Kwa mara ya kwanza nimehisi kuwa na umuhimu

Kwa mara ya kwanza nimehisi kuwa na umuhimu

Maza akiwa na hela mzee atakula vizuri Ila Sasa ngoja baba awe na hela
Haya mambo ni magumu sana, kuna maza wengine wanaitumia kulipa visasi kwa waliyotendewa huko nyuma wengine ni roho mbaya tu amkomeshe mumewe,
 
So umefanya trading money vs baraka words. Ila hongera zako. Mie nimejikita hapo kuwa mzazi akanena baada ya kuwa naye amepata kitu
Sijafanya trading, ni kuhamisha pesa from usd acc to,,,,,,,, acc
 
Hii kila mtu anaweza kuiweka hapa. Nikaipakua nikaandika mtandao mwingine wa kijamiii kutafuta recognition. Weka iyo 8M ilivyoingia,ulivyoitoa 2M na ulivyoituma kwa maza, akaunti weka jina lako moja mengine uyafiche na id yako na yenyewe ufanye ivyo2 tupe jina lako na contract angalau tuone jina moja
Itafute kama hiyo uiweke hapa ukiweza nitumie acc yako ya bank nikupe laki 2 sasa hv
 
Itafute kama hiyo uiweke hapa ukiweza nitumie acc yako ya bank nikupe laki 2 sasa hv
Hata dola Mia haifiki iyo laki 2 yako. Nakuhurumia tuma kwanza alfu kumi tu niitume Kama iyo ,Ila mie Sina account ya 🏦,hela zangu Ni ndogo mno kuweka benki zinaishia mfuko wa Shari tu,Mana kubaruani nalipwa alfu kutwa ,nikitoa kula na nauli nabakiaa na alfu 2 tu pee day
 
Hili ni tatizo sana Kwa watoto wa kiume wanajitakia laana ambayo Haina msingi wowote , Baba aliyekulea hata kama alikufanyia vibaya muheshimu na umpende hakuna njia ya mkato kama umefanikiwa kupata kidogo . Watumie wote kiasi sawa

Hapa ungetuma 1m Kwa Baba na 1m Kwa mama baraka hazitoki upande Mmoja

Elewa watoto wako na wewe watakutenga hivyo hivyo unavyofanya

Fanyeni mambo ya kiume mwanaume , mwanaume unakuwaje na kinyongo ???

Mwanaume umekwazwa ongea yaishe iweke akili yako ktk kutafuta achana na Nia ovu

Wanaume tunatengwa na watoto kwa sababu sisi tulianza kuwatenga wazazi

Hata kama Baba yako ni mwingine siyo yule alokulea hakikisha yeye ndiyo alokulea mpe heshima yake

Naanza Rasmi harakati za kielimisha watoto wa kiume
 
Hakuna moment nzuri kama kumsaidia mzazi hata Kwa kidogo...huwa wanatoa baraka sana
 
Baada ya kumaliza Chuo mwaka jana life ikapiga vibaya mno, kila muda nilikuwa nawaza jinsi gani nitasaidia familia yangu (Ni mtoto wa kiume mkubwa) Ilikuwa inauma sana pale ambapo unaamka asubuhi huna cha kufanya hadi kuna muda unahisi kama kifua kinabana.

Kuna muda nakaa najitafakari naona kama ni mzigo home, but hakuna aliyewahi niambia, sister kuna muda mshahara ukitoka ananitoa laki basi maisha yanaenda.

Mwanzoni mwa mwaka huu kuna mchongo nikaupata katika harakati za kushughulikia ili utiki, nikawa naingia katika mzozo sana na mzee maana mara nyingi nilikuwa narudi usiku anamind, ananisema ila kwa upande wangu inaniuma lakini nakaza ili isionekane kama imeuma (akaanza kuona kama namdharau) sasa kuna muda huna nauli kuomba siwezi so nachukua bike kutoka home hadi kwenye michakato as usual narudi usiku.

Kwenye kuhangaika hivyo mchongo ukatiki nikatumiwa mkataba nikasign nikaenda kazini, nikaona afadhali nimetoka home, mchongo unalipa fresh tu, silipi kodi wala bills kama maji, umeme na utilities zingine, na ni apartment nzuri unyama ni mwingi.

Leo account imesoma kwa newhires wote mzigo umesoma almost M 8, nikatoa M2 nimewatumia home, bi mkubwa ameshukuru mnooo, kuna ile feeling ya kuwa Now na wewe ni wa muhimu, sijawahi jisikia vizuri kama leo, ameninenea maneno ya Baraka hadi nikahisi zinajaa physically. Leo na mimi nimehisi ni wa muhimu.
Bado ipo na ule mchongo mwanangu!!
Najua saizi una ndinga ushasahau kama uli haso.

Nataka unishauri mambo ya magari ! ushauri kutoka kwa muhangaikaji huwa unanoga sana
 
Back
Top Bottom