Kwa masharti haya msahau uchaguzi huru TFF

Kwa masharti haya msahau uchaguzi huru TFF

BASIASI

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Posts
9,732
Reaction score
5,006
Jana nikiwa nasikiliza kipindi kimoja cha michezo nilishtuka sana, mmoja wagombea alilalamikia

Hiki kipengele naamini viko vingi vya kubadilisha

Kila mgombea anahitaji wadhamini si chini ya watano kila mkoa na kama mmoja wa wagombea eg karia akishapita Moshi Mwakagenda haruhusiwi kupita tena

Nini maana yake Kama kuna wagombea 12 urais, means kunahitajika mikoa 12*5

Hapo ndipo utajua PCCB iliundwa kwa ajili gani haya masheria mengine nI magumu sana yanachangia rushwa kwenye uchaguzi

Wajumbe wanauwezo wakuangalia nani mwenye mzigo mrefu ndiye wamdhamini Kama wewe kashunda Nani Kama mm ndugu nakushauri tangaza tu

#Nimejiondoa

#Jambo lingine wagombea wamelalamika sana jana kuna michezoo inafanywa wale wagombea wengine wanasindikiza wenzao

Sasa kwenye kuchuja huwa wanahaoikishiwa kuwemo mpaka last stage

Hapoondipoo utasiki

#NIMEAMUAKUJIONDOA

Sababuuu anaona my Fulani anatoshaa

TFF, PCCB haka kamchrzo kathibitiwe kabaki historia

Tunaomba UCHAGUZI wa huru na haki thanks

#kaziiendeleeeee
 
Ukiwa Rais TFF lazima uondolewe kwa mabavu tu. Inaonekana ndo nature ya mashirikisho ya mpira duniani. Refer Blatter, Ndolanga, Malinzi bila kulazimishwa wasingeondoka kwenye chaguzi!

KARIA atashinda tena TFF hata mara 10 akiachiwa. SwalI ni HILO lina AFYA kwa mpira wa Tanzania?
Kama jibu ni ndiyo, haya TAYARI KARIA KASHINDA, kama hapana lazima aondolewe kwa ZENGWE iwe la Serikali au Vinginevyo!
 
Ally Mayay alijaribu mwaka ule wajumbe wakamwambia "live" mkono mtupu haulambwi, tumetoka mikoani kuja kupiga kura DSM hatuwezi kurudi nyumbani mifuko mitupu, wakamtosa akashinda Karia.

Mwaka huu nao utakuwa hivyo hivyo tu, kama hauna pesa za kuhonga wajumbe usiende kugombea TFF, hiyo pesa bora uchome mbuzi ule.

Wale wajumbe wakija kupiga kura huwa wanajua hawatarudi walikotoka mifuko mitupu, sasa wewe nenda kajidanganye eti unajua kuchambua mpira vizuri kama karanga halafu uone kitachokupata.
 
Huyu msomali aliyemponda Tundu Lissu ili amfurahishe Magufuli. Hii TFF hamna kitu, mpira wa Tanzania hautakaa uendelee.
 
Ally Mayay alijaribu mwaka ule wajumbe wakamwambia "live" mkono mtupu haulambwi, tumetoka mikoani kuja kupiga kura DSM hatuwezi kurudi nyumbani mifuko mitupu, wakamtosa akashinda Karia...
Ndugu yangu ni kweli uliyosema na umeeleweka

Ila naomba kuuliza wewe na wachangiaji wengine KUNA ALIYEMUELEWA mtoa post?

Mgombea inatakiwa upate wadhamini wa5 KILA MKOA,na mmoja akishapata wadhamini mkoa huo mwingine haruhusiwi kupata sasa manaake probability ni kwamba hakuna uwezekano wa kuwa na wagombea wawili mbona?? Kama mgombea wa kwanza akapata wadhamini 5 kila mkoa mgombea wa pili anapata wapi wadhamini?? Nchi jirani au??😂😂
 
Ndugu yangu ni kweli uliyosema na umeeleweka

Ila naomba kuuliza wewe na wachangiaji wengine KUNA ALIYEMUELEWA mtoa post?...
WenWena umeshajij ibu.

Kama wewe UKIPITA mbeya Bujibuji hatakiwi KUPITA huko AENDE mkoa.mwimgine
 
Ndugu yangu ni kweli uliyosema na umeeleweka

Ila naomba kuuliza wewe na wachangiaji wengine KUNA ALIYEMUELEWA mtoa post?..
Hicho kipengele kimewekwa kwa minajili hiyo hiyo - Rushwa, unaweza wewe kwenda kutafuta wadhamini mkoa fulani wakakunyima hata kama hakuna mgombea mwingine aliyepita hapo, wajumbe wamegeuzwa miungu watu wanawatawala wagombea.

