VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kila mmoja sasa anajua kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa Makamu wa Rais wa Mwendazake Hayati Dr. John Pombe Magufuli. Tunajua pia kuwa Rais Samia alichaguliwa kwa kura zilezile za Mwendazake mwaka 2015 na 2020. Alikuwa msaidizi nambari moja wa Mwendazake. Lakini, kikatiba Mwendazake ndiye aliyekuwa akisema na kutenda yote ya maamuzi ya mwisho. Mama sasa ndiye muamuzi wa mwisho.
Pamoja na kusema tena na tena kuwa yeye na Mwendazake ni kitu kimoja, Rais Samia anajipambanua kimaneno na kimatendo kuwa yu tofauti na Mwendazake. Anasema na kutenda tofauti na Mwendazake, angalau kwa muda huu mfupi wa Urais wake. Yeye si muumini wa 'matumizi ya nguvu' kwenye mambo ambayo hata hayakuhitaji matumizi ya nguvu. Yeye ni muumini wa hoja kabla ya uamuzi wa haja.
Yeye havumilii 'ulevi wa madaraka' wa wateule wake ambao wakati ule walilewa na kuwa miungu-watu katika sehemu zao za kiutawala. Anajipamanua kama mpenda demokrasia na maridhiano badala ya kutumia 'amri na nguvu' tu wakati wote wa kusema na kutenda. Hadi hapo, kuna tofauti kati yake na Mwendazake. Kujifananisha na kutuaminisha kuwa wao ni kitu kimoja kile kile ni mambo ya siasa tu.
Sasa, kubadili ni kurekebisha. Kurekebisha ni kutokukubaliana na kilichokuwepo. Kutokukubaliana halafu kutokuwa na uwezo wa kubadili, kupinga au kushauri ipasavyo ni maumivu makubwa. Amini nawaaambia, kwa maneno na matendo yake, Rais Samia alikuwa njiapanda wakati wa Mwendazake. Alikuwa akiishi kwenye maumivu yasiyomithilika. Sasa ana amani na utulivu wa moyo. Anasonga mbele akitekeleza anayoyaamini na aliyokuwa akiyatamani yafanyike wakati ule.
Mama Samia, tupo pamoja kwenye hoja!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)