Kwa mara ya kwanza toka 2018 nakuwa upande wa Mbowe tena

love life live life

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2021
Posts
2,584
Reaction score
3,051
Kwanza nianze kwa kukupa pole kaka na kiongozi wangu mh. Mbowe kwa kusota lupango(ukonga)
kwa zaidi ya siku 226.

Nakukabirisha mtaani kwa nderemo na vifijo tele mimi magufulist a.k.a sukuma gang mtoto yatima,
uje tule na kunywa pamoja katika kipindi hiki kilicho baki cha uhai wetu.

Zaidi sana tuendeleze mapambano ya kudai katika mpya na tume huru bila kuchoka ili kkujenga demokrasia yetu,
Pia nina hakika kuwa kama umeweza kukaa gerezani kwa siku 226 bila kuwapigia magoti watesi wako na imani
kubwa na wewe(Mbowe, Mwamba) utatuvusha(mwamba tuvushe) katika kipindi hiki kwani wewe ni Mandela wa wakati wetu.

Yote tisa kumi ile sera yetu chadema ya serikali ya majimbo kwa Tanzania, ina umhimu kuliko
wakati wotewote. Zanzibari imekuwa chato ya awamu ya sita mara elfu kuliko ya Magufuli.

Mengine tutaongea ukiwa umepumzika karibu uraini japo roho na akili yako haikuwahi kuwa ukonga ni mwili tu.

Mwisho kabisa Mandela alisema siku anatoka gerezani kuwa atatumia kipindi cha uhai wake kilichobaki kuwatumikia wananchi wake, Mbowe njoo ututumikie tena.

Waliokuweka gerezani wamekufanya umekuwa imara kuliko wakati wowote wa maisha yako pengine uhai wako.

Nitakuja kukupa salamu zako ukiwa nyumbani Hai.

NB: katika mwanasiasa wa karne yetu ni Mbowe na katika kiongozi wa karne yetu ni Magufuli.

ukishika dola ntakupa jina jipya kama Ibrahim alivyopewa jina jipya.
 
Mbowe ni mwisho wa matatizo amefanya kazi kubwa na ni mwamba kweli kweli
 
Mm kusema kweri sikua mfuasi wa mbowe kabisa,lakini nilipo sikia amekamatwa kwa kesi ya ugaidi,nika badiri gia angani kwa sasa nipo upande wa mbowe.
 
Cry more mataga, ila ni vizuri sana kama hata watu wa aina yako mmeanza kuona umuhimu wa katiba mpya.
Hiki ndio tunahitaji na sio kuwaponda watu walioanza kurudi kwenye sense zao..
 
Uhaligani rafiki yangu Elitweege, hatimae mwamba yuko Tena huru, ulimeombea mabaya kadiri ulivyoweza ila Mungu amesimama upande wake na hatimae amewashinda watesi wake. Tuungane pamoja kuhimiza upendo,haki na amani Kwa wote.
Lazima tuwe na upendo i lovee your generosity.
 
Tunahitaji umoja sasa sio utengano ndugu.
Na kwa umoja tutashinda inshallah.

Hapo mwisho unatakiwa uandike hivi; Insha Allah! Badala ya inshallah!

Anyway, kuna Sheikh wangu mmoja hivi, alinifuata pm na kunielekeza hivyo. Hivyo ni wajibu wangu na mimi kuwaelekeza ndugu wengine.
 
Tusi-enternentain separability mkuu.
MATAGA ni watanzania kama sisi one day watakuwa upande sahihi.
 
Katika vitu ambavyo huwezi kuvificha basi kikubwa ni ukweli ni mda tu huwa unaamua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…