Uchaguzi 2020 Kwa mambo haya 10, mimi kama Mtumishi wa Umma (mwalimu), John Pombe Magufuli sikupi kura yangu asilani

Uchaguzi 2020 Kwa mambo haya 10, mimi kama Mtumishi wa Umma (mwalimu), John Pombe Magufuli sikupi kura yangu asilani

Mkuu umeongea kwa hisia kali...pole sana.

Watanzania wamekusikia na watakuunga mkono wiki ijayo.
angalia na namba 6 Mkuu wangu...dah!! yan pesa ni yako lakin mtu anakupangia masharti magumu ya jinsi ya kuitumia; ikiwezekana hata ufe uiche..dah! aisee huu uonevu huu!!! apana kwa kweli...magufuli hapana jaman, bora hata angekuwa mwanaccm mwingine lakin siyo huyu mzee..no nooo nooooooo
 
hahahaaa ndio umejitahidiiii kuorodhesha...kwani kama hizo zote ni kero sasa si uache hiyo kazi uje huku kitaa uone kama hujarudi faster? Wewe ukiona kazi mbaya na haina maslahi kwako achana nayo. Hivi unajua kuna kina mama mtaani wanatembeza mboga na mtoto mgongoni na jua kali na faida kwa siku haifiki hata buku 3? Leo wewe nyau unalilia hela ya likizo kwani ulipoomba kazi kazi hukujua utatakiwa kurudi kwenu? Acha kazi kama mbaya.
Si dhani kama mbuzi anaweza kujua undani wa maisha ya kunguru.

Huna ufahamu wowote wa sheria na haki za watumishi idara ya elimu bali wewe ni mpiga debe usiyejua hata haki zako binafsi

Mtu mjinga hawezi kuwa msemaji wa taaluma za watu hasa elimu.

Baki kwenye siasa uchwara
 
*HAWA NDO CHADEMA WANAOTAKA KUCHUKUA NCHI*

Ni hivi, tangu wameingia madarakani, Chadema wamekuwa wakipokea ruzuku ya Shilingi Milioni 336,000,000/= kwa mwezi. Kwa mwaka (336,000,000/= x 12) = 4,032,000,000/=. Kwa miaka mikano (2015-2020) Chadema wamekusanya Jumla ya Shilingi *20,160,000,000/= (Bilioni Ishirini na Milioni Mia Moja na Sitini).*

Chadema walikuwa na jumla ya wabunge 70, kati ya hawa 34 wa kuchaguliwa, na 36 wa Viti Maalum. Kila mbunge wa kuchaguliwa alikuwa anachangishwa Shilingi Milioni Moja 520,000/= kwa mwezi na kila mbunge wa Viti Maalum alikuwa anachangishwa Shilingi Laki Tano (1,500,000/=) kwa mwezi.

Hivyo, idadi ya michango ya wabunge wa kuchaguliwa kwa mwezi ilikuwa (520,000/= x 34) = 17,680,000/=; na idadi ya michango ya wabunge wa Viti Maalum kwa mwezi ilikuwa (1,500,000/= x 36) = 54,000,000/=. Kwa ujumla wake, Chadema walikuwa wanakusanya kiasi cha shilingi 71,680,000/= kwa mwezi kutokana na michango ya wabunge. Kwa mwaka (71,680,000/= x 12 = 860,160,000/=. Kwa miaka mitano (2015-2020) Chadema wamekusanya Jumla ya *Shilingi 4,300,800,000/= (Bilioni Nne Mia Tatu Milioni na Laki Nane)*

Twende sawa hapa

Ruzuku 20,160,000,000/=
Michango ya wabunge 4, 300,800,000/=

Jumla 24,460,800,000/= *(Bilioni Ishirini na Nne Milioni Mia Nne na Sitini na Laki Nane)*

Licha yah hii;
· Chadema wanakusanya fedha kutoka kwenye ada za wanachama kila mwaka,
· Chadema wamefanya harambee ya nchi nzima mara kadhaa, nakumbuka ipo iliyofanyika Dar es Salaam (Serena hotel) na Arusha (hotel ya Mrema nimeisahau jina), na Mwanza kwa kuwataka Watanzania kuwachangia electronically. Hata mara moja hawajawahi kutoa ‘feedback’ kwa Watanzania hawa waliochanga. Kama wanabisha na ni wawazi kama wanavyojinasibu, watoe taarifa kwa kila tukio.