Wanasubiri atakaekuja na pesa ndio wampe huo udhamini, unaweza zunguka hii Tanzania mpaka uone kizunguzungu na muda wa kutafuta wadhamini ukiisha hujawapata ndio umejitoa kwenye uchaguzi automatically.

Kanuni za kipuuzi ziko hapo miaka yote zinapigiwa kelele lakini jamaa hawana habari bado zipo tu, ile TFF ni ujinga na ujanja ujanja mwingi ndio maana hata kuandaa ratiba ya ligi hawawezi viporo kila msimu.
 
Kila mgombea anahitaji wadhamini SI chini ya watano kila mkoa na kama mmoja wa wagombea eg karia akishapita Moshi mwakagenda haruhusiwi kupita tena

Hicho kipengele kimewekwa kwa minajili hiyo hiyo - Rushwa, unaweza wewe kwenda kutafuta wadhamini mkoa fulani wakakunyima hata kama hakuna mgombea mwingine aliyepita hapo, wajumbe wamegeuzwa miungu watu wanawatawala wagombea.

Wanasubiri atakaekuja na pesa ndio wampe huo udhamini, unaweza zunguka hii Tanzania mpaka uone kizunguzungu na muda wa kutafuta wadhamini ukiisha hujawapata ndio umejitoa kwenye uchaguzi automatically.

Kanuni za kipuuzi ziko hapo miaka yote zinapigiwa kelele lakini jamaa hawana habari bado zipo tu, ile TFF ni ujinga na ujanja ujanja mwingi ndio maana hata kuandaa ratiba ya ligi hawawezi viporo kila msimu.
Bwana sijui kama umenielewa mkuu. Ni kwamba HAIWEZEKANI


Kwamba kila mgombea apate wadhamini KILA MKOA na hauruhusiwi kupata wadhamini ambapo mwenzako kapata wadhamini mbona hizo statement zinajifanyia "negation" zenyewe??!

Ni sawa na kusema awe mgombea mmoja tu,na mbona tunaonaga wanajua wagombea wengi kwenye chaguzi???

Hapo ndio ambapo sijaelewa aidha hii statement imekosewa au haipo labda tukione hicho kipengele kwenye katiba ndo ntaelewa.

Najua fitna zinafanyikaga ila sio kwamba kanuni inakataza kuwa na wagombea zaidi ya mmoja

Labda ningesikia kwamba mgombea apate wadhamini at least mkoa mmoja na hairuhusiwi kupata wadhamini mkoa alikopata mwenzako. Manaake hiyo unafungua njia kuwa na wagombea 30+ sasa ukisema KILA MKOA na hauruhusiwi kupata udhamini mkoa aliopata wadhamini mwenzako manaake uwezekano ni kupata mgombea mmoja tu au msiwe na mgombea kabisa(kama mmoja akapata wadhamini mikoa6 mwingine 15 mwingine 10) nani atakua mgombea hapo??? Mie sijaelewa kabisa labda kichwa kizito
 
Huyo kiongozi mzito serikalini aliyemuweka Karia asome alama za nyakati na kumtosa Msomali.
Shida kubwa ni kwamba Rais qa TFF lazima mwana Mikia. Atafute mwingine angalau asafishe upuuzi wake. Akiendelea kung'ang'aniza awe Karia tena, ataumbuka si muda mrefu!
 
Ndugu yangu ni kweli uliyosema na umeeleweka

Ila naomba kuuliza wewe na wachangiaji wengine KUNA ALIYEMUELEWA mtoa post?

Mgombea inatakiwa upate wadhamini wa5 KILA MKOA,na mmoja akishapata wadhamini mkoa huo mwingine haruhusiwi kupata sasa manaake probability ni kwamba hakuna uwezekano wa kuwa na wagombea wawili mbona?? Kama mgombea wa kwanza akapata wadhamini 5 kila mkoa mgombea wa pili anapata wapi wadhamini?? Nchi jirani au??[emoji23][emoji23]
Ila jaman sheria gani hii dhaaaa
Hapa mbona karia kashapita waziwazi
Jamaa wanajisumbua Tu kurudisha
Hzo form pesa Yao Bora wakanywe bia
 
Back
Top Bottom