Ghiti Milimo
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 4,748
- 7,061
Wakuu, salaam zenu!
Moja kwa moja kwenye mawazo yangu. Nimefikiria sana, style ya Mh. Tundu Lissu, ya kuutaka Uenyekiti wa chama chao, nimeona inaweza kuleta athari fulani.
Yeye mwenyewe amesema, ameshawishiwa na wadau, agombee hiyo nafasi! Sina shaka, baada ya hao wadau kuona aliyepo HATOSHI, na Mh Lissu kukubaliana nao, kuwa Mh Mbowe, kweli hatoshi, na "anang'ang'ania madaraka"! Kwa mujibu wa Katiba yao, na Demokrasia kwa ujumla, wana haki, si Lissu tu, bali kwa Mwanachama yeyote mwenye sifa.
Sasa, mimi nilitegemea, kwa kulinda umoja wa Chama chao, wasingetoa nafasi kwa hao Vigogo wawili, kugombea nafasi moja. Hao hao waliomshawishi Lissu, agombee Uenyekiti, wangetumia kila njia, kumshauri na kumshawishi aliyepo sasa, yaani Mbowe, asigombee. Na Mbowe mwenyewe, atangaze kuwa, kwa sasa hatagombea.
Baada ya hapo, wanachama wengine wajitokeze, pamoja na Lissu, ambaye tayari alishakijulisha Chama kuwa atagombea U Makamu, naye atangaze anabadilisha nafasi, na kugombea Uenyekiti. Sina shaka, angeungwa mkono na wapiga kura wengi!
Pamoja na hayo, kwa jinsi nilivyoisikiliza vizuri hotuba yake, ile siku ya kutufahamisha kuwa anautaka Uenyekiti, (hakuwa anatangaza nia, kwani alitangaza kuwa alishapeleka barua kwa Katibu mkuu, kuwa atagombea hiyo nafasi) ilionyesha wazi kuwa ana kinyongo fulani, kwa Mwenyekiti wake.
Na alionyesha, hana heshima kwa Mwenyekiti wake, kutokana na maneno yake. Kwa mfano, aliposema kuwa, Mzee Mtei na Mzee Bob Makani, "hawakung'ang'ania madaraka" kwa muda mrefu, na kuamua kuachia uongozi mapema, ili "wasiondolewe uongozini kwa aibu"! Kwa sentesi hii, Lissu alikuwa anatuambia kuwa, sasa Mbowe anaelekea kuondolewa uongozini kwa aibu!
Pia, siku mbili kabla, Mbowe wakati akiongea na waandishi wa habari, na Mh. Lissu akiwepo, alisema yeye bado yupo sana, kwani bado ana nguvu za kukitumikia chama. Lakini, Lissu kwenye mkutano wake, akionyesha kuwa Mbowe "kisha zeeka", alikumbushia, na kusisitiza kuwa, Mzee Mtei, "hakung'ang'ania madaraka", alistaafu akiwa na miaka 65.
Maneno yake mengi, yalikuwa yanaonyesha kuwa Mh. Mbowe "anang'ang'ania madaraka"!
Ukifuatilia "mabadiliko" ya Lissu, utagundua kuwa yamekuja kuelekea kwenye hizi chaguzi za ndani za chama chao. Na inaonyesha "AMEKASIRISHWA" sana na baadhi ya wagombea fulani, kushindwa, wakiongozwa na Mchungaji Msigwa.
Hapo ndipo alipoanza kukituhumu chama chake, kwa tuhuma ambazo kwa nafasi aliyonayo, alitakiwa kwenda kuziongelea kwenye vikao vyao vya ndani, na si kwenye mikutano ya hadhara, au kwa waandishi wa habari.
Na inaonyesha, zile tuhuma anazozitoa Mchungaji Msigwa, kwa Mbowe, yeye anazifurahia. Cha kushangaza, anasema CHAMA kimjibu. Hivi chama ni nani? Kwa hiyo, yeye si sehemu ya chama? Na mapenzi yake kwa Msigwa, hayafichi, na kudai Msigwa ni sehemu ya waokozi wa maisha yake, kwa kushikilia chupa ya damu, akiwa kwenye ndege akipelekwa Kenya kutibiwa.
Soma Pia: Tundu Lissu achukua rasmi Fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA
Ninachokiona, wale wapambe/chawa wa Mbowe, hawatataka Bosi wao aachie ngazi, kwani itaonekana amemuogopa Lissu, na wao kuja kupata shida, kwa kulipia ule UCHAWA wao! Hivyo, wao ndi watakaomchukulia fomu na kumlipia. Mafahali wawili wataingia vitani!
Sidhani kama nyumba itabaki salama! Hapo, ndipo ninapo ihisi ATHARI!