Hapo hatujaweka michango ya wanachama nchi nzima kila mwaka, Hivyo haya ni sehemu ya makusanyo yao ya miaka 5 tu kama Chama ambacho kimekuwa Chama kikuu cha upinzani nchini kwa miaka takribani 20, bado hii leo:

i. Hakina ofisi yao kama jengo, pamoja na kununua eneo miaka ya nyuma ili kuweka jengo la ghorofa 11kwa minajili ya kujenga ofisi yenye hadhi ya chama kikuu cha upinzani na kupangisha maeneo mengine. Ni kama Milioni 150 zilizotumika kununua eleo zilitupwa tu. Ofisi hii ya Chama inayotumika leo ilinunuliwa na Bob Makani. Kina Mbowe na Lissu wanaojinasibu kuwaletea Maendeleo Watanzania hawajawahi kufanya lolote pamoja na kujikusanyia mabilioni ya pesa kila mwaka.
ii. Makatibu wake wa wilaya wengi (kama sio wote) nchi nzima hawalipwi mishahara wala posho,
iii. Leo hii kampeni zinaendelea Chama hakina pesa za kuendesha kampeni, badala yake wanapitisha kofia kuwachangisha wananchi katika mikutano ya kampeni.

Hii pesa yote iko wapi? Kama imewekezwa, imewekezwa wapi? Mbona wabunge wao wanalalamika wakihoji haya wanaambiwa hakuna kuhoji?

Haya matumizi mabaya yote ya pesa yanafanyika wakati Tundu Lissu (eti mpenda haki huyu, na mtetezi dhidi ya ukandamizaji, na mwanademokrasia) akiwa ‘amebandikwa’ nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama, na Makamu Mwenyekiti wa Chama. Wanachama wanalalamikia haya yote, mwanasheria anateyakiwa kuwatetea, Bwana Tundu Lissu ametulia tulii kama vile hakuna kilichotokea yaani! Eti leo anaimba uhuru, haki na maendeleo wakati Chadema yake hakuna Uhuru, Chadema yake hakuna Haki, Chadema yake hakuna Maendeleo!, nay eye ni Kiongozi mwandamizi wa Chadema.

Ni huyuhuyu Tundu Lissu na Chadema wake wanataka Watanzania wawape ridhaa ya kusimamia utajiri wote wa nchi, waratibu matumizi ya matrilioni ya kodi zote zinazokusanywa nchini, wasimamie miradi yote ili eti walete ustawi kwa Watanzania.

Ni huyu huyu Tundu Lissu na Mbowe ambao ni viongozi wakuu wa Chadema miaka nenda rudi bado wanapanga makao makuu ya chama taifa kwenye nyumba ya mtu (mtaa wa Ufipa-Kinondoni), ndo wanasema eti watawasomesha bure Watanzania, eti watawatibu bure Watanzania wote.


Sasa ona hii, Lissu anajiita eti ni mwanasheria anayesimamia katiba na sharia. Hivi hiyo nafasi ya Mwanasheria wa Chama aliyonayo ndani ya Chadema iko kikatiba? Atoke huko atuonyeshe kwenye katiba kama kuna nafasi ya mwanasheria wa Chama kikatiba. Huyu huyu ameshindwa kusimamia haki ndani ya Chama, ameshindwa kutetea uhuru wa wanaokandamizwa ndani ya chama kiasi cha anayehoji tu anafukuzwa uanachama, ameshindwa kusimamia na kuheshimu katiba ya chama; eti leo hii anataka kusimamia haya akiwa Rais wa Tanzania?

