PostGE2025 Kwa mara nyingine Polisi wakanusha matukio ya TFF, wasema hawajafanya uhalifu

PostGE2025 Kwa mara nyingine Polisi wakanusha matukio ya TFF, wasema hawajafanya uhalifu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Wakuu,

Naona Jeshi la Polisi linatumia nguvu sana kukanusha uwepo wa kundi hili la Tanzania Freedom Fighters badala ya kutuoneyesha wamefanya nini kuwakamata/kuwadhibiti na kurejesha 'amani' nchini.

Ni kama vile wanajaribu kuficha kuliko kudili na tatizo! Baada ya ile clip ya kwanza kusema wameua kiongozi wa CCM tulitarajia wawe wamewakamata wote, au walau kuna washukiwa, lakini mpaka leo holaaa! Nasema hola sababu wangeshika hata mtu mmoja anayejinasabisha na kundi hilo wangetoa press hadi tuzikalili kwa mafanikio hayo!

Wanachosema tu ni kuwa "Tunawafuatilia kwa karibu!" Mnawafuatilia kwa karibu au hamna moja wala mbili wa mahala jamaa walipo? Mnawafuatilia kwa karibu huku mnasema kuna watu wameanza kushawishika kujiunga na kikundi chao? Mnasubiri mpaka liwe kundi kubwa ambalo la kuwashijda 'nguvu' ndo mlete majibu?

Anyhu kwa upande mwingine ni rahisi tu kumaliza haya yote, wananchi wana uchungu na kwakuwa wameona hakuna aliyetayari kuwafuta machozi na kuponya vidonda vyao, kuanzia Rais mpaka watendaji wake, wameamua kujipoza wenyewe!

Waliohusika na mauji ya Oktoba 29 wasipochukuliwa hatua, na utekaji unaoendelea ukakoma, huenda hali ikawa mbaya zaidi. Uwezo wa kumaliza haya yote upo mikononi mwenu... au nakosea guys Dr. Mwigulu Nchemba?🌚

Pia soma PostGE2025 - Tanzania: Kikundi cha uasi kimeanzishwa tayari? Wanajiita Tanzania Freedom Fighters (TFF). Ni hatari sana

======

TAARIFA KWA UMMA​

Jeshi la Polisi linapenda kujulisha kuwa, linaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi kama yalivyoainishwa na Sheria za nchi. Utekelezaji huo unakwenda sambamba na kushirikiana na wananchi katika kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu jambo ambalo limepelekea nchi yetu kuendelea kuwa shwari.

Pamoja na ushwari huo yapo matukio machache ambayo yametokea na yameendelea kufanyiwa kazi na baadhi ya watuhumiwa wameendelea kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kufikishwa mahakamani kama ambavyo Makamanda wa Polisi wa Mikoa wamekuwa wakitoa taarifa kila mara kupitia Vyombo vya Habari.

Aidha, kupitia mitandao ya kijamii, kumejitokeza baadhi ya watu kuendeleza tabia za kuhamasisha wananchi wajiingize kwenye vitendo vya kihalifu na baadhi wameshawishika na kujiingiza kwenye uhalifu wa kimtandao na baadhi wameshakamatwa na wengine wanaendelea kutafutwa.

Pia soma PostGE2025 - Vitisho vinavyotolewa na kundi linalojiita 'Tanzania Freedom Fighters (TFF) visichukuliwe poa. Hofu inatanda, mimi nina ushuhuda!

Baadhi ya watu hao wanaoshawishi uhalifu huo ni pamoja na anayejitambulisha au wanaojitambulisha kwa jina la TFF na kutoa taarifa mbalimbali kuwa, wanafanya mazoezi porini na kwamba wameshafanya matukio kadhaa ya kijinai. Jeshi la Polisi linakanusha taarifa wanazosambaza kuwa kikundi chao kimetenda uhalifu huu na ule kwani si za kweli.

Jeshi la Polisi linapenda kuwahakikishia wananchi kuwa, linawafuatilia kwa karibu sana watu hao pamoja na matamshi na jumbe zao wanazotengeneza na kusambaza kwa lengo la kuleta taharuki kwa wananchi.

Ufuatiliaji unafanyika usiku na mchana hivyo wananchi muondoe hofu na endeleeni na shughuli zenu za kiuchumi na kijamii kama kawaida.

Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuwapuuza watu hao na wengineo pamoja na taarifa na jumbe zao kwani hawapo ndani ya mipaka ya nchi na hata wanacho hamasisha hawatashiriki na hawatakuwa na uwezo wala mwanya wa kuwaruhusu kushiriki.

Wananchi watambue lengo la watu hao ni kutaka kutuchonganisha, kutujengea chuki ili tuhamasike tujiingize kwenye uhalifu na vitendo vya vurugu.

Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua yeyote yule atakaye endelea kujihusisha na vitendo kama hivyo au kujiingiza katika uhalifu wa aina yeyote ile kwani ni kinyume na sheria.

Imetolewa na;
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania

IMG_20260222_155034_369.jpg
Screenshot_20260222_155203_Instagram.jpg
 
Kumekucha ..
Na wale wa kusambaza habari za yule mpelelezi habari za uongo?

Kanusheni hii habari mbaya sana. Inatweza utu wa kamanda na kuhamasisha ujasiri watu kuwateka makamanda wengine.

