Kwa manufaa ya Taifa na Usalama wao, Baraza la Maaskofu TEC na The Free Pentecostal Church of Tanzania, FPCT wahame Kurasini

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
TEC na FPCT Ni vituo vya kidini ya kikristu vilivyoko eneo la Kurasini, Dar es Salaam. Kwasasa vituo hivi vimezunguukwa na shughuli mbalimbali za kiuchumi wa bandari kuu ya Tanzania. Viko katikati ya matenki ya mafuta na makontena.

Uwepo wa taasisi hizi katikati ya shughuli za kiuchumi kunaipunja bandari, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa malori yanayohitaji kuchukua na kupeleka bidhaa bandarini na kusababisha kuegesha njiani na kandokando mwa barabara.

Ukiviondoa vituo hivi bandari itapata nafasi kubwa ya kuweka mizigo na malori kuegesha kwa urahisi.

Swali Ni kwanini taasisi hizi hazikuondoshwa wakati wengine wanaondoshwa Kurasini kupisha upanuzi wa bandari?

Je, taasisi hizi hazioni kuwa ziko kwenye eneo la kimkakati kitaifa?

Je taasisi hizi hazioni kuwa ziko kwenye eneo hatarishi kwao (ajali za Moto, vurugu na kelele)
 
Kuna chuo na kambi ya jeshi vinatazamana na hayo matenki ya mafuta. Kuna eneo la watu wanaishi kubwa sana linatazamana na hayo matenki ya mafuta. Kwanini umeona hizo taasisi za kidini tu ndio ziko hatarini?
 
Huyo bwana nafikiri anataka kwenda kupiga kiberiti pale ila anawaonea huruma hao wa taasisi za dini au ana jingine lake jambo.
 
Kuna chuo na kambi ya jeshi vinatazamana na hayo matenki ya mafuta. Kuna eneo la watu wanaishi kubwa sana linatazamana na hayo matenki ya mafuta. Kwanini umeona hizo taasisi za kidini tu ndio ziko hatarini?
Hizi ziko ufukweni kabisa katikati ya pilikapilika, hata reli pia inapita hapo. Pale FPCT maroli yanapita kwenye geti la taasisi. Afadhali jeshi kuwepo kwa usalama na Ni chombo Cha Serikali kuliko taasisi za madhehebu ya dini.
 
Duh kwahio issue sio hatari iliopo bali madhehebu ya dini? Nauliza hivyo kwasababu nimekujulisha pia kuna makazi yanatazamana na hayo matenki tena makazi mengi si rasmi. Hao vipi hawako hatarini?
 
Duh kwahio issue sio hatari iliopo bali madhehebu ya dini? Nauliza hivyo kwasababu nimekujulisha pia kuna makazi yanatazamana na hayo matenki tena makazi mengi si rasmi. Hao vipi hawako hatarini?
Hayo makazi yanaweza kuwa yaneachwa kwasababu gani wakati makazi yote yameshabomolewa? Hayo makazi yalyoachwa inawezekana yameachwa ili ku justify kubaki kwa taasisi hizi nilizozisema
 
Kwa uandishi wako unaonesha wewe ni dalali, unayataka maeneo hayo uwauzie wachukuzi.
 
Jibu post no 2 hapo juu, kwanini bandari isihame hapo.
Kama maelfu wamehamishwa kwanini wachache wabaki. Yaani kama kuna makazi ya watu wa kawaida yamebaki basi yamebakishwa ili kupisha aibu na lawama za kubakisha TEC na FPCT zenyewe tu katikati ya shughuli za kiuchumi za taifa. Malori yanapata tabu ya kuegesha huku eneo la kimkakati likikaliwa na watu binafsi
 
Kwa uandishi wako unaonesha wewe ni dalali, unayataka maeneo hayo uwauzie wachukuzi.
Hapana mimi napenda yale malori yanayoegeshwa barabarani, kandokando ya barabara za waenda kwa mikuu na pale kwenye chuo cha uhasibu yaondoke maana ni hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…