Kwa Mara ya kwanza, ambao hawakuwahi kuelewa maana ya udikteta, wanapata maana halisi

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Wakati wa utawala wa Jakaya Kikwete, kuna wakati baadhi ya watu walimwita ni dikteta, yeye akajibu kwa kuwauliza kama hao wanaosema kuwa yeye ni dikteta, wanaelewa maana ya udikteta. Akawauliza mmewahi kushuhudia udikteta nini?

Wakati wa utawala wa Hayati Magufuli, Tundu Lisu alimwita Magufuli kuwa ni dikteta uchwara, akimaanisha alionesha viashiria vya udikteta lakini hakuwa amefikia udikteta kamili. Lakini kwenye awamu hii, watanzania wanashuhudia udikteta kamili. Tujaribu kulinganisha udikteta uchwara na udikteta kamili.

1. Wakati wa utawala wa Hayati Magufuli, kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, mwaka 2019, wagombea wa CHADEMA, chama kikuu cha upinzani, karibia wote walienguliwa. Lakini wakati wa utawala wa Samia, msimamizi mkuu wa uchaguzi alimweka mkwe wake, wagombea wa CHADEMA karibia wote walienguliwa, wachache walioachwa, baadhi waliuawa, na hata wachache walioshioachwa, wakashinda uchaguzi, hawakutangazwa.

2. Kwa upande wa mgombea wa kiti cha Urais, Hayati Magufuli alimwacha hasimu wake Tundu Lisu kuwa mgombea, aliiacha CHADEMA ifante siasa na kampeni, japo kuna maeneo ilithibitika kuwa kura za Lisu ziliibiwa. Lakini kwenye utawala wa Samia, siyo tu Lisu amenyimwa haki ya kugombea, bali amefungwa na kutengenezewa kesi, kwa kupitia mahakama bandia, na Tume huru bandia ya Uchaguzi, CHADEMA imezuiwa kushiriki uchaguzi na kufanya shughuli za siasa.

3. Hayati Magufuli alipiga marufuku shughuli za siasa za vyama vya siasa baada ya uchaguzi na siyo wakati wa uchaguzi, lakini wakati utawala wa Samia, CHADEMA imezuiwa kufanya shughuli za siasa kipindi cha uchaguzi ili asiwe na mpinzani.

4. Wakati wa utawala wa Hayati Magufuli, muda usio wa uchaguzi, baadhi ya wakosoaji walitekwa kwa siri, na hawakuonekana mpaka leo. Lakini wakati wa Samia, viongozi wa CHADEMA na baadhi ya wakosoaji wamekuwa wakitekwa hadharani, wakati mwingine mbele ya vyombo vya ulinzi na usalama, bila hofu yoyote na watawala indirectly wakiunga mkono vitendo hivyo kwa kutoa kauli tata, kama vile 'kifo ni kifo tu', hakuna anayetekwa hizo ni drama tu; wanaotekwa na kupotezwa wametoroka madeni au wameenda kwa wapenzi wao. Ni watu wachache sana waliotekwa wakati wa utawala wa Hayati Magufuli, lakini chini ya Samia makumi ya watu wametekwa na ama kuuawa au kupotezwa.

5. Wakati wa Hayati Magufuli, hakuna mwanafamilia ywake yeyote aliyepewa jukumu maalum la kusimamia uovu kwa maslahi ya ndugu yake, lakini wakati wa Samia, Mchengerwa, mkwe wa Rais andiye aliyekuwa msimamizi wa TAMISEMI, ambayo ndiyo iliyosiamua na kuwezesha uovu wote wakati wa uchaguzi wa 2024. Na bado ana jukumu muhimu la uchaguzi bandia mwaka huu kwani wasimamuzi wote wa huo uchaguzi wapo chini yake.

Watanzania mlimwita Kikwete dikteta, Magufuli dikteta uchwara, leo ndiyo mnaoneshwa maana halisi ya udikteta.
 
Tatizo la dikteta wa kizimkazi kwanza ni muoga sana pili mjinga!
So wahuni wanamtumia kwa maslahi yao na yeye kwakuwa ni mjinga haelewi...anabung'aa tu mimacho!.
 
Ninyi mashetani, kila jambo linalohusu haki, kwenu inakuwa pumba maana kwenu jambo la maana ni udhulumaji wa haki za watu, na kila aina ya uovu mwingine.
 
Amemezwa na majitu maovu, yamemweka kati, wlyanamchezesha kadiri yapendavyo.
 
Mwendazake hakosi lawama kwenye hili. Alionyesha njia kama mwanzilishi, kisha akahakikisha ajaye anakuwa na nguvu kubwa kwa kuconsolidate power na kupora uchaguzi kuondoa upinzani bungeni.
 
Tatizo la dikteta wa kizimkazi kwanza ni muoga sana pili mjinga!
So wahuni wanamtumia kwa maslahi yao na yeye kwakuwa ni mjinga haelewi...anabung'aa tu mimacho!.
Ukisema wanamtumia kwa maslahi Yao, kina nani hao?

