Kwa mara ya kwanza tangu ipate Uhuru, Senegal imeanza kuzalisha na kusambaza mafuta yake yenyewe! Tani 90,000 zazalishwa

Gaddadi yeye mwenyewe aliingia kwa mapinduzi, kwanini yeye kupinduliwa iwe ni kuchukiwa na wazungu?

Mbona alipopindua yule Mfalme haikusemwa Mfalme anachukiwa na wazungu wala Gaddafi anapendwa na wazungu. Mtu kaishi madarakani miaka zaidi ya 40, kachokwa. Raia wameingia mtaani kupambana naye kabla wazungu hawajaja.

Vietnam ambako Wamarekani walienda wakakuta raia wanaipenda serikali waliambulia pua, Wafaransa walitoka kapa, Wachina walikuja baada ya Wamarekani wakatoka kapa. Afghanistan walienda Soviets wakafeli, wakakaa Wamarekani 20 yrs wakaondoka mwezi huohuo Taleban wakarudi.

Huwezi pigana na serikali inayokubalika kiraia ukashinda kizembe. Nenda Misri jifanye sijui Mchina sijui Mmarekani ulete chokochoko uone kama nchi itakufa.
 
Mkuu ulitaka Gaddafi atoke madarakani kiulaini tu bila ku
pinga?
Point yangu ni kwamba vita huwa inaharibu uchumi wa nchi, hata Tanzania tulikua na haki kumng'oa Idd Amin ila ndio hivyo ikaua uchumi wetu. Kwahiyo vita ndo iliyoharibu Libya sio wazungu!! Mbona Mugabe alichukiwa na wazungu ila Zimbabwe sio magofu? Sababu hakutaka vita alitoka kistaarabu tu. Kwahiyo funzo ni kwamba hata tukosane vipi tusibebe bunduki maana hata ukishinda vita mnarithi magofu tu.
 
na Walibya walikuwa wanampenda Gaddafi
We umejuaje hili? Nakuhakikishia kura zingepigwa ungeshangaa Gadaffi anaanguka. Ni sawa tu na Nkrumah alikuwa anakubalika sana ila wananchi walimchoka same to Haile selassie, kama angependwa hivyo niamini mimi hakuna namna waaasi wangepewa ushirikiano ule.

Suluhisho ni kuepuka vita Kama suluhu ya mgogoro, ni kheri mmoja apishe ila vita inaharibu uchumi bila kujali mzungu anakupenda au hakupendi.
 
Nimekuelewa mkuu👏👏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…