Kwa mara ya kwanza Serikali sasa kupata 75% ya mapato ghafi ya mafuta na gesi

23 November 2022
Mtwara, Tanzania

Bomba la gesi lenye urefu wa km 35 toka Ntorya hadi Madimba kujengwa

Bomba hilo la kusafirisha gesi asilia kutoka Ntorya kwenda katika kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba, litahusisha kuondolewa kwa wananchi 253 ambao wameorodheshwa Kwa ajili ya kulipwa fidia.


Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mh. Dunstan Kyobya ametoa agizo hilo leo Novemba 23, 2022 katika uzinduzi wa zoezi la uhakiki wa mwisho wa wahusika ambao bomba hilo lenye urefu wa km 35 linatarajiwa kupita, uzinduzi ambao umefanyika katika kijiji cha Namahyakata kata ya Nanguruwe wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya amewataka watendaji katika kata 4 na vijiji 11 vilivyopo katika maeneo ambayo yatakayohusika katika ujenzi wa bomba la gesi kufanya uhakiki wa kina wa wananchi ambao watalipwa fidia kupisha ujenzi wa bomba hilo.


More info :

IPPMEDIA
https://www.ippmedia.com › news
TPDC, gas explorer in refinery logistics talks

6 Jul 2022 — HOW to transport natural gas discovered at Ntorya fields in Ruvuma Region to the Madimba processing plant within the Mtwara Mikindani .....
 
YEAR 2017

Ntorya 1, Ntorya 2 and Ntorya 3 wells in Ruvuma basin Tanzania

Apart from LNG gas, now in the near future there is a big potential for establishing heavy industries the likes of fertiliser and petrochemical in Tanzania ... with huge markets in Asia and other parts of the world..
 
Hii mikataba inakuwaga siri za nchi, wananchi hawawezi kujua kilichosainiwa.
 
Na yeye amepata ngapi
 
Leo tarehe 25/11/2022 tunafanya hafla ya uwekaji saini katika mkataba wa nyongeza wa mkataba wa awali wa uzalishaji na ugawanaji mapato wa Kitalu cha Ruvuma baada ya kukamilika kwa majadiliano baina ya Timu ya majadiliano ya Serikali na wawekezaji.
Statement za hivi ndizo hutufanya tunyolewe kikavu kwa kipande cha chupa
 

ARA Petroleum Tanzania Ltd ni ya Serikali? Sijawahi sikia hiyo kampuni au shirika, sisi tunajua TPDC ndio shirika la serikali, sasa ARA Petroleum Tz Ltd au APT inatoka wapi?

Mmmhhh..!! Kwanini TPDC isiingie mkataba na hao Aminex? 😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢
 
Kusainiwa kwa mkataba huu wa nyongeza ni hatua kubwa katika maandalizi ya kuendeleza gesi iliyogunduliwa na hivyo kuongeza uzalishaji wa gesi asilia nchini.
Kikwete naye alisema hivihivi lakini hadi leo hatuoni faida ya gesi hiyo zaidi ya kukosa umeme wa uhakika, kuendelea kuteketezwa kwa misitu na kuwaneemesha wachache na familia zao
 
Tutolee ujinga na upumbavu,yaani mtu awekeze tril 70 alafu akupe faida ya 75% ya mapato ghafi(gross profit)??!!!😂😂😂😂huo ni wenda wazimu.
 
faida ya 75% ya mapato ghafi(gross profit)??!!!😂😂😂😂huo ni wenda wazimu.

Mh. January Makamba anasema jambo hili (mkataba) ni la kihistoria halijapata kutokea Tanzania ni mara ya kwanza kufanikiwa pakubwa nchi na raia wake wafaidi matunda ya tunu hii ya maliasili yaani gesi, mapato, ajira za kumwaga, viwanda vikubwa vya mbolea, viwanda vya mazao ya petrochemical kama matairi, sabuni za unga n.k vitafunguliwa kusini mwa Tanzania yaani Lindi na Mtwara yetu.

Petrochemicals, produced from petroleum, can be classified as olefins and aromatics [70]. Olefins include ethylene, propylene, and butadiene which are raw materials for making plastics. Aromatics include benzene, toluene, and xylene which are raw materials for making dyes and synthetic detergents.
 
Acha kushiriki dhambi isiyo ya lazima.Toka lini mzungu akawa mjinga kiasi hicho au anamuogopa Makamba??Bora ukaa kimya maisha yakaenda tukafa tukawaachia linchi.Maana wao wanayoyafanya wanadhani nchi hii ni yao na familia zao ndo maana wanajiita watoto wa mjini utadhani wao hawafi au hawatakufa.
 
CHADEMA KANDA YA KUSINI
Maliasili za nchi haziwafaidishi wananchi Ruangwa, Tarime, Shinyanga n.k kote wananchi ingawa ardhi yao ina madini ya thamani lakini ....
 