Hayo maslahi Yao, yeye hayumo?

Leo Zanzibar zinajengwa bandari mbili, uwanja mwingine mkubwa wa kisasa wa mpira, Barabara Lami kila mtaa, Ajira wamejaziwa za bara na za kwao, biashara imekuwa kubwa.

Hayo maslahi ambayo yeye hayumo ni yapi?
 
Lawama zimwendee jiwe
Yeye ndiye architecture wa kila kitu
Huyu tunamuonea tu
 
Akiondoka na huyu akija mwengine utakuja kumuona dikteta zaidi ya mama samia hayo ndo yalivo kijana
 
Ninyi mashetani, kila jambo linalohusu haki, kwenu inakuwa pumba maana kwenu jambo la maana ni udhulumaji wa haki za watu, na kila aina ya uovu mwingine.
Haki gani wewe umenyimwa ..au unaongelea ile haki ya upinde ? ile hapana hatuwezi kukupa haki ya kubutuliwa mtoto wa kiume.
 
Wakati wa utawala wa Jakaya Kikwete, kuna wakati baadhi ya watu walimwita ni dikteta, yeye akajibu kwa kuwauliza kama hao wanaosema kuwa yeye ni dikteta, wanaelewa maana ya udikteta. Akawauliza mmewahi kushuhudia udikteta nini?

Wakati wa utawala wa Hayati Magufuli, Tundu Lisu alimwita Magufuli kuwa ni dikteta uchwara, akimaanisha alionesha viashiria vya udikteta lakini hakuwa amefikia udikteta kamili. Lakini kwenye awamu hii, watanzania wanashuhudia udikteta kamili. Tujaribu kulinganisha udikteta uchwara na udikteta kamili.

1. Wakati wa utawala wa Hayati Magufuli, kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, mwaka 2019, wagombea wa CHADEMA, chama kikuu cha upinzani, karibia wote walienguliwa. Lakini wakati wa utawala wa Samia, msimamizi mkuu wa uchaguzi alimweka mkwe wake, wagombea wa CHADEMA karibia wote walienguliwa, wachache walioachwa, baadhi waliuawa, na hata wachache walioshioachwa, wakashinda uchaguzi, hawakutangazwa.

2. Kwa upande wa mgombea wa kiti cha Urais, Hayati Magufuli alimwacha hasimu wake Tundu Lisu kuwa mgombea, aliiacha CHADEMA ifante siasa na kampeni, japo kuna maeneo ilithibitika kuwa kura za Lisu ziliibiwa. Lakini kwenye utawala wa Samia, siyo tu Lisu amenyimwa haki ya kugombea, bali amefungwa na kutengenezewa kesi, kwa kupitia mahakama bandia, na Tume huru bandia ya Uchaguzi, CHADEMA imezuiwa kushiriki uchaguzi na kufanya shughuli za siasa.

3. Hayati Magufuli alipiga marufuku shughuli za siasa za vyama vya siasa baada ya uchaguzi na siyo wakati wa uchaguzi, lakini wakati utawala wa Samia, CHADEMA imezuiwa kufanya shughuli za siasa kipindi cha uchaguzi ili asiwe na mpinzani.

4. Wakati wa utawala wa Hayati Magufuli, muda usio wa uchaguzi, baadhi ya wakosoaji walitekwa kwa siri, na hawakuonekana mpaka leo. Lakini wakati wa Samia, viongozi wa CHADEMA na baadhi ya wakosoaji wamekuwa wakitekwa hadharani, wakati mwingine mbele ya vyombo vya ulinzi na usalama, bila hofu yoyote na watawala indirectly wakiunga mkono vitendo hivyo kwa kutoa kauli tata, kama vile 'kifo ni kifo tu', hakuna anayetekwa hizo ni drama tu; wanaotekwa na kupotezwa wametoroka madeni au wameenda kwa wapenzi wao. Ni watu wachache sana waliotekwa wakati wa utawala wa Hayati Magufuli, lakini chini ya Samia makumi ya watu wametekwa na ama kuuawa au kupotezwa.

5. Wakati wa Hayati Magufuli, hakuna mwanafamilia ywake yeyote aliyepewa jukumu maalum la kusimamia uovu kwa maslahi ya ndugu yake, lakini wakati wa Samia, Mchengerwa, mkwe wa Rais andiye aliyekuwa msimamizi wa TAMISEMI, ambayo ndiyo iliyosiamua na kuwezesha uovu wote wakati wa uchaguzi wa 2024. Na bado ana jukumu muhimu la uchaguzi bandia mwaka huu kwani wasimamuzi wote wa huo uchaguzi wapo chini yake.

Watanzania mlimwita Kikwete dikteta, Magufuli dikteta uchwara, leo ndiyo mnaoneshwa maana halisi ya udikteta.
Moja jumlisha moja sio mbili bali ni kumi na moja
IMG-20250814-WA0047.jpg
 
Back
Top Bottom