Wahenga walisema “sumu haijaribiwi kwa kuionja”, Chadema hii ya Lissu na Mbowe ni sumu kwa Watanzania.
Na upande wa ccm hesabu yao imekaa vipi?
 
Na mimi nimekumbuka watumishi walivyokuwa wamegeuza ofisi za umma kama mali yao, kwa Magu thubutu tena uone kazi! Halipo tena Magu mitano tena tunampa

2. Walimu waliokuwa wanafundisha kijijini walipofuata mishahara walioamua kulewa takribani wiki mbili bila kurud shuleni wakisingizia foleni mishahara kuchelewa wanafunzi wetu walibaki wakifundishana wenyewe hilo kwa Magu limekomeshwa,wananchi watoto wetu hamzururi ovyo lazima tunamchagua

3. Walimu walitumia michango ya shule ,kuwaambia wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza kwenda na limu,majembe, fyekeo nk. Kisha vyote waliviuza kwa wafanyabiashara baadaye kwa manufaa yao ,leo hayo mambo Magu kayamaliza lazima mchukie lakini kwetu wananchi tunamchagua tena

4. Watumishi walitumia lugha za matusi tulipotaka watuhudumie leo watumishi wanatuheshimu kwa sababu Magu hataki watumishi wasiowajibika kwa wananchi lazima mchukie lakini kwetu wananchi tunamchagua katujali sana

5. Nakumbuka mawaziri ,makatibu wakuu ,wakurugenzi na wakuu wa idara na walivyoshirikiana kutupiga kwenye miradi mbalimbali na kuanzisha semina zilizofanyikia kwenye majengo yao morogoro,Arusha,Mwanza leo hayo hayapo kweli lazima mchachamae lakini tunaowajua leo tunafaidi wote kodi zetu watanzania usifikiri hawaoni watamoatia kura za kishindo magufuri hadi mchanganyikiwe!!!

Ebu ongezea mengine kama unakumbuka vituko vya watumishi
Madai yako mengi yana msingi na umedai kwa sasa yameshughulikiwa hiyo ni sawa kabisa.

Watumishi pia wana madai yao halali ambayo mara nyingi Mh Rais amekuwa anayakwepa na yeye ndiyo yanamuhusu.

Kwa hiyo lazima utambue wajibu mzuri wanaoufanya watumishi lazima uendane na haki zao za msingi pia.
 
CCM mje huku mjibu hizi tuhuma za huyu mwalimu kama ni za kweli au ni za uongo. Fanyeni haraka kabla walimu hawajala vichwa vyenu
Tuhama NI za kweli ilanmtuchague Tena tukazitatue [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Si dhani kama mbuzi anaweza kujua undani wa maisha ya kunguru.

Huna ufahamu wowote wa sheria na haki za watumishi idara ya elimu bali wewe ni mpiga debe usiyejua hata haki zako binafsi

Mtu mjinga hawezi kuwa msemaji wa taaluma za watu hasa elimu.

Baki kwenye siasa uchwara
Hahahaaa acha kazi kama.umepanick..haki haki hivi unajua wapo wasomi wakubwa tu nje wanatamani hata huo mshahara wako unaoita mdogo hata wa mwezi mmoja?? Kama umechoka acha ww sio special upewe kila kitu ww nani
 
Hahahaaa acha kazi kama.umepanick..haki haki hivi unajua wapo wasomi wakubwa tu nje wanatamani hata huo mshahara wako unaoita mdogo hata wa mwezi mmoja?? Kama umechoka acha ww sio special upewe kila kitu ww nani
Kutofahamu haki na stahiki za wenye taaluma yao ya elimu ndiyo ujinga wako.

Maana huelewi yana umuhimu gani ktk taaluma yao.

