T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Gaddadi yeye mwenyewe aliingia kwa mapinduzi, kwanini yeye kupinduliwa iwe ni kuchukiwa na wazungu?Mkuu ulitaka Gaddafi atoke madarakani kiulaini tu bila ku
pinga?
Tofauti ya nchi hizo ulizozitaja na Libya ni raia wa nchi hizo walikuwa against watawala wao, na Walibya walikuwa wanampenda Gaddafi
Choko choko za Western ndio kisababishi cha kumtoa madarakani
Ukiwa tofauti na Western watakupinga kwa hari na mali
Mbona alipopindua yule Mfalme haikusemwa Mfalme anachukiwa na wazungu wala Gaddafi anapendwa na wazungu. Mtu kaishi madarakani miaka zaidi ya 40, kachokwa. Raia wameingia mtaani kupambana naye kabla wazungu hawajaja.
Vietnam ambako Wamarekani walienda wakakuta raia wanaipenda serikali waliambulia pua, Wafaransa walitoka kapa, Wachina walikuja baada ya Wamarekani wakatoka kapa. Afghanistan walienda Soviets wakafeli, wakakaa Wamarekani 20 yrs wakaondoka mwezi huohuo Taleban wakarudi.
Huwezi pigana na serikali inayokubalika kiraia ukashinda kizembe. Nenda Misri jifanye sijui Mchina sijui Mmarekani ulete chokochoko uone kama nchi itakufa.