Ajitokeze mwamba aseme yupo salama hajavuliwa ubingwa.
Ana familia yule. Si vema tuhuma hizi zikiendelea kusambaa hivi bila kanusho.

Mimi binafsi nashauri kama kamanda ana kosa angefikishwa mahakamani ajibu tuhuma za uhalifu.
Siyo kufanyiwa mambo ya kinyama. Kama ninavyo omba Polepole afikishwe mahakamani endapo ameonekana ana kosa la kujibu, sibagui wadhifa wa mtu wa kumtetea haki zake.
 
Kumekucha ..
Na wale wa kusambaza habari za yule mpelelezi habari za uongo?

Kanusheni hii habari mbaya sana. Inatweza utu wa kamanda na kuhamasisha ujasiri watu kuwateka makamanda wengine.

Ajitokeze mwamba aseme yupo salama hajavuliwa ubingwa.
Ana familia yule. Si vema tuhuma hizi zikiendelea kisambaa hivi bila kanusho.

Mimi binafsi nashauri Kama kamanda ana kosa angefikishwa mahakamani ajibu tuhuma za uhalifu.
Siyo kufanyiwa mambo ya kinyama. Kama ninavyo omba Polepole afikishwe mahakamani endapo ameonekana ana kosa la kujibu, sibagui wadhifa wa mtu wa kumtetea haki zake.
Nani wa kumfikisha huko kwenye vyombo vya sheria?..
. Unapoona ile kesi ya Lisu unajifunza nini?.?
 
Wanachosema tu ni kuwa "Tunawafuatilia kwa karibu!" Mnawafuatilia kwa karibu au hamna moja wala mbili wa mahala jamaa walipo? Mnawafuatilia kwa karibu huku mnasema kuna watu wameanza kushawishika kujiunga na kikundi chao? Mnasubiri mpaka liwe kundi kubwa ambalo la kuwashijda 'nguvu' ndo mlete majibu?
Utanisamehe kama nakosea, lakini ni kama unalalamika sana kwa kuwa polisi wameshindwa kufanya kazi yao sawasawa kwa kuwashughulikia hao wanaodhaniwa kuwa mashujaa waliojitoa kutetea taifa hili..

Unazo taarifa za kuwasaidia polisi ili wawashughulikie haraka hao wazalendo?
 
Hivi yule mwanamziki wetu anaekimbilia studio msibani anaitwa nani vilee
 
Hizi habari za Mafwele kupigwa paipu ni kweli au uzushi?
 
Utanisamehe kama nakosea, lakini ni kama unalalamika sana kwa kuwa polisi wameshindwa kufanya kazi yao sawasawa kwa kuwashughulikia hao wanaodhaniwa kuwa mashujaa waliojitoa kutetea taifa hili..

Unazo taarifa za kuwasaidia polisi ili wawashughulikie haraka hao wazalendo?
Sasa wao SI wana intelejensia Kali hd ya kuhisi tu kwamba mtu anataka kufanya uhalifu? Hawa Tff wanawashindwaje hd watake msaada?.....au Inafanya kazi kwa viongozi na wanachama wa Chadema tu😁😁😁😁
 
Sasa wao SI wana intelejensia Kali hd ya kuhisi tu kwamba mtu anataka kufanya uhalifu? Hawa Tff wanawashindwaje hd watake msaada?.....au Inafanya kazi kwa viongozi na wanachama wa Chadema tu😁😁😁😁
Jambo la kwanza, ni lini hawa polisi wakafanya kazi kwa kufuata misingi ya kisheria kama tangazo lao lote linavyodai toka mwanzo hadi mwisho!

Ni kama wanaandika kwa mtu ambaye hajawahi kuishi Tanzania, na ndiyo mara ya kwanza kusikia chochote toka polisi.
Ulaghai huu unamsaidia nani?
 
Wanausalama na serikali wakifanya matukio ya uhalifu, hali ni shwari.

Ila wananchi wakipinga ushetani wao, wanaonekana ni wahalifu
Ulikuwa wapi miaka yote hii mkuu 'Mbaga Jr'?

Sasa naona matumaini makubwa juu ya taifa letu hili, kama akina 'Crimea, Etwege' na wengine wengi nao sasa wanaona michipuko mipya kila sehemu ya taifa hili.
 
Barua yao inachefua.

Polisi wa Tanzania na sheria wapi na wapi?

Sisi wananchi Wala hatuna shida na hao wanaoitwa TFF. Kama kweli wapo na wanafanya hayo matukio kwa askari polisi na sisiem sisi Wala hatulalamiki Wala kusikitika.

Kwa waliyofanya polisi wa nchi hii lolote liwakute tu.

Hivi mfano yule uvisisiem wa Kagera aliyesema mbele ya Samia kipindi cha kampeni kuwa wananchi wanaotaka kuandamana wapigwe shaba,yule likimkuta jambo baya mtu unaanzaje kumsikitikia?

Au wasira 😁😁...unaanzaje kusikitika kwa zile kauli zake?

Sisiem na polisi mtajuana wenyewe!!
 
Ulikuwa wapi miaka yote hii mkuu 'Mbaga Jr'?

Sasa naona matumaini makubwa juu ya taifa letu hili, kama akina 'Crimea, Etwege' na wengine wengi nao sasa wanaona michipuko mipya kila sehemu ya taifa hili.
Nilikuwa wapi kwenye ishu gani mkuu?
 
Back
Top Bottom