetu ipo chini sana, pengine hata 4% a year;
 
Nisome tena hapo juu! Kama WB hawataki serkali iwe na nyunba imekuwaje tunajenga tena? Woga uneisha au shinikizo limeondolewa? Kama tuna ubavu wa kujenga tena ilikuwaje vigumu kukataa kuuza?

Tatizo lingine kubwa ni kuwa uhusiano wa WB na serikali zetu ni wa kudanganyana sana, kuna possibility kuwa zinajengwa bila WB kujua, au wanatoa sababu na kutengeneza policy ambayo WB wameikubali. We need to know deeply what happened
 
In addition, WorldBank wao wanachotaka ni serikali kupunguza matumizi, hata kama wananchi watakufa njaa. Wakati wa mkapa kulikuwa na ule mpango wa kuzisamehe nchi madeni i.e. HIPC initiative ambayo ilikuwa ni danganya toto tu to a large extent. HIPC ilikuja na masharti yake mengi, lakini kubwa likiwa austerity measures on part of our government. WorldBank wana tabia ya kutaka hela wanazotoa ziende kwenye vitu wanavyotaka wao, sio kweney vitu tunavyotaka au tunavyoamua sisi, ndio maana AID Conditionality ni tatizo kubwa sana. Kuuza nyumba za serikali kunawasaidia WorldBank and group vitu vitatu vikubwa: Moja, serikali inapata hela ya kuendesha mambo yake mengine hivyo kupunguza mikopo toka nje ambayo inailemea nchi, huku chances za defaults zikiwa kubwa; na pili, serikali inakusanya hela kutokana na mauzo hayo ambapo sehemu ya fedha hizo uende ku service the debt; na tatu, related to sababu ya kwanza - serikali inaacha kutumia hela kuhudumia nyumba hizi, na badala yake zinaenda kwenye maeneo amabyo worldbank wanataka, maeneo ambayo wao wanasema ni muhimu to stimulate economic growth. tumeona hiyo economic growth very impressive ya 7% avg for 12 yrs now, but guess who benefits? Wawekezaji ambao wanatoka katika nchi zenye shares in the WorldBank. Worldbank inaendesha mambo yake kama vile tu Exim au CRDB. Hawapo hapa kama wasamaria wema.
 
Nisome tena hapo juu! Kama WB hawataki serkali iwe na nyunba imekuwaje tunajenga tena? Woga uneisha au shinikizo limeondolewa? Kama tuna ubavu wa kujenga tena ilikuwaje vigumu kukataa kuuza?
Kujenga tena wapi?
 
Kusema daraja la kKgamboni halina umuhimu kwa taifa nadhani ni kuto watetendea haki wakazi wa Kigamboni ambao maisha yao kwa ujumla yanategemea sana uvukaji wa kipande kile
Hapa issue ni vipaumbele tu, viongozi hawana vipaumbele. tuna mahitaji mengi mno katika taifa hili tatizo ni namna ya kujua na kutambua kipi kianze kurahisisha vingine na kipi kifuatie.
Hivyo daraja la Kigamboni ni muhimu kwa taifa lakini kuna mambo mengine muhimu zaidi yalipaswa kupewa first priority kuliko daraja la kigambo labda kama linajengwa kwa basis ya kibiashara zaidi
 
Tatizo ni kuwa gazeti gani limeandika?
Hata hiyo makala ya TD haina ukweli ndani yake.Ni makala iliyojaa opinions rather than facts.
Sioni mnachobishana.
SOBY, hivi kumbe makala ndizo zinatakiwa kujaa facts!?. Jee opinions ndio huwa "hard news"?.
Kwa kusaidia tuu, lengo la chombo cha habari ni
1. Kuhabarisha-Kupitia habari, hapa hakuna kuweka opinion.
2. Kuelimisha-kupitia makala-hapa opinion inaruhusiwa.
3.Kuburudisha-kupitia hadidhi, katuni etc, burudani, michezo etc hapa mpaka kubuni ruksa!.

JF nayo kama social media, majukumu yetu pia ni hayo hayo, hivyo naomba kuchukua fursa hii kukuelimisha kuhusu makala.

Ukiona makala yoyote, haswa zile za kawaida, yale waliyaandika waandika makala ndio maoni yao, hivyo kwenye makala ile ni mawazo ya MMKJJ, na Waberoya pia anaouhuru wa kuandika makaya yake ama kuijibu hiyo ya MMKJJ au ya kwake nyingine yoyote!.
 
Nakala hii imebeba mambo matano makubwa

1. Historia ya daraja la kigamboni
2. Ufisadi
3. Uwezo na tabia ya magufuli
4. NSSF na kutoa misaada
5. UUzwaji wanyumba za serikali

Update:

1. Imeeleweka na muanzisha thread kuwa MMKJJ hakupeleka ile nakala Mwanahalisi, mwanahalisi waliichukua nakala yake kutoka Tanzania Daima na kuifanyia editing

2. Tunajadili sasa nyumba za serikali kwa nini ziliuzwa

3. Umuhimu wa daraja la Kigamboni

My take:

Daraja la Kigamboni halina faida kwa Tanzania ya sasa inayoanzia Kigoma mpaka Dar, inayoanzia Nachingwea mpaka Biharamulo!!! ukisasa huu tunaoutafuta hatuja tengeneza foundation yake.

Daraja hili ni mradi wa watu wachache ili watimize ndoto yao ya kijenga jiji la kimataifa! is not ours

MODS NAOMBA TITLE YANGU YA AWALI IRUDI.....I expected this!
Mkuu Waberoya, kwa vile thread ilianza na mashambulizi ya makombora ambayo hatimaye yalipanguliwa, kuigeuza igeuke discussion ya tija ya daraja la Kigamboni, haitapata mashiko yanayostahili, nakushauri anzisha thread yingine kuhusu daraja na mji mpya wa Kigamboni tutakumwagia mpaka data.

