Hatima yetu tunayo mikokoni mwetu sisi wenyewe kuingoa CCM
TOKA MAKTABA :
Mistari ya wanamuziki wa Tanzania, vijana enzi ya Nyerere ambayo yanaelemisha hadi leo hii kizazi chetu kuhusu kujikomboa kutoka makucha ya mkoloni, hapa hata mkoloni mweusi aliye CCM anayekandamiza umma wa waTanzania bado ni mkoloni haijalishi rangi wala nini bado ni mkoloni :
Ukombozi wa Afrika - Afro 70 Band
View: https://m.youtube.com/watch?v=CusrvwChw3g
Mapinduzi ya Afrika
Ambayo Lengo lake
Ni Ukombozi kamili wa Mwafrika
Yanapingana Na Siasa,
Za Unyonyaji
Za Ukoloni Mambo Leo
Na Ubeberu
Afrika!
Shabaha Kuu Ya Mapinduzi Afrika,
Ni Kumkomboa Mwafrika Eeh,
Watalaamu Wa Ukombozi Ni Sisi Wenye,
Tunao Nyonywa, Kunyanyaswa
Na Kuonewa,
Eeh Afrika Bado Bara La Watu, Waliomo Katika Unyonge, Wa Kuoonewa Na Kunyanyaswa,
Kutakuwa Hakuna Taifa Lolote Ulimwenguni la Kutufundisha Afrika Jinsi Ya Kujiokoa ...
Wajibu Wa Kujikomboa,
Tupata Katika Mapambano Hayo Yenyewe .......