Kwa makusanyo yaliyopatikana kupitia ofisi ya DPP ni dhahiri Wapinzani muache kupinga kila jambo

Kwa makusanyo yaliyopatikana kupitia ofisi ya DPP ni dhahiri Wapinzani muache kupinga kila jambo

Unaongea nini Mkuu? Plea guilty unaijua au huijui? Mtu amekiri kosa na akawa tayari kulipa faini kwa DPP shida iko wapi? Kama anaona kulipa faini anaonewa asubiri aende mahakamani. Nchi ilikuwa shamba la bibi hii. Kuna muda namkubali JPM sana, kuna wakati tajiri alikuwa na uwezo wa kufanya chochote na hakuna wa kuhoji.
una mwambiaje mtu asubilie kesi yake iende mahakamani wakati unamuweka ndani miaka 5 eti upelelezi haujakamilika? Hayo ni mazingira tosha ya kumtisha mtu akili makosa yake ili mdhurumu pesa yake. Lkn tunasema iko cku mtajibu mbele ya haki, Kama sio nyie basi watoto wenu watawajibia cku haki ikisimama
 
Kwanza jambo la ajabu Sana unamkamataje mtu wakati ushahidi huna? Yaani mtu anakamatwa anawekwa ndani baadae ndio upelelezi unafwata hiyo ni haki gani?. Matokeo yake mtu anasota ndani pasipo sababu ya msingi. Hiyo yote ni hujuma ya serikali dhidi ya watu wake kwa kuwatesa ili kuwatoa hela zao.
pelelezeni kwanza ili mkimkamata mtu mnakua na ushahidi wa kutosha na kesi inaenda haraka na mtu anapata haki yake ya kuhukumiwa
 
Wanabodi hapa JF ninyi ni mashahidi jinsi wapinzani Tanzania walivyopinga utaratibu wa kisheria wa mtuhumiwa wa baadhi ya makosa ya jinai hasa uhujumu uchumi kuingia mkataba na Dpp ili kukiri kisha kulipa na kurejesha walichokuwa wamewaponza watanzania.

Utaratibu huu ulipata baraka za Bunge la Tanzania. Kifungu cha 194 cha CPA kilifanyiwa marekebisho,na mtuhiwa wa makosa hasa jinai anaweza kuingia makubaliano na Dpp kisha kulipa kile acho hujumu.

Nia hasa ya kuleta huu utaratibu ni kuwezesha kesi kuisha kwa uharaka na kupunguza msongamano wa mahabusu gerezani. Lakini jambo ambalo wapinzani wa hapa Tanzania walikengeuka na kuanza kueneza uongo kuwa huu utaratibu umewekwa ili kumnufaisha DPP.

Maneno na porojo nyingi zimetangazwa hapa Tanzania. Mara DPP amepewa mtaji wa kujinuisha,mara huu utaratibu wa kisheria umewekwa kuwakamua wapinzani na wakosoaji wa serikali iliyipo madarakani.

Leo hii kuna gazeti la hapa Tanzania limetoa takwimu kuwa Bil 123.6 zimekusanywa kupitia ofisi ya DPP. Hii ni habari njema sababu pesa hizi zimekusanywa kwa mujibu wa sheria. Na nia kuu ni kuhakikisha waliofanya makosa hawakai rumande muda mrefu,huku magereza yakipumua maana mrundikano wa wafungwa na mahabusu ni mkubwa.

Oni langu, wapinzani msiwe mnakurupuka kupinga kila kitu kisa tu mnatafuta kick kwa wanachi .
Unamaliza mwaka kwa kusifu ajira ya ujambazi kuwa imepunguza umasikini! Wewe si bure! Utakujasifu mkeo akileta kitita cha pesa toka kwa mshikaji wake!
 
Kwani sheria kupita bungeni ndio sio kandamizi? Ni sheria ngapi kandamizi zimepita ndani ya hilo bunge kibogoyo, mpaka ikabidi mataifa ya nje ya kaweka mbinyo ili zibadilishwe?
Ahaaa, unataka kuzungumzi ishu ya takwimu?. Vinalandana na mafisadi kutapika walichokwapua?

Sheria kama haina maslahi kwa umma inarekebishwa na bunge ili ilete maslahi kwa umma.

Kwa hiyo sheria ya takwimu kubadilrishwa sioni kama ni tatizo.
 
Tuanze na nyumba za serikali thamani ya zilivyouziwa hazilingani na thamani halisi ya maeneo husika ni ufisadi Mkubwa sana umetumika pale. Tunaomba yeyeto atakaeshika madaraka haijalishi ni lini arudishe nyumba zote hizi ziliuzwa kihuni, atumie sheria ya utaifishaji. Kama kuna aliyeziendeleza ile kwake abebe jengo lake atuachie nyumba zetu.
Mfano MAGUFULI alinunua magorofa ya NIC Kwa ml 6 kila moja mbona hajarudisha? Aliwanunulia nyumba kina kabula wakati siyo watumishi wa umma mbona hawajakili makosa na kurudisha???
 
Kama joka la makengeza liko nje means Vita ya ufisadi ni maalumu kwa wasio na chapa pekee
 
Kwa nini usikae kimya?
Kuxungumza na kutoa maoni ni haki yangu .mmezoea kuskikika wenyewe tu hata mkiongea upuuzi na uongo mnasifiana kama majuha vile??? Unasifia serikali kupitia DPP kupora pesa za watu lakini hutaki kuambiwa ukweli kwamba serikali kupitia wazir wa nyumba wakati huo sijui ulikuwa wapi ulishawahi kuuza na kagawa nyumba za umma mpaka kwa hawala kina kabula
Namzungumzia huyu anayeitwa mzalendo leo bwana MAGUFULI ambaye alishawahi kukagua Nyumba za shirika za NIC huko dodoma kwa ml 6 tena kwa mkopo? Kama anauchungu na nchi azirejeshe kwanza tuone
 
Back
Top Bottom