WA ULAYA (EU) WAIPA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 380

UMOJA WA ULAYA (EU) WAIPA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 380​

Bashir Nkoromo Wednesday, October 26, 2022 ,featured ,Habari

Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam



Picha : Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiteta jambo na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Kamisheni ya Ulaya Bi. Jutta Urpilainen, baadaa ya kuzindua mpango wa pili wa msaada wa Umoja wa Ulaya kwa Tanzania wenye thamani ya euro milioni 166 sawa na shilingi bilioni 380 kwa ajili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, Jijini Dar es Salaam

Umoja wa Ulaya (EU) umeipatia Tanzania msaada wa euro milioni 166 sawa na takribani shilingi za Tanzania bilioni 380 ajili ya utekelezaji wa miradi mitatu ikiwemo kuibua fursa zitokanazo na bahari (Uchumi wa Buluu), sekta Jumuishi ya fedha na kuimarisha ushirikiano.

Msaada huo umetangazwa leo tarehe 26 Oktoba, 2022 Jijini Dar es Salaam mbele ya wanahabari na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Kamisheni ya Ulaya Mhe. Jutta Urpilainen na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Dkt. Nchemba alisema kuwa msaada huo umeidhinishwa na Umoja wa Ulaya katika mwaka wa pili wa utekelezaji wa ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya kwa kipindi cha miaka saba kuanzia mwaka 2021 hadi 2027, ambapo katika awamu ya kwanza, tarehe 22 Machi, 2022, Serikali ilipokea msaada wa euro milioni 180, sawa na zaidi ya shilingi za Tanzania bilioni 400.

Alifafanua kuwa katika awamu hiyo ya pili ya msaada wa euro milioni 166, mradi wa uchumi wa buluu umetengewa euro milioni 110, mradiwa kuimarisha sekta ya fedha (euro milioni 50) na mradi wa kuimarisha ushirikiano umetengewa euro milioni 6.

“Fedha hizi ni sehemu ya matokeo ya ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, iliyofanyika mwezi Februari, 2022 jijini Brussels, nchini Ubelgiji ambapo Umoja huo ulitangaza kuipatia Tanzania msaada wa kiasi cha euro milioni 426 kwa kipindi cha miaka minne ijayo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini” alisema Dkt. Nchemba

Dkt. Nchemba aliushukuru Umoja wa Ulaya kwa msaada huo mkubwa ambao ameahidi kuwa miradi itakayonufaika na fedha hizo itatekelezwa kwa viwango na kama ilivyokusudiwa kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa haraka.

Alisema Tanzania inathamini kwa kiwango kikubwa ushirikiano uliopo kati yake na Umoja wa Ulaya tangu uanzishwe mwaka 1975 ambapo hadi sasa Umoja huo umetoa misaada na mikopo yenye thamani ya euro bilioni 2.4 sawa na takribani shilingi trilioni 5.9 na mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya euro milioni 270.9 sawa na shilingi bilioni 706.5.

Kwa upande wake, Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Kamisheni ya Ulaya, Mhe. Jutta Urpilainen, alisema Tanzania ni mshirika muhimu wa Umoja wa Ulaya ikiwa ni nguzo imara inayounganisha Mashariki na Kusini mwa Afrika na na kuipongeza kwa kujiimarisha katika nafasi ya uchumi wa kati.
kuwa Umoja huo unafurahishwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi yaliyofikiwa nchini na kwamba wako tayari kuendelea kutoa misaada ili kufanikisha agenda hiyo.

Alisema kuwa msaada huo wa euro milioni 166 umelenga kuimarisha shughuli za uchumi wa buluu uliolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuvumbua fursa za kiuchumi zinazopatikana kupitia bahari ili taifa na jamii inayozunguka fukwe za bahari iweze kunufaika kupitia uvuvi, utalii wa kiikolojia, huku ikihifadhi mazingira na kukuza ajira.
Alisema manufaa mengine ya mpango huo ni kuiwezesha jamii kuzifikia fursa za kiuchumi kupitia taasisi za fedha, uwekezaji wenye lengo la kuchochea mapinduzi ya kilimo, uchumi jumuishi na maendeleo endelevu nchini Tanzania, kuboresha ujuzi wa wananchi na kuboresha mazingira ya sheria mbalimbali.

“Msaada huo umelenga kutekeleza mkakati wa Umoja wa Ulaya ujulikanao kama The Global getway, wenye lengo la kuboresha mifumo ya kidijitali, mabadiliko ya tabianchi, afya, elimu, miundombinu ya usafiri na masuala ya utafiti kwa kuzishirikisha sekta ya umma na sekta binafsi nchini Tanzania” alisema Mhe. Urpilainen

“Watekelezaji wa miradi hii watafanyakazi bega kwa bega na Serikali kutekeleza malengo hayo kwa kutumia misaada ya fedha kutoka Umoja wa Ulaya ili kuongeza uwekezaji zaidi hapa nchini” aliongeza Mhe. Urpilainen.

Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Kamisheni ya Ulaya, Mhe. Jutta Urpilainen, yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na baadae ataelekea nchini Malawi kwa ziara kama hiyo.
 
Hongera Serikali na hongera Makamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…