Haki inapodhurumiwa ni sharti la mwenyekudhurumu achukuliwe hatua ya kulipa alichodhulumu kabla ya aliye dhulumiwa kuondoka.

Vivyo hivyo watumishi hawawezi kuacha kazi mpaka stahiki zao zitakapo lipwa.

Wengi walijitoa nafasi hizo (kuacha kazi) pale haki zao za fao la kujitoa lilipo kuwepo.

Serikali ilivyo kopa mifuko ya watumishi kujenga flyovers (fedha za watumishi) ndio ukawa mwanzo wa matatizo haya ya watumishi kusitisha kuacha kazi.

Kumwambia mtumishi aache kazi akiacha madai yake kwa serikali bila kulipwa ni kumwambia aache fedha zake ziliwe na serikali.

Huu ni ujinga wako binafsi wewe usiyejielewa.

Kabla hujasema hivyo wawalipe stahiki zao kama hawajaacha hizo kazi na kuwekeza kwenye maeneo mengine ya kiuchumi.
 
Siyo mwalimu huyo dalali tu, annual increment kila mwaka imekuwa ikiingia. Madaraja walimu tunaostahili tumepandishwa wale waliostahili kupandishwa halafu hawakupandishwa pasipo sababu walipolalamika maafisa utumishi waliwajibishwa.

Acha kudandia taaluma za watu mimi ni mwalimu niko pamoja na Magufuli.Jikite kwenye siasa zako siyo kuwasemea waalimu.
Acha ujinga wewe binti sayuni, annual increments zimeingia lini? Au unadhani huyo jamaa lofa,anachoongea ni Cha kweli,hakuna alipodanganya,wewe endelea kupigania buku Saba zako,anko wangu ni ticha Kila siku analalamika hayo hayo,halafu unakuja kumtetea hapa.
 
Pamoja na kujipitisha mashuleni kutuomba kura za huruma, mie nimeamua kura yangu sitampa mgombea wa ccm kama nilivyofanya 2015 hii ni kutokana na mambo 10 niliyoyaona kipindi hiki cha miaka mitano

1. Makato ya bodi ya mikopo toka 8% hadi 15% bila sababu maalum tena kwa ubabe.

2. kutunyima nyongeza ya mshahara (annual increment) kwa miaka takribani mitano wakati ni haki ya msingi ya mtumishi.

3. Kutopandishwa daraja mwaka wa 6 huu unakwenda wa 7. Mie nimeajiriwa mwaka 2014 mwezi Aprili, mpaka leo Oktoba 2020 takribani miaka sita imepita huku nikilipwa mshahara wa TGTS D ambao ndio nilioanza nao mwaka 2014 na hata anayeajiriwa leo naye atalipwa hivyohivyo. Halafu wasanii wa bongo fleva wanatanua na kuchezea hela ya serikali kwenye kampeni zako.

4. Kutolipa hela ya likizo kwa wakati. Mfano mie likizo ya malipo nimeenda juni 2017 na juni 2019 JPM ukiwa madarakini, likizo zote nimesafiri toka Lindi hadi Mwanza bila kulipwa hata senti, mwaka huu ndio nimepewa hela ya likizo ya mwaka 2017 tena nusu tu.

5. Hela ya usimamizi wa mitihani ya Taifa kidato cha 4, 2 na 6 kutolipwa yote ya mwaka 2018 na 2019 huku siku za usimamizi (za malipo) kwa wataalamu wa maabala zikishushwa kuanzia mwaka huu toka siku 6 hadi moja.

