Criss
JF-Expert Member
- Mar 19, 2011
- 1,959
- 3,172
Mimi ni mwana CCM kiasili kwa maana ya kuwakuta wazazi wangu wakihudumu kama wanachama na viongozi wa Taifa langu kwa upande wa chama cha mapinduzi
Binafsi nitajiona ninazo sababu nyingi ambazo kwa unyenyekevu wa ndani kabisa wa moyo wangu najiona nisiposhiriki kwenye maandamano ya October 29 moyo wangu utakuwa nikama unavuja damu kwa kosa la usaliti kwa Taifa langu...sipo tayari kulisaliti Taifa langu .
Nipo tayari kwa malipo yatakayonigharimu hata uhai wangu maana hata nisiposhiriki naweza kukutwa na lolote kikiwemo kifo ,Bora nife kwa kumpambania Rais wangu kuondolewa kwenye kiti cha Urais kinachomfanya aje kukosa pepo.
Nimegoma kuzisema sababu zinazonipelekea kuandamana kwangu maana sababu ni zangu ,ikiwa na wewe uko na zako usisite kuungana pamoja kwenye ukombozi wa Taifa letu.
Mama anaweza kuwa hajaua na haui.
Mama anaweza kuwa hatesi wala kuwatuma watu kututesa
Mama anaweza kuwa habani uhuru wa vyombo vya habari
Mama anaweza kuwa haibi na hatumi watu kuiba.
Mama inawezekana hata ile siku aliyoiita katiba yetu ya Jamuhuri ya Muungano ni kakijitabu tu hakusema kwakumaanisha maana ndiyo iliyosababisha leo yeye awe Rais wetu.
Yawezekana Rais wetu hata akawa ameombwa tu kama siyo kushinikizwa aendelee kuiomba nafasi ya Urais lakini pengine wapo watu wanaotaka aendelee kuwapo kitini kwa maslahi yao.
Lakini kwakuwa yote yanayotokea na Mama hachukui hatua ,kwa nia njema kabisa nashawishika kuingia barabarani ili kumnusuru Mama aondoke kitini ili Taifa letu lipone .
Mama anapaswa kupewa support ya kumuondoa kwenye mikono ya wenye dhambi ,kutokuingia barabarani kutamsababishia Mama na Rais wetu mpendwa kuendelea kuonekana msaliti mbele ya sura za watanzania wanyonge .
Tumechoka kulia misiba ya watu ambao hatujui kama wapo hai au wameshakufa kwa kuuwawa .
Tumechoka kuona kikundi cha watu wachache wakineemeka katikati ya kundi la watanzania masikini wasiyojua hata pakuingilia ,tumechoka kuona kila anaesimama kututetea anaokotwa nakuwekwa korokoloni kwa amrinzao , tumechoka kupigwa virungu na askari wanaoendeaha maisha kwa Kodi zetu .
Tumechoka kuitwa majina tusiyoyastahili kila pale tunapoamua kusimama na kukemea uovu unaolitafuna Taifa letu ,tumechoka kuonekana wasaliti wa Taifa letu maana kila anaekosoa anaonekana ni Chadema na adui mkuu ambao kupotezwa ndiyo adhabu tunazostahili .
Kwa mara ya kwanza nimedhamiria kuingia Barabarani kumsaidia Mama na Rais wangu aondoke madarakani.