Kwa mapenzi ya leo!!Mhnnn!!!

Kweli hii ipo sana, mwanaume kipato kikipungua tu, mapenzi hakuna...Japo wapo wachache wenye mapenzi ya kweli.

Inategemea mapenzi enu yalianzaje? kama ulimtongoza kwa kujifanya baaaab kubwa, halafu mwanzoni alikua anakukataa ukalazimisha kwa kila hali matokeo yake akakupendea vijisenti vyako. Vikiisha unategemea nini? Umependa usipopendwa
 


Tatizo la wanaume wa sasa akiona humuombi hela, wala kumlilia shida kuna mawili my dear:
1. Ataanza kudhani unampenda sana ndio maana huombi hela kwake ataanza kukunyanyasa akidhani kwake hupindui
2. Asipofanya hilo hapo juu ataanza kukugeuzia kibao kukuchuna/kukuomba hela wewe akidhani unazo sana ndio maana humuombi kumbe unatumia tu ustaarabu una kijipato kina kidhi mahitaji muhimu kwa nini uanze kumkera mwenzio

Hawana jema hawa
 
Kweli Kakiiza umenena vema..............I just ask myself mbona wanaume wao huwa hawajali kama huyu mwanamke ana uwezo au la? Au kwa kuwa wao ndio wanaooa?
Wanaume wanaangalia sura na maumbo!
 

Au atasema kuna mtu anakuhonga!
 
naelewa maty but asume kila kitu kiko genuine and constant................wewe kama wewe unampenda mwanaume wako ambaye kwa bahati mbaya leo hana uwezo (pengine zamani alikuwa nazo) utathubutu kumwacha kisa mwanaume suruali? (Hapa naye awe genuine si mchunaji au kula kulala)
 
KK huyo mwanamke inategemea wakati unaanzanae uhusiano ilikuwaje,kama ulimpata kwa mbwembwe na tambo nyingi basi yafaa ukubaliane na hali halisi kuliko kuanza kulaumu na kuwalaumu wanawake,nitashangaa tu kusikia kuwa ulimpata katika mazingira ya kawaida ya kutokuwa na vitu kama gari na matanuzi ya hapa na pale na leo hii ndio anakubadilikia,hapo ipo haja ya wewe kulalamika na nakuunga mkono katika hilo.
 
Imekaaje hii inamaana cku wakiamka vizuri ni wote wanaamka vizuri.cku vibaya wote.

Sio kwamba tumeamka vizuri bali wadada wa jf ni watu wenye hekima na adabu zao hawaangalii mapenzi ni pesa, bali mapenzi ya kweli. Ni hao mnaokutana nao uswazi/mitaani ndio wanaowakaba makoo
 

Hapana my dia tena ikimtokea hivi ndio nitamuonyesha mapenzi ambayo hata hajawahi hisi yapo, ili kumtia moyo kwani ni mapito tu ambayo yanaweza mpata yeyote.
 
Sio kwamba tumeamka vizuri bali wadada wa jf ni watu wenye hekima na adabu zao hawaangalii mapenzi ni pesa, bali mapenzi ya kweli. Ni hao mnaokutana nao uswazi/mitaani ndio wanaowakaba makoo
maty taratibu bana. Nijuavyo mie wanawake wa udhunguni ni wepesi sana kunyanyasa wakizipata kulinganisha na wa uswazi (Sijui kama nazungumzia zamani maana nami nimezeeka). Mwanamke wa udhunguni yeye akikuomba pesa ya saluni ukampa pesa mbuzi hakawii kukurushia usoni na siku utakapodeclare kuwa huna ndo atakutolea uvivu mwanaume suruali wa kazi gani. Na isitoshe siku akipata pesa zinakuwa zake yaani zake zake, zako zake.

But wale wa Uswazi, akiomba ukampa hata kidogo utapata hewala bwana Mungu akuzidishie; na wengine hicho hicho kidogo ulichompa atakibana ili akununulie nawe japo handkerchief kama ishara ya kukushukuru. ... Sina uhakiak kama nao wanawezasema mwanaume suruali (hapa nazungumzia wale walo kimapenzi zaidi na si kibiashara)
 
Umeona eeeeee we acha tu! au sa nyingine unaambiwa unaringa/unajisikia kaazi kweli kweli
Tuna kazi..maana kila tunachofanya ni tatizo.Ukiwakataa unaringa..ukiwakubali mrahisi!Ukitaka vijisenti vyao unawachuna..usipotaka unajiona!Ukitulia nao unawaganda..ukiwaacha hujatulia!Tabu tupu!
 
Ikitokea hivyo ujue hakupendwa mtu bali kitu.
 

Hahahaha MJ hamna bwana unajua hawa wa udhunguni ndio wamesababisha marioooo kwa sababu ya kuwahonga? huku uswazi mwanamke wa kukuhonga utamtoa wapi maisha yenyewe haya. Ila mi nadhani inategemea na huyo mwanamke mlipatana vipi na je anakupenda? unajua wanaume wenye hela huwa wanapenda wanawake walio juu na maisha yao ya juu sasa mwanamke kama huyo utamweleza nini?
 
Ah mie nimekupa tu na scenerio nyingine uone. Unajua most of these tabia mbaya huwa wanazisababisha wao na bahati mbaya sie hatuchambua tunafollow tu sasa madhara yakitokea twabebeshwa lawama sie...........anakupenda mwanzo kwa kukupa kila kitu wengine ukitoka nao bar ukiomba kulipa bill hataki, ukimnunulia zawadi hataki sasa anasahau kuwa anakuzoesha na ujumbe unaoupata wewe ni kuwa mwenzangu hapendi nimnunulie zawadi au nilipie bill............siku wakichacha na wewe ukaendelea kuishi ulivyozoeshwa ni kesi. Wnawake tuna kazi kweli kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…