6. Sheria mpya ya wastaafu ambayo umejifanya Kuibatilisha hadi 2022 ni geresha tu kupisha uchaguzi mkuu huu ufanyike na baada ya hapo kikokotoo kipya kianze kazi. malipo ya mkupuo kwa wastaafu (Lumpsum) kwa Kikokotoo kipya kinataka mstaafu apewe 25% ya mafao yake yote, na 75% zinazobaki apewe kidogokidogo hadi kufa kwake mfano milioni 100 upewe milioni 25 halafu milioni 75 nilipwe kidogokidogo. Mie kama mtumishi hii kwangu haiingii akilini na ili isiniumize ni kukunyima tu kura yangu

7. Ulituahidi Laptop kila mwalimu 2015 lakini muda wako wa awamu ya kwanza unaenda mwishoni bila dalili yoyote ya kupewa hiyo Laptop.

8. Uzalilishaji unaofanywa na wateule wako kama Ma-RC na ma-DC mbele ya wanafunzi wetu na wewe umekuwa kimya. Mfano kutulazimisha kulala kwenye mwenge tena kwa kuitwa majina kama watoto.

9. Ninachangia bima ya afya (3%) kila mwezi halafu dawa za muhimu zimeondolewa na unapoenda hospitali tunalazimika kujinunulia kwa hela yetu.

10. Sababu za Kutoa kufundisha walimu wa masomo ya sanaa wa sekondari kwenda shule za msingi ni za ajabu sana
Wape hayo madini walimu wengine kama 50!
Nimewapa madini askari siyo chini ya 80 kwa nyakati tofauti, hakuna atakayepigia kura hao watu
 
hahahaaa ndio umejitahidiiii kuorodhesha...kwani kama hizo zote ni kero sasa si uache hiyo kazi uje huku kitaa uone kama hujarudi faster? Wewe ukiona kazi mbaya na haina maslahi kwako achana nayo. Hivi unajua kuna kina mama mtaani wanatembeza mboga na mtoto mgongoni na jua kali na faida kwa siku haifiki hata buku 3? Leo wewe nyau unalilia hela ya likizo kwani ulipoomba kazi kazi hukujua utatakiwa kurudi kwenu? Acha kazi kama mbaya.
Anachokizungumzia Kiko kwenye mkataba wake wa kazi,acha dharau,Kama hujaajiriwa usimuonee gere, mwandika bandiko
 
Siyo mwalimu huyo dalali tu, annual increment kila mwaka imekuwa ikiingia. Madaraja walimu tunaostahili tumepandishwa wale waliostahili kupandishwa halafu hawakupandishwa pasipo sababu walipolalamika maafisa utumishi waliwajibishwa.

Acha kudandia taaluma za watu mimi ni mwalimu niko pamoja na Magufuli.Jikite kwenye siasa zako siyo kuwasemea waalimu.
Acha uchawi mdogo wangu.
 
Siyo mwalimu huyo dalali tu, annual increment kila mwaka imekuwa ikiingia. Madaraja walimu tunaostahili tumepandishwa wale waliostahili kupandishwa halafu hawakupandishwa pasipo sababu walipolalamika maafisa utumishi waliwajibishwa.

Acha kudandia taaluma za watu mimi ni mwalimu niko pamoja na Magufuli.Jikite kwenye siasa zako siyo kuwasemea waalimu.Wewe pia umedanganya,kwenye hoja zote mtoa post yupo sahihi
 
Siyo mwalimu huyo dalali tu, annual increment kila mwaka imekuwa ikiingia. Madaraja walimu tunaostahili tumepandishwa wale waliostahili kupandishwa halafu hawakupandishwa pasipo sababu walipolalamika maafisa utumishi waliwajibishwa.

Acha kudandia taaluma za watu mimi ni mwalimu niko pamoja na Magufuli.Jikite kwenye siasa zako siyo kuwasemea waalimu.
Acha uongo hiyo annual increment umepewa wewe peke yako au? Na mimi pia nmeajiriwa 2014 sijapanda daraja,we ndo dalali hiyo aliyeanzisha mada ndo mwalimu na yote alosema ni kweli,tokeni hapa na kiccm chenu wanyanyasaji wakubwa nyie na mkae mkijua Mungu ni wetu site IPO siku mtajibu kwa dhuluma hizi
 
Back
Top Bottom