Kama kivuko cha feri kimeshapoteza maisha ya zaidi watu 100, then daraja la Kigamboni, hata likigharimu bilioni 1000, kama lita save just one life!, its worth it!.
 
SOBY, hivi kumbe makala ndizo zinatakiwa kujaa facts!?. Jee opinions ndio huwa "hard news"?.
Kwa kusaidia tuu, lengo la chombo cha habari ni
1. Kuhabarisha-Kupitia habari, hapa hakuna kuweka opinion.
2. Kuelimisha-kupitia makala-hapa opinion inaruhusiwa.
3.Kuburudisha-kupitia hadidhi, katuni etc, burudani, michezo etc hapa mpaka kubuni ruksa!.

JF nayo kama social media, majukumu yetu pia ni hayo hayo, hivyo naomba kuchukua fursa hii kukuelimisha kuhusu makala.

Ukiona makala yoyote, haswa zile za kawaida, yale waliyaandika waandika makala ndio maoni yao, hivyo kwenye makala ile ni mawazo ya MMKJJ, na Waberoya pia anaouhuru wa kuandika makaya yake ama kuijibu hiyo ya MMKJJ au ya kwake nyingine yoyote!.
Opinions are based on facts..... you are entitled to yuor own opinion, but your not entitled to your own facts.
Opinions that aren't based on facts are vague and benign.

Facts are based on observations, facts that aren't based on observations are prejudicial and unsecured.

Observations, in order to deduct facts, should be with no prejudice. That is to say, they should prefarably be confirmed by more than one observer and agreed upon that observation.
Other than that...... utakuwa unaandika hekaya.
 
Inabidi wananchi waelewe madudu haya ya IMF, WorldBank, ushauri wao na madhara ya ushauri huo katika uchumi wetu. Ni muhimu sana-sana wananchi waelewe hili. Hata mradi wa umeme wa mchuchuma, ni hawa ndio wamekuwa wanauzuia kwa muda mrefu kwasababu IFC (biz wing ya worldbank), wana hisa katika mradi wa gesi ya songosongo, na umeme wa makaa ya mawe utaitoa biashara ya umeme wa gesi from the map in a minute. Worldbank wanataka kwanza angalau payback period ya investment yao isogee sogee, na tunakaribia huko.

Mkuu hapa ndipo serikali yetu inapoingia matatani, maana wao wamewekwa na wananchi kutuwakilisha kwenye mambo kama haya. Kawaida inatkiwa waangalie priority zetu kwa naiba yetu!! Kwa kweli lile daraja halitufai, hatulihitaji na halina tija yeyote kwenye kutuendeleza sisi kama wananchi!

Wao wanatekeleza matakwa ya kina-GWB na huo mji wao!! Fikiria hali ya uchumi wetu, hadi hii leo serikali bado haijaona umuhimu wa kuboresha reli yetu ya kati na kuiongeza ili bandari ya Dar iwe efficient!!! Economically huwezi kutofautisha reli na bandari, its just not possible, you will wonder it is very true in TZ.

Kwanzan huo mji utapoata wapi umeme!! Katika mipango yap ya muda mrefu hatujaona plan za dhati kwenye power!!! Hizi ni hadithi za pwagu na pwaguzi...
 
Kujenga nyumba za serikali kinyume na matakwa ya WB kama Mchanbuzi anavyotaka tuamini.

World Bank advised against serikali kumiliki nyumba, just as they advised against serikali kumiliki public companies back in the days. Kama unaelewa logic behind Foreign Aid with conditionality, World Bank, IMF, Donor community hawataki fedha zao ziende kwenye matumizi yasiyokuwa na tija kwao bali ziende kwenye sekta ambazo zita stimulate economic growth ambayo ofcourse kwa miaka 12 sasa 7% average on that imewafaidisha wao tu, huku sisi tukikubali kwamba njia hiyo itatusaidia kumaliza umaskini. Sasa kama serikali ina fedha zake zenyewe from Gold Exports etc na kuamua kuzitumia kujenga nyumba au hata kumbi za sinema, World Bank hawajali sana hilo ilimradi matumizi hayo yasitokane na fedha za walipa kodi wao kwani fedha za walipa kodi wao have to go in areas where world bank believes ina add value to their 'cause'; lakini vilevile wanajaribu sana kubana matumizi ya serikali haat yanayotokana na mapato yetu wenyewe, yasi jeopardize malipo ya madeni yetu kwao i.e tusi default madeni. Huu ni ukweli that we gotta live with;

Serikali kumiliki nyumba nyingi so sahihi, lakini kuziuza kwa bei ya chini pia haikuwa sahihi, badala yake zingepelekwa National Housing, huku serikali ikibakisha nyumba chache kwa ajili ya viongozi kadhaa. Lakini obviously mpango huu uka back-fire both kisiasa lakini pia kimantiki tu kwani ilianza kuwa ngumu kwa mawaziri wapya au makatibu wakuu to commute from kiluvya, kigamboni etc, pamoja na argument kuhusu usalama wa viongozi huko kwenye makazi yao; It back fired just like advice za WorldBank na IMF kuhusu serikali kujitoa kwenye elimu, afya, etc, only for them to ask the government kurudi tena, na ndio maana tunaona shule za kata etc. WorldBank na IMF wana nguvu katika maamuzi yetu kwa sababu moja tu - we depend on their finance kwenye bajeti yetu ya maendeleo na ya kulipa mishahaar watumishi wa serikali. Ni hilo tu. Tukijikwamua toka kwenye hilo, tutapiga hatua kubwa sana na kumbakisha mdudu mmoja tu - WTO;
 
Back
Top Bottom